Njoo tumzungumzie msanii Marioo

Njoo tumzungumzie msanii Marioo

ubelito

Senior Member
Joined
May 19, 2015
Posts
169
Reaction score
259
Uhali gani mwana JF?

Binafsi nimetokea kumjua Marioo tangu 2017 alipotoa wimbo wake wa Bure. Nikawa shabiki wake ila japo hakuanza kuimba rasmi ila alikuwa akitungia watu tu nilitamani atoe nyimbo zake binafsi.

Ndipo alipokuja na ngoma rasmi ya Dar kugumu na kuendelea hadi ya uchungu.

Nachompendea jamaa ana mashairi makali sana, melody tamu mno labda tu kwakuwa mimi napenda nyimbo za kusikiliza na sio za vurugu.

Mwaka ukiwa unaishia huu wa 2019 ngoma kama Inatosha, Raha & Ya uchungu ndio ngoma zangu bora kabisa za kufungia mwaka.

Marioo endelea barikiwa, toa muziki mtamu daima.

Toa mchango wako wowote kuhusu muziki wake. Taja na ngoma tamu toka kwake unayoipenda.
 
Nalala nikisikiliza Playlist yangu
Screenshot_20191109_231550.jpeg
 
Ndio msanii anayeimba nyimbo za kueleweka kwasasa..!
Aendelee kufanya anachokifanya, muda sio mrefu watu watakuja kujua kuwa wanapoteza muda wao kwa two overrated artists wa Tanzania..!
 
Anajua sana sema ajitahidi kucheza na melody mana anarudia sana
 
Back
Top Bottom