Numbisa
JF-Expert Member
- Dec 12, 2016
- 301,221
- 1,172,274
Hawa ni bata wale wafugwao,kama ilivyo kwa kuku bata hawa pia wanauzwa masokoni na wachinjaji hadi wanyonyoaji wapo huko huko sokoni,wananyonyoa na kukukatia katia nyama vizuri,pesa yako tu inaongea.
Nyama yake ni tamu sana hasa ukipatia kumpika vizuri na kumkaanga.
Mahitaji
Nyama ya bata
Tangawizi
Kitunguu swaumu
Chumvi
limao\ndimu
Maji
Mafuta ya kupikia lita moja
Jinsi ya kupika
Osha nyama vizuri weka limao na chumvi,kisha tenga jikoni,maji ya kwanza yakishakaukia weka ya pili kiasi.(hii inasaidia kuilainisha nyama na pia kuondoa mafuta kwa wale wasiopenda mafuta ya bata)
Twanga tangawizi na vitunguu swaumu. Maji ya pili yakishakaukia sio sana,epua sufuria changanya kwenye nyama vitunguu swaumu na tangawizi rusha rusha au geuza geuza kwa mwiko mpaka vichanganyike vizuri.
Tenga kikaangio jikon,weka mafuta ya kukaangia,acha yachemke kisha weka nyama kiasi kaanga mpaka ziwe rangi ya kahawia zinakua zimeshakaangika vizuri,toa kwenye mafuta weka kwenye chombo safi,fanya hivyo kwa nyama zote.
Baada ya hapo nyama yako itakua tayari kwa kuliwa unaweza kula kwa ndizi,chips,wali,ugali,pilau nakadhalika
Vitunguu swaumu na tangawizi zinaleta harufu nzuri na ladha murua
Unaweza kufanya hivi pia kwa nyama ya kuku etc