Njoo tusimualiane Mambo ya kutisha/kuogopesha uliyowahi kushuhudia hapa Duniani

Ni wazi alex alikufitini[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Hehee nmeona mmeelezea mmenipa courage ya kusimulia na mimi kisa cha ajabu ajabu kilichonitokea..(mtanisamehe sio muandishi mzuri) nlifanikiwa kusoma shule ya boarding na ilikua ni mixture..boys na girls...kuna binti mmoja mrembo sana shuleni alikua anamaliza kidato cha sita yani ni mwaka wake wa mwisho na sisi newcomers form five tulibahatika kumkuta hapo.. basi huyo binti watoto wa o level waliokaa muda mrefu shuleni ambao ni boyz wakawa wamempachika jina wanamuita mpenzi jini.

nilidhani ni sababu ya uzuri wake tu na nyimbo ya z-anto ndio ilikua inatamba sana kipindi hicho hivyo nikapuuzia..nlibahatika kupata ukiranja na eneo la kusimamia usafi nililopatiwa alikuemo yeye na sikuwahi kumuona akilifanyia usafi na sikuwahi kulikuta chafu..hakua na marafiki kwa sababu sikuwahi kumuona akiongozana na mtu yoyote shuleni kama best yake..sasa sijui huko mabwenini alala wapi na vipi.nikawa sijisikii vizuri kila siku namkosa kwenye eneo lake na sijawahi kumkuta na nlitamani sana hata nimuongeleshe si ushaelewa mtoto mkali..

basi nikatega kamtego siku kwenye eneo lake nikampa kakazi cha kubuni tu ambacho sijatumwa na yoyote kwamba eneo lake ni njia ya kwenda ofisi ya mkuu wa shule so maua fulani ya kitenge yatapendeza nikamwambi jioni nitamsaidia kupanda akakubali lakini kwa dharau sana alinionesha.. basi jioni nikawa charming sana mpaka nikamjua na jina lake na akanizoea.. sasa kisa kikaanza usiku huo baada ya kumzoea nikiwa usingizini nmelala bwenini kwangu nikaota yupo hapo pembeni ya kitanda changu akiniambia kamwe nisirudie kumsaidia kazi nimpe atajua anafnyaje mwenyewe..asabuhi nikapuuzia ndoto tu tukakutana foleni ya chai hii sio ndoto sasa akaniambia nadhani umenielewa nlichokwambia jana usiku. Nikashituka sana hadi nikajiuliza alikuja bwenini kweli au?

Sasa muda wa kwenda asembly nikapita eneo lake yale maua tuliyopanda jana yake yalikua yameshaota na yamekua makubwa kitu ambacho hakiwezekani kabisa..tangu hapo nikawa naanza kumuogopa ila nikawa na kiununda fulani hivi najifariji kuwa labda network zangu kichwani hazisomi vizuri labda kuna jambo limenipita si unajua kuna muda unatafuta kasababu cha kujitia moyo. Nikaja piga story na madogo wa olevel kwanza wakanishangaa nimewezaje kuzungumza nae pili wakanisimulia visa vyake ambavyo nikadharau tu hawa madogo na shule yenyewe ya bush washamba maana kulikua na shida ya maji shule ilikuwa sehemu ya ukame ila hakuwahi kuonekana akihangaika na maji wala kuwa mchafu na mara zote alikua akinukia marashi tu..

nkasema washamba hawa watoto.. kisa kikubwa zaidi kikafuata usiku uliofuata tumemaliza prepo nikamvizia wanapotoka madarasa yao kumuhoji huwa anafanya usafi eneo lake saa ngapi akanijibu anafanya usiku wa manane nkamuacha nikasepa mbioo.. usiku huo wa manane nikiwa mzima najitambua nlimuona dirishani kwangu just imagine bweni za boyz na hairuhusiwi girls kuwepo na ulinzi wote ule alifikaje pale. akaniambia huu ndio muda nafanya usafi na akatoweka sikulala usiku mzima nlijaribu kuamsha roomates walizidiwa nanusingizi hakuna alienisikiliza nkakesha mpaka asubhi nikajiandaa kwenda assembly nikiwa natetemeka maana lazima tuonane nankweli asubhi nikamkuta assembly na akaniangalia huku akitabasamu nliogopa sana nikaamua kukimbilia ofisi za taaluma zilipo jirani cha ajabu naingia ofisi ya hizo za taaluma namkuta tena humo ofisi yabi asemmbly yupo na taaluma yupo..

nlipioteza fahamu na nligoma kurudi shule kabisaa nliwasimulia walimu na wazazi na ikabidi nihamishwe tu shule ila shobo na kilanga viliniingiza chaka...lakini wenzangu woote wanamuona tu na hakuna aliyewahi kuwa na habari nae.. na kila mlipojaribu kufanya utafiti hakuna aliyrmzoea kabisa anaishi kivyake... hata walimu darasani hawajawahi muhoji au kumpa kazi yoyote na nlipowauliza walimu (hapo nikiwa nawenge hospitali) mnawezaje kufanya nae maswala ya kitaaluma shule walimu majibu yaoo hata siyaelewi wanasema tunamuona darasani tu na assembly na kazi zabdarasani anafanya ila hakuna aliyewahi kumuuliza maswali wala kushughulika naekielimu na hao walimu hawajui kwanini kila mtu shule hajawahi mtilia maanani huyo binti..

waliniambia tu majina yake mawili ndio ikaishia hivyo.. mpaka sasa sijaelewa ni nini kilikua kinaendelea na binti yule pale shule
 
Du ilikuwa hatari.
 
Duuh,jina lake nani huyo binti??
 
Ulitaka kujionyesha kua wewe ni mtoto wa mjini, wenzio ni washamba
 
Pole sana Mkuu.
 
Pole sana mkuu. Ila Nimecheka [emoji23]. Pole sana
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]Aisee majini yapo bhasi
 
Si kweli.Mambo ya kufikirika ukiyazingatia Sana hugeuka kuwa kweli.Ni hisia

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Ni balaa
 
Ngoja namimi nisimulie changu kifupi kidogo, ni huko huko maeneo ya shule za Boarding school,

Nipo form four tupo tunasoma prepo( hii ni kujisomea usiku yani) lakin hapo sisi ni ile prepo ya kuanzia sa 5 usiku hadi sa 7, sasa hapo madogo wengine wa madarasa ya chini wameshakwenda kulala tumebak form 4 tu, sasa kuna manz mmoja alikuwa ni mzuri sana anatokea Dom alaf pia ni kichwa class ( ndio mwenye tukio)

Napiga zangu Doria hapo nimechoka kusoma nakuta darasa moja watu wanafanya maombi ile kama wanakemea mapepo alaf wamewasha mishumaa (school yetu tulikuwa tunatumia generator so madarasa mengine umeme ulikuwa aufiki) sasa namimi nikaingia kulikuwa na washikaji wawili walokole wa shulen hapo na demu mmoja mlokole pia na huyo manzi mkali ndio kaweka kati anaombewa sasa kwenye kuombewa nikashuudia kwa macho yangu anatapika kucha kavu yani kucha zinamtoka mdomon baadae nywele zikawa zinamtoka pia.

Daaahh aiseeee baadae wakamchukua wakamsindikiza bwenini nakumbuka siku mbili baadae ndio nikawauliza wale waliokuwa wanamuombea mmoja akanijib ni miujiza, sikumuulizaga yule manZi kwasabab sikutaka ajifikkrie vbaya maana ndio maana ilikuwa inafanyika kisiriri kwenye kumuombea.
 
Kudadeq.......ungemla kimasihara
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…