Njoo tusimualiane Mambo ya kutisha/kuogopesha uliyowahi kushuhudia hapa Duniani


Mungu aliumba vitu vinavyoonekana na visivyoonekana
 
Binafsi hizi habari nazisikia tu, machache sana nimejionea lakini hayana tafsiri ya moja kwa moja na ushirikina

Tabora, miaka flani niliishi, stori nyingi sana za majini lakini sikuwahi kushuhudia.
Then tulihamia mkoa mwingine kanda ya ziwa. Nyumba tuliyohamia asubuhi mama anasimulia vibweka alivyosikia usiku. Mara asikie mchanga umemwagwa batini lakini hasikii unatiririka kumwagika chini (unakua kama umeganda), mara mapaka, mara watu wanakimbizana darini etc

Then nikiwa chuo,mwaka wa mwisho tunakaa hostel (mabibo) mshkaji wangu tumebebana akawa analalamika kama wiki nzima akilala znamuona mtu anamkaba kooni, anajaribu kufurukuta au kupiga kelele lakini anakosa nguvu, hadi mwishoni jamaa akiondoka ndo anashtuka, ananiambia mimi lakini nampuuza...

Baadayenikapata kazi, ,miaka ya 2010s nikapelekwa mkoa flan unasifika kidogo kwa ushirikina. Bosi wangu akanipangia kituo cha nje ya mji kidogo, naripoti namkuta jamaa mwenzangu na mlinzi. Hiyo ni siku ya kwanza. Huyu usiku akatupigisha sana stori za wachawi na miujiza anayoshuhudia usiku hapo. Ilikua usiku, nilipochoka zile stori nikaaga nikalale. Napanda kitandani tu, hata dakika kumi hazijapita namuona yule mlinzi HUYOO, kanikalia tumboni akanikaba kooni, nikajaribu kufurukuta au kupiga kelele WAPII! Tukio likadumu kama dakika tano mlinzi akatoweka, ndo nikakurupuka. Niliwaza sana kuhusu yule mlinzi. Siku za mbele nikaambiwa yule mlinzi ni mganga na mshirikina. Nikamkumbuka rafiki yangu niliyekuwa nanpuuza na tukio lililonitokewa, nikasikitika kwanini nilikuwa nampuuza

Kwasasa sijaona tukio la ajabu, na ninatembea sana usiku tena maeneo yanayosemekana ni hatari lakini siogopi wala sioni kitu kibaya, tena ninajenga hisia labda USHIRIKINA ULIKUWA ZAMANI, miaka hii umekuwepo kidogo sana, MAY BE!

Kuna rafiki yangu ALIOKOKA, siku moja alinipa somo akaniambia, mambo ya ushirikina na uchawi huwakuta zaidi watu wanaoyaamini, WAKICHANJWA CHALE au KWENDA KWA WAGANGA. wanakuwa kama wametiwa SIGNAL ambazo wachawi wanaziona hivyo kuanza kuwafuata. Kama SIMU INAVYOPATA SIGNAL ZA NETWEK ya mtandao flan.Hata kazini nawaona wenzangu mara wamepakwa marangi, machale n.k nawashangaa tu maana sioni cha zaidi wanachopata wala mimi kuumizwa nao. EVERYTHING JUST NORMAL.
 
Japo tukio hili silichukulii kuwa la ajabu sana but ni tukio ambalo nililishuhudia na nikabaki na maswali kuwa ilitokeaje.

Kipindi cha nyuma mdogo wangu wa pili alikuwa mchanga kabisa, mama alikuwa amemuweka kwenye kochi ili awe anachezacheza hapo huku yeye na mimi tukiwa nje yeye (mama) akifua mimi nikicheza na ndani hakukuwa na mtu mwingine yeyote ndani.

Sasa ikawa mama anaingia kufuata kitu akamkuta mtoto yupo chini sakafuni akiwa anacheza na ametandikiwa nguo kama alivyokuwa ametandikiwa pale kwenye kochi.
Mama alistuka sana, akadhani labda alianguka, lakini kama angekuwa ameanguka lazima angeumia na angelia pia zile nguo zisingekuwa katika mpangilio vile.
Hadi sasa hivi hicho kitendawili sijawahi kukitegua.
 
hili tukio sijui niite ndoto au uhalisia.

nikiwa na miaka 14 mikoani mbeya wilaya ya kyela, kuna siku nimelala usiku nikaota nipo sehemu na mtoto wa jirani yangu na baba yake ambao wanakijiji walikuwa wanawatuhumu kwamba ni wachawi, sina uhakika kuhusu hilo.

basi huko tulipokuwa tulikuwa tunafanya mambo mengi ni kama sherehe hivi, baadae baba wa yule kijana akasema mda umeisha inatubidi turudi nyumbani. Tukaanza kupaa wakati tunakaribia kufika nyumbani ghafla nikawa kama nimeshtuka kutoka usingizini kabla sijaingia ndani, lakini chakushangaza nikiwa bado sijielewi vizuri nikaona ukuta unafunguka na nikaingia kwa kasi ya kama spidi 500 mpaka kitandani. Nilivyofika kitandani akili ndio ikaa sawa, sasa nikawa najiuliza hii ni ndoto au uhalisia sijawahi pata jibu mpaka leo.
 
Duh!mzee ulienda kuwanga wewe bila kujijua[emoji2] [emoji2]
 
Mkuu ilikua kweli hio
ila najiulizaga hii teknolojia ya kufungua ukuta inawezekanaje hasa process zake
 
Hii ilikua kweli[emoji26]wachawi sio watu wazuri
 

Huikujirudia tena hio hali?
 
Aliweka yeye hii, mtumishi hagangui kama waganga
 
Dah stori inatisha hii
 
Ukitaka kufatilia mambo ya kutisha iandae akili yako na mwili vinginevyo unaweza data kabisa,

Nikiwa kijijini nyumbani nasoma shule ya msingi nilikuwa mkorofi sana na jeuri siku moja rafiki yangu wa kike alinunuliwa Baiskel zile za gia na baba yake akatoka nayo kwao mjini hadi nyumbani kijijini basi mm na ukorofi wangu nikachukua ile baiskel nikaiendesha njia zote za kijijini zile nzuri nawavimbia watu kwamba nina chombo yenye gia nne ilipofika saa 12 jioni nikarudi home,nikapaki na rafiki yangu alinambia analala ataondoka kesho yake.

Ratiba yangu lazima nisafishe uwanja jioni ili nikiamka asubuhi uwanja msafi naamkia shambani laah kabla ya usafi nikachukua baiskeli nikaiweka ndani nikafunga chumba na kufuli kubwa la store then nikasafisha uwanja kilichofata ni kulala hapo ndio tatizo lilianza usiku nilishtuka usingizini nikasikia kelele nje ila sasa kelele ni kama mtu anaendesha baiskeli mwanzo nilijua mwizi ila nikatulia kidogo ndipo nilipogundua mchana nilifanya kosa kuwalingia watu na kile ki baiskeli usiku ule kama masaa matano baiskeli ile iliendeshwa kuzunguka nyumba mpaka nikachoka kusikiliza sauti nilipomwamsha kaka asikilize zile sauti ajabu hasikii kitu, nikijaribu kuwasha kibatari unatokea upepo unazima mpaka nikachoka nikaaamua kulala tu asubuhi nilikuta mistari ya baiskeli mji mzima kufungua store baiskeli ipo vilevile niliogopa hata kuigusa
 
N
Ndo ukome!!
 
Binafsi sikuwahi kushuhudia mambo ya kutisha,hata Kama yalikuwepo madogomadogo yalikuwa ya kawaida tu..Ila baada ya kuoa na kubarikiwa na mwanangu wa kiume mambo yalianza kubadilika.

Ni hivi,

Mwanangu wakati akiwa na miaka Kama mitano hivi alianza kuongea kuhusu mambo yaliyotushangaza sana mimi na mke wangu..kuna wakati mmoja kulinyesha mvua ya rasharasha tu tukawa tunarudi home kutoka madukani naye..kawaida Kuna Ile harufu ya mchanga baada ya mvua ya aina hii kunyesha baada ya muda mrefu..sasa kilichonishangaza ni kuwa mwanangu alianza kusema kwamba anahisi harufu ya mungu..nikamwambia ni harufu ya mchanga tu Ila akawa mkali kidogo kwamba nakataa kukubaliana naye kuwa mungu hunukia hivo..tulipofika home lile Jambo likanifikilisha sana nikasema japo huenda ni upuuzi tu wa kitoto wacha nimwambie mke wangu..ndipo naye akaniambia kwamba kuna wakati kijana wetu alikuwa akimtayarisha kuenda shuleni kisha mtoto akamwambia kwamba anampenda sana na sio Kama mamake yule mwingine wa "nyumba iliozeeka"alisema kwamba yule mamake mwingine ni mkali na wakati mwingine hampi hata chakula kizuri..hili Jambo lilitushtua Sana na siku moja nikamwambia mwanangu anipeleke "nyumbani kwao huko kulikozeeka"

Yani nilishtuka mwanangu aliponiongoza hadi tunafika sehemu flani kuna jumba kubwa na ambalo kwa muonekano ni Kama lilijengwa miaka ya zamani na ambalo hamna anayeishi humo..japo hatukuingia nilishtuka sana.

Ilipita siku nyingi mwanetu akitupa shuhuda za mambo ya ajabu ajabu nasi tukawa tunaomba Mungu sana amuepushe na mambo ya kivile..Ila yaliendelea tu..

Siku moja nakumbuka ilikuwa jumapili fulani naelekea home mida ya saa tatu hivi usiku..nikawa nimepitia kwenye njia flani ambacho kipo katikati ya shamba kubwa na wakati ule limepandwa mhindi..niseme tu nilikuwa nimetoka kujipumzisha kidogo na marafiki kwa hiyo nilikuwa nimenyonya Guiness mbili hivi..ila nilipoinua macho kuangalia mbele nilishtuka kuna mwanamke mbele yangu na manukato yake nayahisi kabisa..alikuwa mrefu kidogo ana mwili wa kawaida tu nikimaanisha kimaumbile..alionekana kutembea Kama mtu aliyechoka sana kwa hiyo hakuwa anaharakisha..kilichonishangaza ni kwamba nilijitahidi sana kuharakisha nimkaribie yule mwanamke Ila ilishindikana..nikawa ni Kama vile nimesimama kabisa naye akawa bado anatembea..

Ni mambo mengi tu ila kwa sasa ni muda sana sijasikia mambo Kama hayo tena na namshukuru mungu sana..tukio la mwisho lilitokea 2004
 
Pole sana vp dogo anaendeleaje?
 
Wakati tupo vijana wadogo, watu walikuwa wanaamka asbh Sana kuwahi hosp.
Jirani yetu mkewe alilazwa akadamka asbh Sana kupeleka maji ya Moto hospitali, Ile kufika mitaa ya mlapakalo anakangalia juu anamuona jamaa bize juu ya angana na baiskeli shati linapepea.

Aligeuza fasta home na kusimulia kisa Cha kushindwa kwenda hospitali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…