LGE2024 Njombe: Wananchi wataka wanasiasa kufanya kampeni za kistaarabu na zisizo na matusi kwenye Uchaguzi wa Serikali za mitaa

LGE2024 Njombe: Wananchi wataka wanasiasa kufanya kampeni za kistaarabu na zisizo na matusi kwenye Uchaguzi wa Serikali za mitaa

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Wakati zoezi la uchukuaji fomu za kugombea uenyekiti na ujumbe wa serikali za mitaa likiendelea nchini, wakazi wa Mtaa wa Kambarage mjini Njombe wameomba kampeni za kistaarabu zisizo na lugha za matusi pindi zitakapoanza.

Wananchi hao wamesisitiza umuhimu wa kampeni zenye kujenga umoja na maendeleo kwa ajili ya ustawi wa mtaa wao.

Mgombea wa nafasi ya uenyekiti kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Emmanuel Kayombo, pamoja na wajumbe wake, walichukua fomu huku wakiwa na matumaini ya kuchaguliwa ili kusaidia kutatua changamoto mbalimbali, hususan usimamizi wa miradi ya maendeleo na masuala ya kifedha.

Soma pia: RC Njombe awaongoza Wananchi kujiandikisha Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

Kwa upande wake, Nicodemus Funi, ambaye ni msimamizi msaidizi wa uchaguzi katika mtaa huo, alieleza kuwa hadi sasa ni vyama viwili tu, CCM na CHADEMA, ambavyo vimechukua fomu za kugombea.

Uplands.png

Wanachama wa CHADEMA waliomsindikiza mgombea wao katika zoezi hilo wameonyesha imani kubwa kwake, wakiamini kuwa atachangia kuleta maendeleo ya kweli kwa wananchi wa Kambarage.

Source: Uplands FM
 
Back
Top Bottom