*****Kuna siku moja hapo hotelini, kuna mfanyakazi mmoja alienda choo cha kufanya haja kubwa usiku, kufungua mlango akamkuta paka amejifia katikati ya sink ya choo, na alikuwa paka ameshiba kweli, yaani hakuwa na madonda labda ukasema alipigwa akaja akafia pale. Ebana, wee, staff wote waligoma kwenda kumtoa. Apo hoteli walinzi wetu walikuwa ni JKU, ni jeshi la Zanzibar, akatoka mmoja akaenda kumtoa na kwenda kumzika nje ya hotel. Kila staff akawa ameingiwa na woga, mana wanaona sasa yale mambo ya Zamani ya kukoseshana amani yamerudi tena kwa kasi. Hakuna aliekuwa anaenda chooni ikifika Saa nne usiku.
Sasa mimi kama nlivosema awali, naamini haya mambo yapo, lakini kabla ya ku conclude na assume ni kitu kingine cha kawaida tu.
Siku moja kama kawaida yangu baada ya kumaliza Youtube, navuta taulo naenda zangu choo cha haja kubwa halafu ndio niingie shower. Mara nakaribia chooni, nasikia kama vile mtu anajimwagia maji, lakini hio haikuwa chooni sasa, kuna sehemu karibia na kona ya fensi kuna generator, hapo ndipo nikawa naskia sauti inatokea hapo. Kiroho kikaanza kunidunda, sijui nirudi tu chumbani nikaushie ama vipi. Lakini nkasema hapana, ngoja nipate ushahidi kamili, nikasogea sogea ata kufika lile eneo bana, kuna bidada alikuwa anajimwagia maji kumbe staff wa hotel 😀 😀 😀 Alishtuka kuniona, nikarudi nyuma kwenye position ambayo simuoni kumpa stara uku nikamuelewesha aache kuoga chini ya generator atasababisha matatizo. Nikamuuliza, choo kipo, tena kina maji ya moto na baridi, unaoga kwa raha, kilichokufanya uoge maji ya baridi usiku huu pembezoni mwa generator nini? Akanijibu hakuna anaekwenda chooni baada ya saa nne tangu tukio la yule paka! nikamwambia aache upumbavu tu. Mi nikaingia zangu chooni nikiwa nimejikaza kisabuni tu. Mana nlikuwa na wasiwasi ivo ivo. lakini nlimaliza yangu fresh.
Kutoka sasa naskia tena kuna pirika pirika, katika hilo eneo kuna kontena ya mambo ya maintainance, kama kawaida nkasema ngoja nikatafute ushahidi kamili, akatokea fundi kwa nyuma uku akiwa amemaliza kukojoa, Nilimchana kidume kizima na yeye anasita kuingia chooni kufanya haja zake.
*****Hii hapa nilijiroga tu mwenyewe..... Usiku wa manane nilitoka room kwangu nikaenda jikoni kujipikia mana njaa ilinibana sana. Mzee baba nikasikia vishindo ndani ya jiko na mimi nimo humo humo ndani, izo mbio nilizotoka apo breki ya kwanza nilikwenda kumuamsha Chef mkuu, nkamwambia bana jikoni kuna mauzauza yamenitokea wakati najitaarisha kupika, hapo moyo unakwenda mbio kiama. Halafu chumba changu kilikuwa kinaface moja kwa moja na main entrance ya jiko. Chef mkuu akatoka akasema hebu twende, tukaingia jikoni, tunaanza kuangaza, kumbe bana mle ndani kulikuwa na paka tu alitoka mbio. Dah! roho apo ikatulia afadhali.
Aisee hio hotel hata kama hakuna mauzauza mazingira yake pekee yanatisha, ni sehemu ambayo ipo kimya sana. Na nilikuwa najitahidi kuwa jasiri, mana kuna baadhi ya siku ilinilazimu mida ya saa nane usiku nitoke niende nikamuamshe mgeni kwa ajili ya departure, vyumba vipo mbali sana na staff house, dah apo ilikuwa ni kuomba usiyakute njiani.