Njoo tujuzane kuhusu Hisa

CEOgwamzy

Senior Member
Joined
Jun 14, 2014
Posts
139
Reaction score
50
Huu ni mtazamo wangu binafsi juu ya soko la Hisa (shares) ambalo nadhani unaweza kumsaidia mtu yoyote kwa namna yoyote ile.

Nini maana ya uwekezaji katika soko la HISA?
Ni kitendo cha kununua vipande vya hisa vya makampuni mbalimbali ambayo yamehalalishwa na soko hilo (Mfano; CRDB, NMB & TBL), hivyo kumfanya mnunuzi kuwa na umiliki juu ya kampuni hiyo kulingana na vipande alivyonunua. Kama ilivyo katika uwekezaji mwingine pia hapa mnunuzi anakuwa na lengo la kupata faida (profit maximization).

HISA ni nini?
Ni sehemu ya umiliki ambayo inawakilisha kiasi halisi ambacho mmiliki amechangia katika mtaji wa kampuni, umiliki huu unampa mtu husika(share holder) haki ya mgawanyo wa faida ya kampuni kulingana na kiasi alichochangia kwenya mtaji wa kampuni wakati wa kununua hisa.

Nini maana ya soko la HISA?
Ni sehemu ambayo uuzwaji na ununuzi wa hisa na bondi unafanyika.kwa Tanzania tunalo soko la hisa la dar es salaam(dar es salaam stock exchange market) ndilo soko kubwa na maarufu nchini.

Namna gani unaweza kufaidika na HISA?
Hapa ndipo kiini cha habari kilipo,hisa zinaweza kumfaidisha mtu kwa njia mbalimbali(njia kuu tatu):-

i) Gawio la faida(through dividends):
Hapa mmiliki wa hisa anapata gawio lake la faida ambayo kampuni imeipata katika kipindi hicho.Gawio hilo linategemea kiasi cha faida iliyotengenezwa, kama faida tengenezwa ni kubwa pia mgawanyo huwa mkubwa na hupungua pale faida inapopungua.Gawio la mtu husika linakokotolewa kwa kuchukua jumla ya hisa za mtu anazomiliki unazidisha na malipo ya kila hisa ambayo kampuni inakuwa imeweka.

Kwa mfano: kama wewe unamiliki hisa 5000 za CRDB na bodi ya kampuni imeweka malipo ya Tsh.300/= kwa kila hisa, gawio lako kwa kipindi husika litakuwa Tsh. 1,500,000 (yaani 5000x300=15,00,000).

Muhimu: Makampuni mbalimbali nchini hutoa gawio mara tofauti tofauti, benki nyingi hugawa mara moja kwa mwaka, makampuni mengine mara mbili pia kuna baadhi hugawa mpaka mara tatu kwa mwaka mfano TBL (Tanzania breweries limited) ila ukokotozi wa gawio unabakia ule ule kama nilivyoelekeza hapo juu.

ii)Kupanda kwa mtaji wekezwa(through capital gain)
Hii ni faida nyingine ya hisa na ndo ambayo wawekezaji wengi wanailenga.Hii inatokana na mtaji(pesa) uliowekezwa kupanda kulingana na kupanda kwa bei(thamani) ya hisa.

Kwa mfano: Chukulia una mtaji wa Tsh.2,000,000/=na unataka kununua hisa kampuni ya NMB ambayo kwa kila hisa moja huuzwa kwa Tsh.400/=, hii inamaana utanunua hisa 5000 za NMB (yaani; 2,000,000/400=5000).

Baada ya muda fulani kupita na bei za hisa zikapanda (chukulia bei ikapanda kutoka Tsh.400/= hadi Tsh.2,000/=),mtaji wako pia utapanda na kuwa Tsh.10,000,000/= (hisa 5000x2000/=).

iii) Kutumia cheti cha umiliki wa hisa kama rehani ya kuchukulia mkopo benki na kwenye taasisi zitoazo mikopo
Hii faida nyingine ya hisa inaweza kuwa haitambuliki sana, ila ukweli ni kwamba unaponunua hisa za kampuni yoyote unapewa cheti cha kuhalalishwa kuwa na wewe ni mmoja ya wamiliki ya kampuni hiyo(share certificate).

Hivyo basi hicho cheti kwa kuwa kinatambulika kisheria hivyo kina mamlaka ya kuwekwa rehani pindi mmiliki wa cheti hicho anapotaka kuchukua mkopo benki au kwenye taasisi nyingine za mikopo. Na kiasi cha mikopo mhusika anachoweza kupewa au kupata kinategemeana na kiasi cha hisa zimilikiwazo.

ATHARI ZINAZOWEZA KUTOKEA JUU YA UWEKEZAJI KATIKA SOKO LA HISA/UMILIKI WA HISA??

Kama ilivyo katika uwekezaji wowote ule pia hisa zinaweza kuwa na athali mbalimbali;

Athari kubwa ni ile ya kupungua kwa mtaji wekezwa kutokana na kushuka kwa thamani ya hisa (bei ya hisa) hii ni kwa mfano umewekeza Tsh.2,000,000/= ukanunua hisa za NMB kwa Tsh.400/= kila hisa ina maana utapata hisa 5000, ikatokea bei ya hisa ya kampuni hyo NMB kushuka na kufikia Tsh.300/=kila hisa ina maana mtaji wekezwa pia utashuka na kufikia Tsh. 1,500,000/= (yaani; 5000x300=1,500,000/=)

Wapi ninaweza kununua au kuuza Hisa?
Hisa zinanunuliwa na kuuzwa kupitia madalali(shares brokers) maalum ambao wamehalalishwa na serikali na wana leseni za biashara hiyo.

Kwa wakati gani na kwa namna gani ninaweza kununua Hisa??
Kwanza kabisa inabidi kuhakikisha kampuni unayotaka kununua hisa imeorodheshwa(is listed company) na soko kuu la hisa la Dar es salaam.

Mpaka sasa soko limeorodhesha kampuni zipatazo 21, kampuni 14 zikiwa za ndani ya nchi na 7 zikiwa za kutokea nje.Pia unahitajika kujua bei kwa kila hisa ambazo unahitaji kununua.

Ukishajua hayo, unatakiwa uende kwa dalali wa hisa kwa ajili ya usajili na ununuaji wa hizo hisa.kumbuka bei za hisa unaweza ukazipata kutoka kwenye tovuti ya dse.go.tz alafu nenda kwenye market reports uchague daily market report hapo utaona bei za hisa za kampuni zote kwa siku husika.

NB: Bei husika ni hyo closing price na sio opening price. Na pia kama huna uhakika na hisa unazotaka kununua ni vyema ukapata ushauri kutoka kwa dalali(share broker).

Mahitaji yapi natakiwa niwe nayo wakati wa kununua Hisa?
Ili uweza kusajiliwa na dalali wa hisa unaweza kuhitajika kutoa taarifa fupi zinazokuusu wewe kama vile; jina kamili, mawasiliano yako,namba ya akaunti yako, kitambulisho chochote na muhimu mtaji wako ulionao uanotaka kuwekeza.

Gharama zipi hutozwa pindi ununuapo Hisa?
Dalali analipwa ada ya asilimia 2 ya mtaji wekezwa (2% of capital). N gharama ya Tsh. 1000/= kwa ajili ya kuingiza fedha kwenye akaunti ya dalali.

Mfano; Tuseme kwamba unataka kununua hisa 200 za CRDB ambazo gharama yake ni Tsh.400/= kwa kila moja, inamaana unahitajika uwe na mtaji wa Tsh.80000/=(200x400=80000).ada ya dalali unamlipa Tsh.1600 yaani 2%x 80000=1600/=.

NB; Kiasi cha chini cha Hisa unachotakiwa kupanga kununua kwa Tanzania hakitakiwi kipungue hisa kumi(10).

ZIADA:
- Orodha ya madalali na mawasiliano yao;

**Orbit Securities Company Limited
P.O. Box 70254, DAR ES SALAAM
Offices: 4th Floor, Golden Jubilee Towers, Ohio Street,
Tel: 255 22 2111758, Fax: 255 22 2113067
E-mail: orbit@orbit.co.tz

**Core Securities Ltd
P.O. Box 76800, DAR ES SALAAM.
Offices: Fourth Floor ?€" Elite City Building, Samora Avenue,
Tel: +255 22 2123103, Fax: +255 22 2122562
E-mail: info@coresecurities.co.tz
Website: www.coresecurities.co.tz

**SOLOMON Stockbrokers Limited
P.O. Box 77049, DAR ES SALAAM
Offices: Ground Floor ?€" PPF House, Samora Avenue/Morogoro Road.
Tel: 255 22 2124495/2112874, Fax: 255 22 2131969
Mob: +255 714 269090 +255 764 269090
E-mail: solomon@simbanet.net, info@solomon.co.tz
Website: www.solomon.co.tz

**Zan Securities Limited P.O. Box 5366,
Dar es salaam P.O. Box 2138, Zanzibar
Offices: Mezzanine Floor, Haidary Plaza, Dar es salaam 1st Floor, Muzammil Centre, Malawi Road, Zanzibar
Tel: +255 22 2126415, Fax: 255 22 2126414 Mob: +255 786 344767, +255 755 898425
E-mail: info@zansec.com

**Rasilimali Limited P.O. Box 9373, DAR ES SALAAM
Offices: 3rd Floor, CHC Building, Samora Avenue,
Tel: 255 22 2111711 Fax: 255 22 2122883
Mob: +255 713 777818 / 784 777818 / +255 754 283185
E-mail: rasilimali@africaonline.co.tz

**Tanzania Securities Limited
P.O. Box 9821, DAR ES SALAAM O
ffices: 7th Floor, IPS Building Samora Avenue/Azikiwe Street
Tel: 255 (22) 2112807, Fax: 255 (22) 2112809
Mob: +255 718 799997 / +255 713 244758
E-mail: info@tanzaniasecurities.co.tz
Website: www.tanzaniasecurities.co.tz

**Vertex International Securities Ltd
P.O. Box 13412, DAR ES SALAAM.
Offices: Annex Building ?€" Zambia High Commission, Sokoine Drive/Ohio Street,
Tel: 255 22 2116382 Fax: 255 22 2110387
E-mail: vertex@vertex.co.tz, operations@vertex.co.tzWebsite: www.vertex.co.tz
 
Kiwango cha chini cha hisa anachotakiwa kumiliki mtu kwa Tanzania ni hisa 10, so unatakiwa ujue bei ya kila hisa moja unazotka kununua then zidisha mara idadi utakazoweza nunua na isipungue hisa kumi
 
Mimi siwaelewi hawa CRDB wanachezea soko hisa zao zinashuka tu

Kushuka kwa hisa inategemea na demand and supply na pia kama umekuwa makini kufuatilia utagundua hata dola inapobadilika sana huchangia na hisa kubadilika bei.
 
Asante sana mkuu!
Swali, je endapo nitanunua hisa 100 mfano za TCCL nikapewa cheti cha hisa tajwa, na baada ya miezi kadhaa nikaongeza tena hisa 100 zingine za TCCL, Je nitakuwa na vyeti viwili vya hisa au nitapewa kimoja chenye hisa 200?
 
Okay ili niweze kununua hisa katika kampuni yeyote nahitaj kua na mtaji wa shilingi ngapi na utaratibu ukoje
Hakuna kiasi maalumu,kama hisa za NMB ni tsh 400,siamini kama huna tsh 400,kiwango cha pesa unachoweka ndiyo faida kubwa unayoipata.
 
Hapo kwenye Athari kwanza ni fikira potofu zinazofanya watu wengi wasijaribu kununua Hisa.

Katika uwekezaji wowote ule,hatushauri na hatupendekizi.Mfano:-Huwezi kuweka mayai yote,kwenye kikapu ina maana yakiharibika yote umeingia hasara.

Kwenye Hisa ili usiishie kupata hasara unapoenda ukakuta soka la kampuni uliyonunua ya hisa limeshuka ina maana lipo kwenye mstari mwekundu unakuwa una siku 14 ndani ya hizo siku ni vizuri ukaongea na Broker wako ukauziuza.Hivyo usipate hasara
Mfano mara nyingi kwa makampuni yanayotaka kufilisika.

Athari kubwa pia ni kuingia kwenye solo la hisa bila kutokuwa na malengo.Na kuamini uwekezaji unafanywa na watu weupe.

NB:Kwa sasa Tanzania ina soko moja la hisa hivyo ni muhimu kuchangamkia


Kwa walio makini,nitaingia kiundani zaidi.
 
Je kama ntamiliki hisa za kampuni X, na nikapewa cheti cha umiliki hisa, ikatokea hiyo kampuni kufanya vibaya kiasi CHA kushusha thamani ya mtaji, vipi status ya kile cheti nkienda kuombea mkopo!
 
Asante sana mkuu!
Swali, je endapo nitanunua hisa 100 mfano za TCCL nikapewa cheti cha hisa tajwa, na baada ya miezi kadhaa nikaongeza tena hisa 100 zingine za TCCL, Je nitakuwa na vyeti viwili vya hisa au nitapewa kimoja chenye hisa 200?

Inategemea, kwanza kabisa ni vzuri ukawa unamtumia dalali mmoja (broker) na pindi uongezapo hisa unaweza ukafanya update ya cheti cha zamani ili kipandishwe thamani....au alternatively waweza kuwa navyo viwili
 

Ni kwel mkuu hio inaitwa "diversification" yaan kusamba mtaji
Hio niliipanga kuisema kwenye mada zifuatazo yaani jinsi ya kupunguza madhara yanayoweza kutokea kwenye soko la hisa buti ASANTE SANA mkuu tuendelee kujuzana
 
Asante sana kwa somo zuri ambalo watanzania wengi hawajui.

Ni kwel mkuu kwanza inabidi kama watanzania hasa vijana tujuzane kuwa stock exchange market(soko la hisa) ni sehemu ambayo unaweza ukavuna utajiri.....mifano mizuri ni kina warren buffet wamekuwa ma-billionaire b'se of shares
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…