Nyafwili
JF-Expert Member
- Nov 27, 2023
- 4,240
- 10,561
𝗪akazi wa wilaya ya ludewa mkoa wa njombe wamelalamika kugongwa 𝗠IHURI kimiujiza katika Maeneo ya mgongoni, huku wakielekeza tuhuma hizo kwa baadhi ya wazee wa kijiji cha kilima hewa.
Wamelazimika kuitisha mkutano maalumu ili kujadili suala hilo ambapo wamesema, awali tatizo hilo liliripotiwa na wakazi wa kata jirani ya Lupingu wilayani humo na baada ya kupigiwa kelele, tatizo hilo lilikoma, lakini hivi sasa limehamia katika kijiji cha kilima hewa, huku wakiwataka wazee wanaotuhumiwa kurudisha mhuri huo waliopo utoa.
Bado wahusika wa matukio ya kugonga watu mihuri kimiujiza, hawajatajwa moja kwa moja, licha ya kwamba wanaohusishwa ni baadhi ya wazee waliosamehewa kufanya shughuli za maendeleo na serikali kutoka na umri wao.
Kiongozi wa wakazi wa kitongoji cha kilima hewa, Isaya Mwailamula amemwambia mwandishi wetu kuwa mkutano huo umeitishwa maalumu kujadili malalamiko ya uwepo wa mihuri ya kimiujiza kwa wakazi wa eneo hilo, baadaya kupokea malalamiko ya mara kwa mara kutoka kwa watu wake.
Mkutano huo ulihudhuriwa na kiongozi wa dini wa kanisa la TAG, alietambuliwa kwa jina la Martin Kabojoka, ambae alishauri suala hilo lisimamiwe na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ili hatma ifanyike na kura zipigwe kuwabaini wahusika wa matukio hayo.
Hata hivyo bado haijawekwa wazi madhara ya Muhuri huo unaodaiwa kuwa ni wa kichawi, licha ya kwamba hofu inaonekana kutanda miongoni mwa wakazi wa kijiji cha kilimahewa huko wilayani ludewa.
Bado hadi sasa hakuna kauli yeyote iliyotolewa na mamlaka za serikali ngazi ya wilaya kuhusu tukio hilo la watu kugongwa mihuri ya kichawi kimiujiza.
Cc : Radio Free Africa Online