Wacha nimshushie mistari mrembo wangu.
Duniani kuna wengi,
Lakini kwako nimenasa, mtoto umeumbika utadhani ni Cleopatra wa zama hizi.
Rangi yako ya kupendeza, na ngozi yako nyororo ukichanganya na sauti yako mwanana, unifanya nipagawe.
Umahili wako katika mahaba, ni dhahiri umefundwa pia ukafundika.
Kwani asili yako mapenzi ni jadi yenu,
Uko wapi mpenzi nikupigie zeze na kukuimbia,
Nikupe maneno matamu ya huba na mahaba.
Mapema nitafika kwenu wazazio niwaone, niwaombe ruhusa mwanao nimtwae.
Wenye vifaru na mizinga wameshindwa kuniteka,
Lakini wewe kwa mahaba na maneno matamu umefanikiwa kuniteka.
Wanakuita shunie, lakini mimi upenda kukuita shuni, mtoto portable kifuani mwangu unaenea.
Love you.