Njoo tuwashauri viongozi wa Yanga

fimboyaasali

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2011
Posts
8,617
Reaction score
8,244
Kama wewe ni mwananchi njoo tuwashauri viongozi juu ya mambo yafuatayo:

1. Usajili wa wachezaji, je wansajili nani na wamuache nani msimu ujao?

2. Je, kocha yupi aongezwe ambae kwa sasa hawana?

3. Tathmini ya klabu tayari kwa kuuza hisa,unadhani ni kampuni ipi au mtaalamu yupi anafaa kufanya kazi hiyo?

4. Ujenzi wa miundo msingi ni kifanyike wajenge kiwanja, hostel, hospitali na ununuzi wa vifaa vya muhimu vya mazoezi nashukuru kwa wote mtakaosoma na kutoa maoni kwenye yzi huu
 
kama wewe ni mwananchi njoo tuwashauri viongozi juu ya mambo yafuatayo:

1. Usajili wa wachezaji,je wansajili nani na wamuache nani msimu ujao...
Kwa sasa nitajikita tu kwenye kipengele cha miundombinu. Natamani kuona Yanga wanamiliki uwanja wao wa kisasa na uliokamilika kwa ajili ya mazoezi, mechi za ligi kuu, na pia zile za Kimataifa.

Haiwezekani miaka zaidi 80, tangu klabu ilipoanzishwa mpaka sasa wanajivunia uwanja wa Kaunda. Inashangqza pia kuona vilabu vilivyoanzishwa miaka ya juzi kama Azam, Ihefu, nk vinamiliki viwanja vyao, halafu ukija kwa timu kubwa na kongwe kama Yanga, haina uwanja wake binafsi.

Kuhusu usajili na benchi la ufundi, nitashauri wakati mwingine.
 
Kwa sasa nitajikita tu kwenye kipengele cha miundombinu. Natamani kuona Yanga wanamiliki uwanja wao wa kisasa na ulio.
Ili binafsi napingana na wewe, labda uwanja wa mazoezi pekee nitakubaliana na wewe.

Ila uwanja wa kuchezea ligi kuu hilo halina faida kwa Tanzania ni kuwapa tu ulaji watu.

Kwanza sheria za TFF zibadilishwe katika swala la mgawanyo wa mapato. Haiwezekani kuwe na makato mengi kiai hiko ( VAT, TFF, bodi ya ligi, BMT, DFA)
 
Ili binafsi napingana na wewe, labda uwanja wa mazoezi pekee nitakubaliana na wewe. Ila uwanja...
Kwani hayo makato yatawaathiri Yanga tu! Vipi kuhusu Azam, Ihefu, nk! Yaani uwanja wa Taifa ukifungwa kwa ajili ya matengenezo au ratiba nyingine, basi ni sahihi kabisa kwa timu kama Yanga kwenda kucheza Chamazi Stadium!

Unaona ni sahihi kabisa wakati wa Pre season Yanga kwenda kukodi maeneo ya kufanyia mazoezi, huku timu ikiwa na umri sawa na mzee kikongwe!! Miaka zaidi 80, Yanga iendelee tu kutegemea viwanja vya serikali, kwa sababu ya kuhofia makato!!

Aisee katika hili, hapana.
 
Ushauri wangu.

First task iwe ni kuwabakiza benchi la ufundi na wachezaji muhimu.

Second, wasajili winger moja matata sana ya kuteleza yenye uwezo wa ku cut in na kufunga. Pia waongeze kiungo no 🔟 alete changamoto kwa waliopo.

Walete center back kusaidiana na waliopo. Na walete striker kama backup ya mzee wa kutetema na musonda.

Mwisho japo sio kwa umuhimu; uwanja ujengwe hata kwa harambee au ubia.
 
Ndio maana nimesema kuwa kwa uwanja wa mazoezi nakubaliana nawe ila kwa uwanja kwaajili ya mechi unachookoa ni kiasi kidogo tu. Kwanza kilichopaswa ni kupaza sauti kwa haya makato mengi yasiyo na maana. Kihesbabu tu unadhani kama uwanja wa Yanga umeingiza mapato ya sh milioni mia tano kwa mechi moja, je kutakuwa na tofauti kubwa kiasi gani katika kiwango anachokipata Yanga kwa kuchezea viwanja vya serikali kwa mapato hayo hayo. Point yangu sio kwamba ni nani atakayenyonywa bali napingana na sera ya TFF ya unyonyaji katika mgawanyo wa mapato ya viingilio.
 
Waambie Bahati haiji mara mbili.
 
maoni mazuri
 
asante
 
Kuwekeza kwenye team za vijana na wanawake.

Kubakisha wachezaji muhimu kwenye team.

Kuwekeza katika facilities za kisasa kama vile vifaa vya michezo.

Kuandaa mipango madhubuti kuelekea kwenye mashindano ya kimataifa mwakani.
*We must have consistency in each year.

Kuongeza pato la team.

#since 1935[emoji172][emoji169].
 
Azam ndio wanakiwanja kwa maana ya stadium, huyo Ihefu ana play ground.
 
Uwezekano wa kulibakiza benchi la ufundi ni mdogo sana, hapo kwa Mayele angalau kunaweza kuwa na matumaini.
 
asante kwa maoni yako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…