Njoo uwekeze kwenye biashara ya mafuta (Fuel) kwa laki 1 tu kama kima cha chini

Njoo uwekeze kwenye biashara ya mafuta (Fuel) kwa laki 1 tu kama kima cha chini

Hii ndo pata potea,shoka linaungua mpini unabaki na soksi inavuka mguu unabadi ndani ya kiatu[emoji1544][emoji1538][emoji1550]‍♂️[emoji1550]‍♂️[emoji1550]‍♂️[emoji1550]‍♂️[emoji1550]‍♂️


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naomba wahusika wafute huu Uzi, mhusika ameshindwa kujibu maswali Muhimu.
 
Mwanzo niliposoma uzi nilipatwa na presha ya matumaini ya ajabu, lakini kadri ninaposoma comments presha inashuka pole pole.
 
Location ya business kwa petroleum product kwa Chanika unaweza uzaa ltrs 20,000. Per month uka generate loss ya more than ten million per months
 
Mkuu sisi tuna Kituo cha mafuta yani retail service station, mafuta yetu tunanunua depot yoyote yenye bei nzuri ya soko kwa siku husika. Ni kweli faida mara nyingi haizi 200 ila naomba nikufafanulie kwa faida ya wengine pia.
Kwa mfano sisi kwa mwezi tunauza lita laki 3 kwa faida ya 150 Tsh kwa kila lita ni 45 million baada ya Matumizi utapata net kama 39 to 40 million.
Sasa let's assume we umeweka pesa yako million 5 that means utapata faida laki 5 out of 39 million, na wengine wote utaratibu utakua ni huo huo. Kumbuka tuna limited number of people that means pia tuna Kiwango cha pesa za uwekezaji ambazo ni target means ukifikia hapo tutafunga dirisha la uwekezaji! I hope umenipata vyema mkuu, karibu ofisini kwetu ujuonee physically!

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu angalia hesabu zako vzr, Lita laki 3 kwa wastani wa 2,000 kwa Lita ni uwekezaji wa milioni 600 bila kuhusisha fixed asset yoyote! Sasa kama utapata faida ya milioni 40 net means umepata faida ya chini ya 10%. 10%ilitakiwa iwe milioni 60! Sasa wewe ukigawa 10% kwa wawekezaji kila mwezi utakuwa unapata hasara ya 20m ambayo lazima iwe inatoka kwenye mtaji au sehemu nyingine! Hapo napata doubt. Simple mathematics bila hata kushika kalamu na kuandika. Ebu nifafanulie hapa
 
naona dalili ya kuanza kurejesha madeni ya benki kwa ujanja baada ya kushindwa kurejesha kwa mapato yenu; badala ya kufilisiwa na benki mmeamua kuingiza pesa kwa ujanja kwa njia hii. semeni ukweli mmekopa na kushindwa kurejesha mnahitaji pesa
 
Kuna point 2 zinanipa shida,
Moja ni kwanini mwanahisa anahusika na faida tu lakini hausiki na hasara.
Mbili...
Je biashara hii ikitokea hasara pesa ya kuwalipa wanahisa inatoka katika mfuko gani?
Na nyongeza ni kwamba ukokotozi wa mgawo wa wanahisa huwa unabase ktk faida iliyo ktk financial report. Sasa kama wanahisa hawaambiwi hasara, nyie kuna siku mtakosa cha kuwalipa wanahisa maana inamaanisha kuwa hapatakuwa na ukaguzi ktk fedha wala mahesabu ya kampuni.
Na nyongeza ni kuwa vp kuhusu isuarance ya mtaji??????????
Kama kampuni haina financial report haiwezi kujua km ina faida au hasara.

People be care this may be a scam
Ndio yale yale ya Mr. KUKU eti hasara itakuwa covered na bima ya AAR ya biashara 😂😂😂 matokeo ni kipigo cha mbwa kachoka.
 
Back
Top Bottom