Njoo ujifunze kutengeneza masweta, kofia na soksi za watoto ndani ya mda mfupi ujiajiri!

Njoo ujifunze kutengeneza masweta, kofia na soksi za watoto ndani ya mda mfupi ujiajiri!

Fahari

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2014
Posts
1,044
Reaction score
698
Ndugu wanabodi,tunafundisha utengenezaji (ufumaji) was masweta,kofia,scarf nk kwa kutumia machine.Ada yetu ni tsh 300,000/=(laki tatu ).Mda Wa mafunzo ni miezi 2 lakini tunaweza kuongeza mwezi mmoja bure iwapo hujaelewa.Tunapatikana Tabata,DSM.
 
Karibu ujifunze ujuzi ambao utajiajiri kwa urahisi ,kumbuka shule zote wanafunzi wanahitaji sweta.
 
1517601295435.jpg
 
Dah bonge la fursa, nitakutafuta aiseeee, hii ni fursa adhimu saaaana, nashangaa vijana wamejazana kule kwenye mapenzi. Natamani Mods wauweke sticky huu uzi
Vijana wamelala
 
Tunaweza pia Kutoa mafunzo kwa vikundi mikoani.
 
Je, baada ya mafunzo mwanafunzi atalazimika kununua mashine maalumu kwaajili ya kazi yake ya kujiajiri?
Kama ndio je, hiyo mashine mnaiuza nyie?
Na inauzwaje?
Au mkono pasipo mashine utamaliza kazi zote?
Mbona hamjaweka wazi kipengele hichi cha means of production?
 
Mkuu Mpelengana, means of production ni machine,hata hivyo sisi hatuziuzi.Kazi yetu sisi ni kukufundisha namna ya kutengeneza masweta na hivyo vitu vingine.Baada ya kupata ujuzi unaweza kununua mashine kutoka kwa wauzaji.Kuhusu bei inategemea na ukubwa wa mashine,aina ya mashine na features zilizopo kwenye machine husika lakini minimum laki tano unapata machine.
 
Back
Top Bottom