Njoo tusimualiane Mambo ya kutisha/kuogopesha uliyowahi kushuhudia hapa Duniani

Nakumbuka Miaka ya 90 na kitu hivi kuna sehemu inaitwa Mwananyamala mchangani, kuna kaeneo wamekapa jina "jitu kubwa" ama "mtini" kwenye mti huu panasifika sana kufanyika mambo ya kishirikina, na inasemekana kwenye huu mti ndio makutano yao wazee wa kazi. Wazazi walikuwa wanatukataza na kutuonya sana tusiende kucheza maeneo yale. Lakini cha ajabu watu kila kukicha watoto kwa wakubwa tulikuwa tukikutana pale na kukaa kwenye mizizi ya mti huo ambayo ni mikubwa mfano wa magogo(ma benchi) na kupiga soga pamoja na kuendelea na michezo mbali mbali ya kitoto bila kujali maonyo ya wazazi wetu. Hii nadhani ni kutokana na hewa nzuri inayopatikana mtini hapo.

Basi siku moja tukiwa tunaendelea na michezo mimi na mwenzangu chini ya mti, mara matunda mfano wa vitunguu vikamwangukia kichwani, kila akijaribu kutoa havitoki, ikabidi akimbilie nyumbani kwao, nami nikimbilie home kwetu. Baada ya muda kidogo tunasikia vilio kwa majirani kwamba yule dogo amefariki, hakika niliogopa sana na sikutoka nje siku nzima kwa hofu. Ilifikia stage nikitumwa dukani natafuta njia nyingine ama nikipita pale napita na speed 100 hata iwe mchana. Hili tukio sitalisahau na leo kwa mara ya kwanza ndio nalisimulia kwani sikuwahi kumwambia mtu yeyote hii kitu.
Pmengi yametokea ktk mti huo ikiwemo la jamaa aliyekutwa amekufa akiwa amelala hapo mtini.

Kwa sasa ni miaka takriban 30 imepita najiuliza km vile vitu vingeniangukia mimi sijui ningekuwa wapi le hii. Sina hakika km huu mti bado upo maana kila watu wakijaribu kuukata kunatokea vikwazo eidha uwake moto ama kwa baadh ya watu kupinga zoezi hilo. Kuna mzee alikuwa anasifika kwa zoezi la ukataji miti lkn kwenye huu alichemka na mara baada ya kumaliza jaribio la kuukata naye akapoteza maisha.

Wachawi wanapata faida gani kwani?


Mungu ashukuriwe.
 
Aiseee pole sana
 
Hii nyumba tangu nipo mdgo naisikia habari zake. Nimeamia dodoma rasmi mwaka 2000 na mtaa ninaokaa sio mbali sana na mtaa ambao nyumba hiyo inasemekana ipo. Ni maeneo ya chamwino/area A kama sikosei
 
Kama sio ndoto..jiangalie vizuri..isijekuwa..umeazima /umechukua mwili wa creature mwengine. .sasa sijui wewe utakuwa...wa spice gani... ... !
 
Kuna siku nilikuwa katikati ya daraja la reli pale mbalizi Lile daraja la treni Lina futi Kama 50 Cha ajabu nilipishana na mtu anatembea kea miguu pembeni ya reli kitu ambacho hakiwezekani Yani kakanyaga chini futi hamsini na tukasalimiana hii nawaza mpaka leo
 
Nilikua nipo kwenye mood ya kumasturbate yaani nilikua natafuta uzi wa mwisho kabla sijaingia xvideos sasa nimefika hapa na xvideos siendi leteni visa niburudike.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mm niliwahi kuishi na mtot wa shangaz yng alikuwa anaishi kenya before alikuwa mtu wa church sasa kwa mitamaa yake akatembeaga na mwanafunzi kenya ikawa msala akakimbilia bongo wale jamaa walimtafuta mpaka wakaja bongo ila wakamkosa unavyoonekana juhudi za kumkosa wakaamua kwenda kwa sangoma jamaa alikua tukilala usiku full mauza uza mara achwapwe viboko ashtuke apige makelele, mara ananyongwa yan visa nilikuwa silali sasa mm nilikuwa havinigusi sasa kwa akili za kipindi kile nikawa nawaza km mshkj hamna chochote anazingua tuu ilifikia kipindi mpaka akawa anakimbilia kulala kanisani. Sasa siku moja alienda kwa sangoma na yey akaja na dawa akaipaka chumbani,,, bwana bwana wale jamaa walikasirika na mm niliipata ile siku.

Kwanza nilikuwa nimelala nikahis km miguu inavutwa nje yan navutwa nje na mm najivuta ndani sasa nimeshtuka usingzn kumbe navutwa kweli japo bado nina mawenge ya usingzi, sasa kuna kiatu kilikuwa km kimening'inizwa juu ya seeling body nilipigwa cha kichwa mpaka nikajiuliza iv ni kwel kile kiatu kimefikaje uku akili inarudi nahusa hiv nimevimba.

Aaa mama mdgo alimfukuza jamaa akamwambia vita yako isiwapate wengine we nenda tuu. Ila kile chumba nilikuwa sina amani kbsa kukaa peke yangu mule
 
Kwahiyo alirudi Kenya kwa wabaya wake na alimalizana nao vipi?
 
Ikawaje mkuu? endelea
 
Nimekuwa karibu na mtu ambaye amekuwa na mahusiano na pepo. Dunia ina mengi sana jamani yaani ilifka wakati ukimuuliza tu habari ya hilo dude lake sauti inamkauka hapohapo na hawezi ongea tena mpaka kesho yake!

Inatokea mpo matembezini mbali kabisa na nyumbani na mkiagana hazipiti dk 5 anakwambia kashafika nyumbani kwao wakati pana umbali wa zaidi dk 15.visa ni vingi sana nmeshuhudia na nilikuwa nashangaaa sana maana yanamtishia sana akitoa siri zao maaana akiongea tu kuhusu wao kesho yake lazima ashindwe amka. Niishie hapa ila hii dunia ni Mungu tu ndio mwokozi kwetu
 
Mpk Leo au yalishaisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…