Pre GE2025 Njombe: Waziri Jafo ataka mradi makaa ya mawe ukamilike haraka

Pre GE2025 Njombe: Waziri Jafo ataka mradi makaa ya mawe ukamilike haraka

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
NJOMBE: WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Dk Selemani Jafo ameliagiza Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) kukamilisha majadiliano na Mwekezaji wa Mradi wa Makaa ya Mawe Ketawaka Kampuni ya MM Steel Resource Public Ltd( MMSR) kufikia makubaliano ndani ya wiki tatu ili utekelezaji wa mradi huo uanze.

Vilevile, Waziri Jafo ameliagiza shirika hilo kushirikiana na wadau wake mbalimbali katika mradi wa Makaa ya Mawe Mchuchuma na Katewaka kujenga majengo mawili katika Shule ya Msingi Nkomang'ombe iliyopo katika maeneo ya miradi hiyo.

Pia soma: Pre GE2025 Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Waziri Jafo ametoa agizo hilo Februari 17, 2025 wakati wa ziara yake mkoani Njombe katika Wilaya ya Ludewa yenye lengo la kukagua maendeleo ya utekelezaji wa Mradi Mchuchuma na Ketawaka, Liganga na Maganga Matitu pamoja na kuongea na wananchi wa maeneo hayo.
Screenshot 2025-02-18 125229.png
 
Mwambieni hakuna mwekezaji Mhindi au Muarabu kwenye madini au mafuta na gas tena kampuni yenyewe MM steel.
Uwekezaji wa Mhindi, Muarabu na Mchina ni hatari kwa ustawi wa nchi na maisha ya watu.

Hao wanachangamkia dili la kustock makaa Ulaya baada ya WaEurope kutokuwa na trust na Russia anayewasambazia gas. ULAYA wanastock makaa ya mawe kujiandaa na lolote litakalotokea dhidi ya Russia.
Ilikuwa ndio wakati wakukusanya mapato yakutosha na kuijenga Songea na sio kuwachekea Matajiri kujenga chumi zao binafsi na familia zao.

Kinachotokea Songea nikutifua ardhi na kuacha mashimo kule na umasikini kama palivyokuwa.

Miaka nenda rudi makaa yanachimbwa na kusafiri kutoka Luanda kuja Kitai kwenye storage then malori yanakwenda kupeleka Mtwara port, hakuna anayewaza kujenga Ile Barabara ya Luanda - Songea kwa kiwango cha lami wala kujenga rail line kuelekea Mtwara port na kupumzisha bandari.
 
Back
Top Bottom