Njoo tusimualiane Mambo ya kutisha/kuogopesha uliyowahi kushuhudia hapa Duniani

Njoo tusimualiane Mambo ya kutisha/kuogopesha uliyowahi kushuhudia hapa Duniani

Du
Kuna Bar iko mitaa flani hivi kule chuganian,ukimuelewa mhudumu fresh unampanga then anazuga zuga pale baadae anaingia chini ya meza(ni zile meza zenye cover za plastics ndefu) unashusha zipu kiaina yeye anaendelea kunyonya mkuyenge huku wewe unakunywa zako bia kama vile hakuna kinachoendelea,ukimalizana nae anatoka chini ya meza nduki anaendelea kuhudumia wateja kawaida kabisa.

Itakua wateja wa pale wamenyonywa sana na majini kule chini ya meza.
 
Sema mimi sio mchongo wala nini

Jeshi kuu mnaongoza kuleta stori za jeshi lenu huku kuliko majeshi yote
 
Pumbavu unaleta story za jeshini huku,hayo mambo ya kazini kwako unatuletea raia ili iweje?hujaiva wewe
Wasamehe bure kila kozi lazima itoe askari ambao hawajaiva,inaweza kuwa madogo walikuwa wazee wa vitengo sana(bustani,maua,walinzi wa hanga)
 
Kaka mtoto wa mama mkubwa alienda kutandika kitanda baada ya kula usiku waende kulala.Pembeni ya nyumba yao kulikua na msufi mkuuuuuuuubwa ndio mti mkubwa zaidi pale kijijini.

Alipoenda kutandika hakurudi tena hadi saa linapita mtu hatoki ndani, kwenda kumtafuta hayupo! Walimuwinda nyumba nzima hawamuoni karibia masaa 3 nyumba yote hawaoni mtoto. Baadae walimuona chini ya meza ya kula (ndogo tu) kajikunyata hawesi kuongea. Wakampeleka kwa mganga usiku huo huo kafanyiwa dawa ndio akaanza kuongea kua kuna kitu kilimchukua kikampeleka ndani ya huo msufi.

Tumewangiwa utotoni kinoma noma..ilibidi mama ahamishe kitanda tulale chumbane mwake. Alikua akiwasha kibatali aone vizuri ndani anaona kiganja kinazima kibatali.

Wachawi waliniiba wakanitoa chumbani wanipeleka kunilaza chini ya mtungi..kwenye kona la nyumba. Walinipata asubuhi nikiwa nimesinzia nimefunikwa ushungi kama mtoto mchanga.

RIP kuna mbwa wetu alikua anapambana nao usiku wakamuuua
Fugeni paka, mbwa hapambani na mauzauza anapambana na wizi tu, kikubwa anabweka tu na kusepa. Ila paka bob, haondoki mpaka kieleweke, ama afe yeye au afe mchawi/shetani. Paka ni mlinzi mzuri kwenye haya maswala, hatuwaelewi tu mana wanajiskia sana wanyama hawa.

Watalaamu wanakwambia ukiona paka amekujua mguuni na kukuzonga sana haondoki ujue anakulinda na ubaya wa mauzauza, ila sisi tunaona anatusumbua tunampiga teke 😀
 
Fugeni paka, mbwa hapambani na mauzauza anapambana na wizi tu, kikubwa anabweka tu na kusepa. Ila paka bob, haondoki mpaka kieleweke, ama afe yeye au afe mchawi/shetani. Paka ni mlinzi mzuri kwenye haya maswala, hatuwaelewi tu mana wanajiskia sana wanyama hawa.

Watalaamu wanakwambia ukiona paka amekujua mguuni na kukuzonga sana haondoki ujue anakulinda na ubaya wa mauzauza, ila sisi tunaona anatusumbua tunampiga teke 😀
Hii ndio nasikia leo.
 
Hii ndio nasikia leo.
Paka ni mnyama ambae ana ujasiri mkubwa sana, mbwa haingii ndani. Bora ufuge paka kuliko mbwa linapokuja maswala ya mauzauza.
Mbwa utamkuta anabweka sana, lakini hapigani, labda auliwe kunyamazisha kelele zake lakini hapigani na mauzauza. Yeye mwenyewe mwoga kwenye hayo mambo.
 
Paka ni mnyama ambae ana ujasiri mkubwa sana, mbwa haingii ndani. Bora ufuge paka kuliko mbwa linapokuja maswala ya mauzauza.
Mbwa utamkuta anabweka sana, lakini hapigani, labda auliwe kunyamazisha kelele zake lakini hapigani na mauzauza. Yeye mwenyewe mwoga kwenye hayo mambo.
Kumbe! Kuna watu huwa wanadai paka hutumiwa na wachawi kumbe wanapambana na wachawi pia!
 
Hapa naweka stori ambayo nimehadithiwa na shuhuda na moja nili experience mwenyewe lakini sikutaka kuamini kuwa ni mauzauza.

****Niliwahi kufanya kazi kwenye hotel flan, hio hotel hapo ilipo, ikifika magharibi tu, hutamani kutoka, mana ipo isolated. Na ipo kwenye kijiji kimoja ambacho kuchawiana ni kama kunywa maji, watu hawaoni tabu kabisa kuambizana kuwa nitakuonesha. Haya mambo ya ushirikina ukiyashiriki, basi makazi yako yataathirika pia. Katika hii hotel naambiwa na wafanyakazi wa zamani kuwa mauza uza hayaishi, walinzi waliniambia kuwa walishawahi kumuona bibi kizee usiku wa manane anaenda kwenye pool anavua nguo zote anaogelea kisha anasepa zake. Kuna mfanyakazi mmoja alianguka chooni, akaanza kupapatika, kwa bahati kuna mfanyakazi (mwenyeji wa vijiji vya karibu na ilipo hotel) akasikia kishindo, akawashtua wenzake na kuwaambia wachote maji ya kwenye shimo la choo, wakampa jamaa akamnywesha yule dada, alizinduka.

*****Huyu mtu aliemnywesha hayo maji mwenzake, nimeambiwa yeye aliwahi kumfanyia dada mmoja aliekuwa mbishi kitisho. Wakati wanatia stori alimwambia kuwa hapa tulipo kuna mji mkubwa sana watu wanatembea hapa, yule dada akambishia kwa dharau, jamaa akamuuliza, je unataka kuyaona, akajibu ndio, akamwambia basi utayaona leo. basi kufika mida kila mmoja anaingia room kwake staff house, yule bi dada alikuja kumuona mshkaji yupo chumbani alipiga kelele kutoka kwa wenzake anamkuta jamaa yupo nje, jamaa alimuuliza tu nini. Bi dada naskia aliishia kusema kuwa hataki tena kuyaona.

*****Huyu huyu jamaa aliwahi kunihadithia story ambayo yeye alishuhudia mara hii. Na hii nimeconfirm kutoka kwa dada mhusika ambae kaka yake ndio yalimkuta haya. Katika management office ilikuwa kuna jamaa ameitamani nafasi ya mwenzake, maana ilikuwa ni ya kushika hela. SIku hio wakati mshika fedha kenda likizo, jamaa ananambia yeye alikuwa Restaurant anataarisha cocktail za wageni, ndipo alipomuona huyo anaetamani nafasi ya mwenzie akiingia na vibabu vizee vitatu ofisini. Ukikaa resta ilikuwa unaona ofisini ndani kama hawajafunga mlangu. Sasa mshika fedha alikuwa ameacha laptop ofisini. Vile vibabu vikafungua laptop ile na kujifanya kama vina type ivi, huku jamaa resta anawachora tu. Baada ya vile vibabu kumaliza, kila mmoja akapewa buku 50 wakasepa. Siku ya kurudi kazini mshika fedha hakufikia ofisini moja kwa moja. Alikuwa anachill TV lounge akitizama TV mwenyewe ndip hafla kichwa kikamuuma. Akainuka akamwambia yule jamaa alishuhudia mchezo sasa kuwa amtengezee chai konki mana kichwa kinamuuma, jamaa akamuuliza kimeanza kukuuma wapi, akamwambia wakati yupo anatizama TV, basi jamaa akamwambia tulia hapo hapo nakutengezea chai. Mshika fedha akasema anaenda ofisini kumalizia kazi za watu atume files kwa boss mana mda umepita wa kutuma report, jamaa akamwambia asiende ofisini na atulie tu hapo hapo kwenye TV chai inakuja. Mshika fedha alibisha na kwenda ofisini, kufika ile anafungua laptop yake tu, alianza kupiga makelele vibaya, wafanyakazi wengine walishtuka na kwenda wanamuona mtu kapata wazimu hafla, huku jamaa yupo resta anaendelea kutengeza chai aijuae mwenyewe anawachora tu. Wale wafanyakazi wakambeba kumpeleka chumbani kwake, jamaa akawaambia msimpeleke chumbani, mrudisheni TV lounge, hapo ndipo yalipoanzia, chai yake ishakuwa tayari, wafanya ubishi, wakampeleka chumbani, huko ndipo yalipozidi, akaanza kujipiga na makuta na kuvuja damu. Hapo wa dini zote wakasoma aya zao, jamaa alikuja akawaambia tu huyu kashakwisha tayari, niliwaambia mumuweke TV lounge mkajifanya wabishi. Akarudishwa kwao bara, akafariki maskini.

*****Katika kijiji icho icho, kuna jamaa alikuwa na jahazi yake katoka kupakia mizigo anasafirisha kuelekea Pemba na mombasa. Wakati anasafiri, maji yalikuwa ni low tide, kwa bahati lile jahazi likagonga mwamba na kutoboka, maji yalianza kuingia ndani lakini hayakuzamisha jahazi kwa sababu hakikuwa kina kirefu, sema jahazi lililala upande. Mwenyewe akashuka na kuliangalia, akaanza kusikitika, alitokea mzee from nowhere, akamuuliza shida nini kwani, jamaa akamuelezea akamwambia usijali utaondoka hapa, jahazi lilipigwa makofi na likainuka na kuendelea na safari. Hii siwezi kusema kama kweli au uwongo, alienipa hii habari ni mtu wa hapo kijijini na alikuwa serious, mana alikuwa ananipa mikasa ya kijijini kwao.

Sasa nilioshuhudia mwenyewe kwa macho, sio ya kutisha kiivo, naamini uchawi upo, lakini kwanza napenda kufikiria kuwa ni mambo yanayoeleweka kwanza kabla ya kuconclude ni uchawi.

******Nilitoka kazini mida ya saa sita usiku na kwenda staff house, nikatulia natizama documentaries youtube mpaka kama saa tisa inakaribia, nikasema niende nkaoge then nirud kulala tu. Niko kwenye shower maji yalikuwa baridi kidogo lakini si kiivo, nilanza kuona naishiwa nguvu, halafu kama kuna mikono mabegani yananisukuma chini, najiforce kusimama lakini nilishindwa nikajikuta nimekaa kwenye shower chini mzee sina nguvu, moyoni najisemea yale nnayoyasikia kweli yanataka kunitokea? basi sikufanya ubishi nikatulia kitako chini nikakubali nisiforce mwili kupambana, apo apo nikasema, au labda maji haya yalikuwa yabaridi. hapo bado maji yalikuwa yanatiririka. Nikajitahid kufikia mfereji kwa mkono nikapata ya maji ya moto, nikayafungua full nikarudi kupata nguvu nkasimama fresh. nikajisemea kuwa kama sababu maji ya baridi au ya moto, wacha nitoke chooni nkajilalie. Lakini akili ikanambia nimalizie tu kuoga, niliendelea kuoga na maji mchanganyiko yabaridi na yamoto yanatiririka lakini ya moto yalikuwa yamoto kweli mana hakukua na baridi, ebana hali ikajirudia tena, nikakalishwa chini, nikatulia hapo na nilipopata nguvu y kusimama nilivuta taulo nkaenda chumbani tu kulala.

****** Hii hapa ilikuwa nipo TV lounge hapo hoteli, baada ya kumaliza mechi ya Champions League tukabaki watu wawili tu tunatizama Tv mpaka saa nane usiku hapo mwangu ulokuwepo ulikuwa na wa TV na choo cha TV lounge tu hio Lounge tulizima taa, mara hafla nikasikia harufu nzuri sana, nikauchuna. ikapotea. Mara baada ya mda mfupi kidogo, nikasikia tena ile harufu hapa nikashindwa kuvumilia, nikamuuliza mwenzangu "Nasikia mie au na wewe umesikia?" Akaniuliza hio harufu? nkamwambia ndio, akajibu baba namie niliisikia mwanzo ikapotea ila ikarudi saivi, nkamwambia zima TV mzee baba tuwaachie wenye ukumbi wao. Tulisepa zetu tu.
 
Kumbe! Kuna watu huwa wanadai paka hutumiwa na wachawi kumbe wanapambana na wachawi pia!
Paka unaemfuga au hata wale tunaosema mapaka majizi, kama wanalalia kwenye nyumba yako, wanapambana na wachawi mkuu.

Hapa home nilipo, kila akifa paka lazima anakuja paka mwingine kuweka kambi na sijui wanatokea wapi. Na cha kushangaza mkuu, huwa sometime sipo home wiki nzima, hakuna msosi anaopata hutoka home, lakini huyu paka halali kwa jirani. Huyu paka wakati yupo mdogo, nilimgawa kwa majirani mana walimtaka, alipokuwa tu ameruka ukuta na amerudi hapa home. Sasa ivi tayari naona kuna paka mwengine ameanza kujisogeza sogeza, wanapokezana vijiti kuishi hapa nlipo 😀
 
Paka unaemfuga au hata wale tunaosema mapaka majizi, kama wanalalia kwenye nyumba yako, wanapambana na wachawi mkuu.

Hapa home nilipo, kila akifa paka lazima anakuja paka mwingine kuweka kambi na sijui wanatokea wapi. Na cha kushangaza mkuu, huwa sometime sipo home wiki nzima, hakuna msosi anaopata hutoka home, lakini huyu paka halali kwa jirani. Huyu paka wakati yupo mdogo, nilimgawa kwa majirani mana walimtaka, alipokuwa tu ameruka ukuta na amerudi hapa home. Sasa ivi tayari naona kuna paka mwengine ameanza kujisogeza sogeza, wanapokezana vijiti kuishi hapa nlipo 😀


Paka wanatunza kumbukumbu balaa labda kama ungemgawa akiwa mdogo sana angesahau alipotoka.
 
Back
Top Bottom