Njoo uwekeze kwenye biashara ya mafuta (Fuel) kwa laki 1 tu kama kima cha chini

Kwanini msisajiri kampuni yenu kwny STOCK MARKET zinazoeleweka hapa nchini.

Ili Tukawafate huko huko kusaini MIKATABA

Kuliko hii ya KUSAINISHANA mikataba UCHOCHORONI

Bila utaratibu rasmi Unaotambulika kisheria kuhusiana na hizi ishu za SHARE HOLDING

Naomba ufafanuz



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna watu wanaenda pigwa hapa
Mafuta faida yake ni 200 hadi 500 kwa lita
Kwa mtaji wenu nyie mtanunua kwa hawa wakubwa maana yake faida imepungua tena sio 500
Hao watu 100 wakijichanga kwa 2mil kila mmoja ni 200mil ambayo mtafanikiwa nunua tanker 2 kwa mkupuo
Faida huwez pata ya kuwagawia wote 10pc ya uwekezaji

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kwanza naomba nifafanue vizuri kuwa sisi hatuuzi shares bali unawekeza pesa yako kama unavyoweka fixed deposit bank, kisha utakua unalipwa 10% ya pesa uliyowekeza kwa kila mwezi bila kuathiri pesa yako uliyowekeza. Kumbuka pesa hii utakayolipwa inatokana na faida tunayopata kwenye biashara yetu, hivyo shares hazihusiki hapa mkuu.

Pili tunasainishana mikataba kwa mujibu wa sheria ndio maana tunakuruhusu kuleta mwanasheria wako ili ujiridhishe kuwa unachoenda kufanya sio longo longo wala utapeli.
Karibu tufanye biashara mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo kampuni yako haina jina?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu napenda kukufanulia kuwa baishara ya mafuta haiko hivyo kama ulivyoandika jaribu kufanya utafiti. Napenda kukufahamisha kuwa 10% ya 200 mil ni 20mil tu ambayo ni pesa ya kawaida sana kwenye faida ya Kituo cha mafuta kwa mwezi. So biashara hii ni tofauti sana na unavyoandika mkuu na usipate woga kuijaribu siku moja ili uujue undani wake!

FYI wala usiongelee tankers mbili nyingi sana hizo ni lita elfu 80, hata nusu tanker tu lita elfu 20 pekee inaweza kutoa hiyo 20 mil kwa mwezi na kampuni ikabaki na faida nzuri tu!
Karibu sana tufanye biashara mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ofisi iko wapi na kituo cha mafuta iko wapi
 
Tuambie mkuu mafuta na gesi ipi. Ni kampuni ya uchimbaji au wanauza hizo bidhaa moja kwa moja je ikitokea kampuni imepata hasara mtafanyaje kumlipa muwekezaji

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Faida ya 10% kwa mwezi,sidhani kama mtatoa hiyo kwa muda wote.Ungesema 10 or 20 kwa Mwaka ningewapa kipaumbele kidogo.Waelezeni wawekezaji ukweli,iyo faida mnayotarajia in kubwa sana,hats makampuni ya DSE hayatoi kiwango hiko kwa Mwaka,yaani almost 120%profit per year.
 
Nikiwa kama mfanyabiashara Uliposema tu muwekezaji hatahusishwa na hasara ndo uliponipeperusha........hio deal wazungu wanasema ni "too good to be true"
Kwani mkuu ukiweka bank fixed deposit then kwa bahati mbaya bank ikapata hasara pesa yako itapotea ama utaipata? So huo ni mfano tu mkuu, ungekua shareholder ndio ungehusika kwenye hasara haya mbona yanafanyika sehemu nyingi tu Duniani mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu hapo juu nimeeleza ni kila baada ya miezi 3 tunapitia mkataba wetu, sasa mambo mengine yanabadilika kulingana na wakati. Utaratibu huu wa 10% pesa uliyowekeza inawezekana sana mkuu, yani sana tu. I wish ufike ofisini nikuonyeshe mifano halisi ya wanufaika waliowekeza pesa zao. Karibu sana mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mafuta mnanua wapi na mna7zia wapi mpaka mpate faida ya 10% kila mwezi? Labda kama mnayatoa Nigeria kwenye zile meli za wizi halafu mkiimport hamlipi kodi. Lakini Tanzania faida ya mafuta nyie kama sio importer haizidi 200/_ unaponuna 2500/_ kwa Lita. Kama wewe ni mkweli changanua tuone mtaji na faida uweke wazi. Ila kwa kuwa watanzania wasivyokuwa makini utawapata . halafu ukishapata mtaji utakuwa umewapa mtaji wao ndani ya miezi 10 halafu kampuni hewa itasambaa, na hapo utakuwa mjungwana sana, vinginevyo hiyo ni deck iliyoboreshwa wtu waibiwe nakampuni iyeyuke .sasa kama mafuta yana faida kubwa hivo he yule Kijana Forbes inamtambuakuwa ni mtanzania Kijana mwenye bilioni 30 so kia mwaka utajitiri ungekuwa maradufu kila mwaka?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…