Njoo tusimualiane Mambo ya kutisha/kuogopesha uliyowahi kushuhudia hapa Duniani

umesema vyema,mimi ni mmoja wa watu hao,nimewahi kuona wachawi usiku,mchawi akija nikiwa ndotoni kuna ndoto fulani ni ngumu kuieleza huwa naiota

story ni ndefu sana lakini kwa ufupi, kuna siku nilikuwa nimelala wakati nipo darasa la nne,ghafla nikastuka kutoka usingizini na kusikia sauti ya watu wanaimba,nilipotazama vizuri (kulikuwa na taa ya umeme) nikawaona hao wachawi na wakapotea ghafla

juzi kati mida ya saa tano usiku tupo Home tunapiga stories huku mlango ukiwa wazi nikaona kivuli cha mtu kama kile cha ukitembea juani kinatembea usiku
 
Nilienda mkoa fulani bana muda mwingi niliutumia kukaa kwetu nilivyoanza kutoka sasa kusalimiana na watu na wazee bana bana nilijuta, mauza uza yalianzia apo usiku nilikuwa naombea usifike kabisa maana yalikuwa mateso, yai nalala kuna barid ila nahis kama nyoka au dubwasha linanibana mara kitu kije kiondoke mara nihis kama navutwa utumbo, mara joto lipande na moyo kwenda kasi sanaaa, yanivurugu mpaka nikasema naondoka yani sikukaa ule muda niliopanga kukaa kule,
Ila nilisali sana ilisaidia kwakeeli ila ile hali nilishindwa kuvumilia
 
Umenikumbusha mwaka 2009 nikiwa nasoma form six shule moja wilayani Njombe miaka hiyo.

Ilikuwa usiku wa saa nne na dk kadhaa.Mimi na kijana mwenzangu tukiwa maeneo ya shule, tulikutana na bibi wawili wazee sana baada ya kutuona walicheke kicheko kirefu na baada ya sekunde kadhaa wakapotea machoni petu...baada ya sekunde kadhaa walitokea Dada wawili warefu sanaa kiasi cha kuogofwa wakiwa na nguo zao nyeupe na safi haswaaa mbele letu kiasi kwamba hatuwezi kusonga mbele bila kuwapita...Kwakeli tulipata nguvu ya kukemea kupitia jina la YESU punde Wakatoka mbele yetu kama upepo.

Kwakweli tulipoteana kidogo baada ya kwenda bwenini tukawa tunaelekea eneo lingine kabisa, baada ya kama dk moja akili zikarudi katika Dunia hii nakujua kuwa tulikuwa tunaelekea eneo lisilo sahihi.Tukarudi bwenini salama.
 
Mi binafsi sijawahi kuona mambo ya kutisha Sana ila nmeshuhudia utaalam wa hayo mambo.

Nina mjomba wangu anaishi msumbiji huwa anakujaga Tanzania kuwasaidia watu wenye matatizo mbali mbali ila somehow ni nyang'au na Mimi ni rafiki yangu sana so huwa ananiambia kila kitu and huwa haogopi ananiamini sana.

Kuna siku Kuna msanii mkubwa tu wabongo flava 2012 alikuja home Mtwara anataka kusafishiwa nyota sijui sasa alifatana na mwanamke mmoja anadai ni mke wa mkubwa serikarin anataka kumtuliza mmewe sijui asa uncle tukiwa pale chumbani night akamwambia yule mama anahitaji nywele za sehem ya Siri za mmewe Yule mama Hana na haezi safiri Kwenda Dar usiku ule mi niko nachezea sim huku naskiliza uncle akamwambia atoe 200k atume kijana afate Dar. mama akauliza itachukua siku ngapi uncle akacheka akamwambia saizi tu zinaletwa. Mi nikapause kidogo sikuelewa kauli nikasema uncle mbona kama anataka kumpiga chnga la macho huyu madame anapataje nywele ziko Dar within few minutes. Sasa bhana mama kishingo upande akasema sawa, bas uncle akajifunika nguo nyeupe baada ya kupewa jina kamili akaongea ongea kidogo na kiarabu juu then akajifunua story zikaendelea na mambo mengine. Ndani ya dakika kama 10 hizi akawanyamazisha akachukua karatasi nyeupe kama anakinga kitu juu ile kutua chini nywele hizi hapa [emoji23] kazi ikafanyika asubuhi yule mama anakuja anatuambia mmewe kampigia na meseji katuma katuonesha anasema amtafute mtaalam huku Mtwara maana anahisi wakubwa wenzake wanamchezea wamemnyoa nywele zote za Siri am'bebee dawa ikibidi maana ye alimuaga amekuja Mtwara kufanya survey ya mazao [emoji23][emoji23] bas nilishtuka nikamuuliza uncle imekuaje akacheka akasema nitakusimulia kesho. Akanambia vyote alivyofanya.

Cha pili Kuna mtu alimuagiza alete kunguru mzima ambae sio mkubwa Sana jamaa akasema hawezi winda kunguru kwanza wasumbufu atapata shida uncle akasema leta 20k ya supu nkuwindie ile jamaa kutoa pale pale unlce kaongea ongea nini sijui kunyoosha mkono juu akatua kunguru toka juu ya mwembe Hadi mkononi hii sikushtuka nlicheka maana jamaa akawa anamwambia uncle amrudishie hata buku 10k maana kamshika kirahisi [emoji23][emoji23] uncle akampa buku5 Tu [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Experience yangu na uncle imenifanya niamini haya mambo

Ahsanteni
 
[emoji38][emoji38][emoji38]
 
Newala iyo[emoji3][emoji3][emoji3]
 
Na cc wenye matatizo ya kutolala ucku hatuna element za kichawi kweli??

Sent using Jamii Forums mobile app
Fanya mazoezi walau nusu saa kabla ya saa 10.kisha ukielekea kulala tafuta mbegu zinaitwa shomari au kwa kiingereza Kennel seeds pika chai ya vijiko viwili ya hiyo chuja pooza kunywa ukielekea kulala.utaamka asubuhi hakuna cha ndoto wala mchawi
 
Mjomba wako nipo tu hapa nakufuatilia.
Oooya [emoji23] sema labda asiwe kwenye harakati Tu maana na sijataja jina lake. Ukilitaja Tu anajua anaeza akupigie simu anakuambia Uncle punguza kuniongelea afu anakucheka [emoji1787] afu anapenda pisi vibaya mno
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…