Njoo tuwasifu wapenzi wetu kwa Mitindo huru/freestyle.

Bro acha zako
Kitambo najua mambo yako
Na hizo fikra zako
Narudia najua tatizo lako
We Bado bikra hujawahi kugusa kunako
So tuheshimu kaka zako
Sisi Toka kitambo tupo na dada zako
Dada zangu wapi,
Unachukua makapi.
Njoo nikupeleke ohio,
Kama kweli pesa unayo
 
Walikufuata matajiri visenti vya chenge
Ukakataa kuvaa gucci ukafuata Vitenge
Mi ni wako we ni wangu kwanini usiringe
Penzi lako dawa tosha siendi samunge [emoji4][emoji4]
Wacha kumdanganya mtoto wa watu kwa maneno ya kizembe,
Unamwambia uongo we mtulivu wapi we jamaa kiwembe,
We mkulima we mvuvi mchimba chumvi usijiite jembe,
Mtoto hataki perepeche bila pesa utapelekwa king'ombe
 
Demu huna? [emoji23] [emoji23] John cena basi rudi wrestlemania

Hapa ni mitongozo ya kirusi wana tunakaba mpaka cremia

Washikaji tupo in da area


Tuna teka kuku wote Cena Kausha vifaranga wacjelia
Uwezo wangu mkubwa muulize dabi kaka yako,
Mke wa mtu mi siibi mtaani natoka na dada yako,
Wajanja penati hatukabi tuna kismati cha mzee wa upako,
Ukizingua sikupigi nakuchana freestyle za nako2nako
 
Wacha nimshushie mistari mrembo wangu.

Duniani kuna wengi,
Lakini kwako nimenasa, mtoto umeumbika utadhani ni Cleopatra wa zama hizi.

Rangi yako ya kupendeza, na ngozi yako nyororo ukichanganya na sauti yako mwanana, unifanya nipagawe.

Umahili wako katika mahaba, ni dhahiri umefundwa pia ukafundika.
Kwani asili yako mapenzi ni jadi yenu,

Uko wapi mpenzi nikupigie zeze na kukuimbia,
Nikupe maneno matamu ya huba na mahaba.
Mapema nitafika kwenu wazazio niwaone, niwaombe ruhusa mwanao nimtwae.

Wenye vifaru na mizinga wameshindwa kuniteka,
Lakini wewe kwa mahaba na maneno matamu umefanikiwa kuniteka.

Wanakuita shunie, lakini mimi upenda kukuita shuni, mtoto portable kifuani mwangu unaenea.

Love you.
 
Moyo wa ushairi vina. Vipo wapi vina vyako. Shunie usije [emoji125] [emoji125] [emoji125]
 
baby najihisi kunenepa sio kwa mistari hii [emoji8][emoji8] love you too hun.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…