Njoo tusimualiane Mambo ya kutisha/kuogopesha uliyowahi kushuhudia hapa Duniani

Njoo tusimualiane Mambo ya kutisha/kuogopesha uliyowahi kushuhudia hapa Duniani

Mungu aliumba vitu vinavyoonekana na visivyoonekana. Na kwa Bahati nzuri akaweka kizuizi kwa kupitia uwezo wake wa kiungu hili tusiweze kushuhudia viumbe hivyo ambavyo havionekani kwa macho yetu ya kibinadamu isipokua kwa utaalamu flani wa mambo ya kiroho.

Viumbe hivyo vikiwemo , Malaika, Majini , Wachawi pamoja na viumbe vingine vya kutisha sana, ikiwemo wanyama wa ajabu wenye ukubwa wenye kutetemesha na kuogofya kwa wanadamu wa kawaida.

Danieli 7:4 “Wa kwanza alikuwa kama simba, naye alikuwa na mabawa ya tai; nikatazama, hata mabawa yake yakafutuka manyoya, akainuliwa katika nchi, akasimamishwa juu kwa miguu miwili kama mwanadamu; naye akapewa moyo wa kibinadamu.”

Danieli 8:3 “Ndipo nikainua macho yangu nikaona, na tazama, mbele ya mto alisimama kondoo mume, mwenye pembe mbili; na pembe zile mbili zilikuwa ndefu; lakini moja ilikuwa ndefu kuliko ya pili, na ile iliyokuwa ndefu zaidi ilizuka mwisho.”

Danieli 8:5 “Nami nilipokuwa nikifikiri, tazama, beberu akatoka upande wa magharibi, juu ya uso wa dunia nzima, bila kuigusa nchi; na beberu yule alikuwa na pembe mashuhuri kati ya macho yake.”

Danieli 7:6 “Kisha nikatazama, na kumbe! Mnyama mwingine, kama chui, naye juu ya mgongo wake alikuwa na mabawa manne kama ya ndege; mnyama huyo alikuwa na vichwa vinne; akapewa mamlaka.”

Wengi tukisoma Habari kama hizi za kuona simba mwenye vichwa vinne na miguu kama ya binadamu, beberu mwenye pembe kumi, nyoka mwenye vichwa saba na wanyama wengine wa kutisha, tunajipa moyo na kusema hiyo ni lugha tu ya biblia/ lugha ya picha hakuna viumbe kama hivyo. Ila ukweli ni kuwa viumbe hivyo vipo na vinaishi kwenye ulimwengu mwingine tofauti na huu wetu unaonekana. Na kuna binadamu wenzetu wameshashuhudia kabisa kwa macho yao.

Tuachane na hayo na turudi kwenye maada yetu ya leo . Tuzungumzie kuhusu mikasa ya kutisha ambayo tumewahi kukutana nayo kwenye ulimwengu huu ambayo kwa namna moja au nyingine vimekuacha midomo wazi na kukufanya uwe traumatized.

Ngoja nianze na mikasa / mambo ya kutisha niliyowahi kukutana nayo hapa duniani ambayo mpaka sasa hivi bado najiuliza kama ni viini macho au ni kweli , lakini ukweli unabaki kuwa ni kweli .

1. Jini kuchomoza baharini na kuelea hewani.

Nakumbuka ilikua ni usiku wa manane, nikiwa kwenye harakati za ushikirikina Uko sehem( sipendi kutaja jina). Nikiwa na mganga akiendelea kufanya mambo ya kishirikina baharini, Ambapo alisema anaita kiumbe( jini) hili anitimizie haja zangu . Kwa akili yangu nilijua tu ni danganya toto, hakuna lolote. Baada ya kama dakika 45 za yule mganga kufanya ushirikina wake. Ghafla akatokea mwanamke mrefu tofauti na urefu wetu wa kawaida wa binadamu alikua baharini anaelea tu, miguu haionekani kwa kweli nilikimbia, Bahati nzuri wale wasaidizi wa mganga wakanikamata kunizuia nisikimbie. Uzuri hakua anatisha wala nini, alikua tu ni mwanamke wa kawaida ingawa alikua na urefu usio na kawaida, na alikua kakasirika sana, alikua analalamika tunamuita sana tuna shida gani.....

2. Niliwahi kushuhudia kwa macho yangu , binadamu akiwa nusu mtu , nusu simba, Ana sura ya kutisha sana , mbaya mfano hakuna, ilibaki kidogo tu nizimie.

3. Binadamu mfupi kama stuli, Ana ndevu nyingi mpaka chini na alikua na mguu mmoja tu , na macho yake yanawaka moto.

4. Mzimu wa mtu maarufu ambaye alikufa miaka mingi iliyopita.

Hii ndo mikasa ya kutisha niliyowahi kukutana nayo hapa duniani, ambayo kiukweli mpaka leo inanipa shida sana, na ilichukua miaka kadhaa mpaka kuweza kukubali hii hali mpaka kufikia kuzoea kidogo. Ila hapa duniani kuna viumbe vya ajabu mno, na kama ukitaka kuviona unaweza.

View attachment 1430585



Sent from my iPhone using JamiiForums
Mkuu mbona kama fix hivi? Yaani kama zile shuhuda za walokole za kutunga?!
 
Dah imenikumbusha miaka ya 90s nikiwa Tabora wilaya moja hivi kijijini nikichukua elimu ya msingi shule yetu ilikuwa upande wa magharibi kuna makaburi halafu shule ina miti kibao ya mikaratusi,mikorosho mijohoro mizambarawe na miti fulani hivi inatoa ubani upepo ukipiga inavuma kama gari,

Dah nakumbuka hiyo siku niliamka kwenye kigheto changu pale home kama saa nane hivi mabalamwezi imekubali nje maana ilikuwa wiki ya mwalimu mmoja hivi kusimamia usafi na wechelewaji na ukichelewa unapata bakora za miguuni na lile baridi la kijijini balaa mwanaume mbalamwezi ile nikajua kumekucha nikanawa faster faster hata sikuwastua wazazi ambapo sio kawaida huwa lazima niwaamshe kwenye gheto lao mzee nikanyanyua ufagio mkononi na kidumu cha maji mbio kwenda kabla ya kufika shule kuna kipori fulani lazima ukipite ndio ufike shule mwanaume sikujari japo njiani sikuona mtu yeyote hiyo haikunistua mie nilijona mshindi leo nawahi namba shule,

aisee nimepita chini ya mikorosho na hiyo miti mingine bila kujari nahisi akili haikuwa yangu nakumbuka nafika shule nikakimbilia darasani nafika mlangoni nilichokishuhudia acha niliona moto mkubwa unawaka mule na kuna watu wamekaa kama wako kwenye kikao halafu wote wakaniangalia ila sura sikuziona hapo ndio akili ikarudi kwamba nimezingua niligeuka mbio kurudi home halafu ule upande wa makaburi nilishuhudia watu wakiwa na mguu mmoja wanaruka ruka kwa mstari mbio zangu nilikuwa nahisi kuna kitu nyuma kinanifata kugeuka nyuma niliona mtu mrefu sana kichwa hakionekani ila kavaa vazi refu linag'aa kama mbaramwezi ilivyokuwa inag'aa mwanaume niliongeza speed nilienda nikaingia na mlango mpk ndani yule jini sijui nini nilipokaribia nyumbani nilisikia msonyoo mmoja hatari sana wazazi wakaamka kufungua mlango kuja kunikuta sijitambui wakanichukua nikaenda kulala kwao asubuhi ndio kuwaelezea ni moja ya tukio ambalo huwa sipendi kabisa kulikumbuka maana baada ya hapo mpk leo kuna vitu huwa naviona ambavyo sio vya kawaida na niliwasumbua sana wazazi baada ya hapo . nimejaribu kufupisha ila kuna mambo mengi sana kwa ule usiku na miaka ile niliyashuhudia baada ya ilo tukio.
Waalimu wa shule za msingi miaka ya nyuma walikuwaga wakuda sana halafu wapenda sifa yaani kuna mwalimu zamu yake mnahesabu bamba saa kumi na moja alfajiri!
Sasa wengi ilitutokea kuamka usiku wa manane ukiona mbalamwezi unajua kumekucha unakurupuka kuwahi kumbe bado ucku!
 
Nikiwa na miaka 9 au 10 hivi nilikuwa naishi mkoa mmoja pembezoni mwa Tanzania. Siku moja nikiwa nacheza mpira barabarani na wenzangu mpira ulimgusa (sio kumpiga) bibi mmoja aliyekuwa anapita hapo barabarani.

Bibi aliinama na kuuokota ule mpira. Akaushika mkononi. Nikiwa sina hili wala lile nilimfuata yule bibi na kumtaka anipe ule mpira niendelee kuucheza na wenzangu. Bibi alikataa. Akauliza kwa ukali kwanini ule mpira umempiga. Nikajibu ni bahati mbaya lakin pia ni kwamba umemgusa tu hivyo haujamuumiza. Nilisema hayo maneno huku nikinyoosha mkono ili niuchukue mpira kutoka mkononi mwake.

Lakini bibi alikuwa kadhamiria kutonipa ule mpira. Akawa anataka labda nibembeleze lakin mim sikuona kosa tulilofanya hivyo sauti yangu na matendo yangu yakawa sio ya kubembeleza wala kuomba msamaha. Nikazidi kunyoosha mkono kuelekea ulipo mpira mkononi mwake na yeye akazidi kurudisha mpira nyuma ya mwili wake.

Alivyoona sielekei kutulia wala kubembeleza akautupia mpira kwenye majani yenye miiba miiba kando ya barabara. Nilikereka sana. Sijui hata kwanini. Nikamropokea maneno mabovu. Ilikuwa sio kawaida yangu lakin kwakweli nilisema maneno ambayo si mazuri kwa mbibi kama yule.

Nafikiri ni ujinga wa kitoto au vile nlikuwa na kiherehere cha kutaka kuendelea kucheza haraka na nilijua fika kuutoa ule mpira kwenye miiba ile kutanichukua muda mrefu maana inabidi niwe makini na niingie polepole sana ili nisichomwe.

Sasa baada ya kumtamkia neno mbofu yule bibi aliondoka bila kusema neno. Yaani aliurusha mpira majanini, mim nikamtamkia neno la ovyo wakat anaondoka na alisikia.

Nilichukua dakika chache kuutoa halaf nakumbuka hata dakika 2 hazikupita tangia nianze tena kucheza nikaanza kujisikia kuumwa. Dalili zote za kuumwa nilikuwa nazo. Nguvu sina. Kichwa kinauma, joto limepanda.

Nikawaambia wenzangu naondoka naumwa. Wakashangaa. Nikaenda kujilaza nyumban. Dingi akaenda kuitwa shamban. Akakuta nimelala mkekani, naumwa. Si kawaida mim kuumwa, zaman mpaka leo. Niko hivyo. Na nikiumwa sio wa kulala. Sasa kunikuta naumwa mpaka nimelala wakat lisaa limoja kabla nilikuwa njema kabisa alishangaa sana.

Akauliza naumwa nin nkajibu najskia tu kuumwa. Dingi aliuliza vitu vingi nilivyokula au kunywa lakn sikuwa nimekula wala kunywa chochote tofaut na vya pale maskani.

Katika kudadisi zaidi ndo ikaibuka stori ya bibi tuliyempiga na mpira. Dah, duh, loh. Dingi akafura. Haraka akatuma watu wawili wamfuate fasta sana bila kuchelewa.

Bibi akafika home. Dingi macho yakiwa yamemuiva akaanza kumkoromea bibi. Akatishia kumkata kata na mapanga. Akaanza kuongea mengi yanayosemwa juu ya bibi na kwamba yeye atammaliza na hata muda huo anataman aingie ndani achukue panga amkatekate. Dingi yangu alikuwa mkali sana lakin sikuwahi muona akiongea kwa ukali na kudhamiria kama siku ile. Dingi akasema nipone muda huo huo lasivyo atamfuata kwa mumewe akamuulie hapo. Bibi akafukuzwa aondoke haraka kabla hajafuata panga ndani.

Bibi aliongea kwa unyonge kuwa ni bahati mbaya nimeumwa ila nitapona tu. Akanyanyuka aondoke. Dingi macho mekunduuu, midomo inatetemeka kwa hasira

Ajabu sana. Ile bibi anapotea tu machoni petu yaani kafika mita 30 hivi kapitia kwenye mahindi na mihogo ya pale maskani hivyo hatumuoni mim nikaanza kuzungusha macho kutafuta mpira uko wapi. Nikauona. Nikanyanyuka. Nikauchukua huyooo mbio barabarani tena kucheza, nishapona hivyooo

Niko fiti kabisa na kwa muda huo bibi atakuwa hata 1 ya 10 ya safari ya kufika kwake hajaimaliza. Ndugu na jamaa wanakuja kuniangalia mgonjwa mim niko bize kwenye mpira nishapona. Nimepona ponaje? Niliumwa umwaje?

Mkwara wa dingi ulisaidia japo najua dingi yangu akili zake alikuwa anazijua mwenyew kumkata kata bibi alikuwa hatanii. Baadae ndo nilikuja kujua kuwa bibi alikuwa anaugua mpaka anakufa halaf anafufuka. Pia nilikuja kujua kuwa bibi alikuwa anaoza nusu ya mwili wake mpaka funza wanatoka lakin hafi. Kumbe Bibi alikuwa master wa uchawi pale kijijini

Hiki ndo kinanifanya nibabaike sana ninaposikia uchawi haupo na kwamba kama upo eti unawakumba wanaoamini tu. Sasa mimi mbona nilipigwa dafrao na bibi wakat nilikuwa sijui kama bibi ni master?

Kama haupo ilikuwaje mimi kuumwa baada ya kumkera yule bibi? Ikumbukwe sikuwa na background information yoyote juu ya uchawi wa yule bibi na nilikuwa simwogopi. Na yule bibi alikuwa na mjukuu wake wa kike nilikuwa nasoma nae darasa moja na siku ya tukio alikuwa ameongozana nae na alikuwa best yangu

Ijapokuwa kipindi kile sikutishika (sababu ya utoto?) lakin lile tukio ndo linanifanya mpaka leo niamin uchawi upo na ukijaa kwenye anga za wachawi wanaweza kukufanya kitu mbaya
Hatari sana.
 
Mimi nitasimulia kisa kimoja tu, tena cha utotoni maana kiliniogopesha sana kwa umri ule wa miaka isiyofika hata kumi. Hiki ni kisa kati ya visa vingi vya nguvu za giza nilivyovishuhudia, na ninavyoendelea kuvishuhudia mpaka kesho. Mnivumilie na mnisamehe mdogo wenu maana nitaandika kurasa ndefu.

Picha linaanza pale marehemu mama(PKA mama yangu mzazi, na Mungu akurehemu kwa rehema zake) alipoolewa na baba yangu. Kwa miaka zaidi ya mitatu, mama hakuweza kukaa na ujauzito zaidi ya miezi mitatu, na badala yake mimba ziliharibika.
Mama aliisha kwa masimango, na kuonekana sawasawa na papai linalobeba corona badala ya vitamin! (Ni mchezo uliokuwa ukichezwa na majirani zetu, wenyej wa Kigoma, na Ukweleni hapo)....Lakini mama hakuchoka kuvumilia, na kumwomba Mungu.

Hatimaye mama akashika ujauzito wangu, haukutoka tena, na nikazaliwa pale MNH, na nikaitwa jina la "dawa ya Mungu", maisha yakaendelea kijijini kwetu Boko.

Katika makuzi yangu, utotoni wazazi wangu walikumbana na matukio na changamoto nyingi za kukatisha tamaa. Kuna wakati usiku mama alimka na akakuta sipo kitandani, ananitafuta kwa mda mrefu wakiwa na mzee, hatimaye wananikuta chini ya uvungu wa kitanda nalia, au wananikuta kwenye pembe ya nyumba, mama alikuwa akilia weee, hatimaye maisha yanaendelea. Ilifika mda nikiwa na umri wa mwaka na nusu, nililishwa nyama ya kisigino ya maiti, niliumwa sana kutikana na hili chupuchupu nilambe udongo, wazazi walipambana, Mungu akasaidia, nikatoka salama.

Balaa kwa macho yangu, lilikuwa hapa sasa. Nikiwa darasa la pili, miaka hiyo ya tisini nilitokewa na tukio la kwanza, mubashara ambalo lilinitisha sana maana hapa niliona kwa macho na akili zangu. Usiku nikiwa nimelala ghafla nywele nikahisi zinasisimuka, damu inaenda mbio, na mwili unachemka....ghafla nikashtuka na kuamka paaap! Uso kwa uso na mwanaume aliyeshika kitanda changu, miguuni mwangu nywele zake zinawaka moto mkubwa ila haziteketei, macho yake yanawaka moto kama mkaa wa moto, na mikucha mirefu.

Kulia kwangu, wanawake wanne wakiwa uchi kabisa, wamebeba vyungu kichwani vinawaka moto. Kushoto kwangu wanaume watatu wapo uchi nao wamebeba vyungu, nao vinawaka moto, na mtu mmoja wa kiume(jini) mrefu akikaribia kugusa paa, mweupe kwa rangi(mwarabu) amevaa miwani mweupe, kanzu ndefu, nyeupe mpaka chini, na alikuwa na ndefu ndefu kiasi.

Tukakaziana macho sana, nikawa nawageukia wote mithili nataka niamke niwarukie ila nahisi nazuiwa, nataka kupiga kelele sauti haitoki. Baada ya dakika kama 3 au 4, nikaanza kuuona ukuta kwenye pembe ya nyumba, mubashara unafunguka na wanaanza wanawake kutoka nje kinyumenyume, wakifuata wanaume, na yule jini anakuwa wa mwisho. Hatimaye ukuta unajifunga tena baap! Na hatimaye ndo sauti inatoka mamaaaaaaa........!!!

Mama na baba wanakuja, wananikuta nalia na nimeloa jasho mwili mzima. Hatimaye nawasimulia, mama analia sana, ananikumbatia, na anamlilia Mungu, ananichukua ananipeleka chumbani kwake kwenda kulala nao chumbani kwao. Mama akaniambia watoto ni malaika, huona majini na wachawi ila ukikua hutowaona. Ila haikuwa hivyo mimi mpaka kesho hawa washenzi hawakatishi anga zangu.

Asubuhi ikafika, nikajiandaa kwenda zangu shule, na mama akaniambia kwa sasa hali ilipofikia itabidi niwe nalala na mbwa chumbani kwangu, yaani mbwa anafungwa kwenye mguu wa kitanda changu. Hii ilinisaidia ila hawa washenzi walimuua mbwa wetu(PKA Jeck) ni mbwa aliyepambana sana na hawa washenzi, ila usiku mmoja alipiga kelele kushtuka damu zinamtoka puani na mdomoni ndo ukawa mwisho wake Jeck wangu.

Hili ni tukio mojawapo kati ya matukio mengi niliyokumbana, na ninayokumbana nayo. Ila kama ukilala unaamka tu flesh bila kuona haya mavitu, muombe Mungu akujalie hivyo hivyo. Haya mavitu yanatisha sana.
Asanteni, na poleni kwa kuwachosha!

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe ni mbadhiri wa Mungu tangu utotoni,

Wewe ni mtu ambaye asili Yako ni Kutoka juu,

Nikiseme mengi hapa, ila dumu katika kumtumikia Mungu.

Ubarikiwe 🙏
 
Dah imenikumbusha miaka ya 90s nikiwa Tabora wilaya moja hivi kijijini nikichukua elimu ya msingi shule yetu ilikuwa upande wa magharibi kuna makaburi halafu shule ina miti kibao ya mikaratusi,mikorosho mijohoro mizambarawe na miti fulani hivi inatoa ubani upepo ukipiga inavuma kama gari,

Dah nakumbuka hiyo siku niliamka kwenye kigheto changu pale home kama saa nane hivi mabalamwezi imekubali nje maana ilikuwa wiki ya mwalimu mmoja hivi kusimamia usafi na wechelewaji na ukichelewa unapata bakora za miguuni na lile baridi la kijijini balaa mwanaume mbalamwezi ile nikajua kumekucha nikanawa faster faster hata sikuwastua wazazi ambapo sio kawaida huwa lazima niwaamshe kwenye gheto lao mzee nikanyanyua ufagio mkononi na kidumu cha maji mbio kwenda kabla ya kufika shule kuna kipori fulani lazima ukipite ndio ufike shule mwanaume sikujari japo njiani sikuona mtu yeyote hiyo haikunistua mie nilijona mshindi leo nawahi namba shule,

aisee nimepita chini ya mikorosho na hiyo miti mingine bila kujari nahisi akili haikuwa yangu nakumbuka nafika shule nikakimbilia darasani nafika mlangoni nilichokishuhudia acha niliona moto mkubwa unawaka mule na kuna watu wamekaa kama wako kwenye kikao halafu wote wakaniangalia ila sura sikuziona hapo ndio akili ikarudi kwamba nimezingua niligeuka mbio kurudi home halafu ule upande wa makaburi nilishuhudia watu wakiwa na mguu mmoja wanaruka ruka kwa mstari mbio zangu nilikuwa nahisi kuna kitu nyuma kinanifata kugeuka nyuma niliona mtu mrefu sana kichwa hakionekani ila kavaa vazi refu linag'aa kama mbaramwezi ilivyokuwa inag'aa mwanaume niliongeza speed nilienda nikaingia na mlango mpk ndani yule jini sijui nini nilipokaribia nyumbani nilisikia msonyoo mmoja hatari sana wazazi wakaamka kufungua mlango kuja kunikuta sijitambui wakanichukua nikaenda kulala kwao asubuhi ndio kuwaelezea ni moja ya tukio ambalo huwa sipendi kabisa kulikumbuka maana baada ya hapo mpk leo kuna vitu huwa naviona ambavyo sio vya kawaida na niliwasumbua sana wazazi baada ya hapo . nimejaribu kufupisha ila kuna mambo mengi sana kwa ule usiku na miaka ile niliyashuhudia baada ya ilo tukio.
Hii imewahi kunikuta japo mimi sikukutana na vitu vya ajabu tofauti na manyau makubwa ambayo hadi leo sijapata kuona nyau wakubwa namna ile
 
Mk

Mkuu huyu mtoa maada alishatangulia mbele za haki mda kidogo .
huyu mganga nilenda kwake kwa maelekezo ya ndugu yangu
niliyakuta na kufanyiwa sitasahau. mwisho nikagoma kuendelea na akaniambia hapo tulipofikia na kuyafanya tuyatunze mioyoni mwetu, yaani iwe siri. naogopaga hata kusimulia
Mimi naijua dini ila sometimes najitoaga ufahamu na kufanya ya duniani, hivyo nina ka hirizi kangu natembea nako
juzi kati nikawa safarini kwenda dasalam, nikasema ujinga huu kutembea na hirizi kwenda jijini, nikaiweka kwenye kimfuko cha pembeni ya begi
kufika sehemu ya kuchimba dawa ,ile nanyayuka, maumivi makali kwenye nyonga, nikasema labda sababu ya kukaa sana, nilikuwa seat ya mwisho .Nimekaa dar siku nne zote nameza dawa za maumivu ya nyonga,lakini wapi, yapo tu
Jioni ambayo kesho yake narudi bara, nikasema ngoja nichukue kahirizi kangu nikakaweka mfukoni. Maumivu yakapotea ghafla.
Mpaka leo silewi kilikuwa ni nini
Mshana Jr
Bado unako hako ka hirizi? Mtukutu wa Nyaigela
 
Back
Top Bottom