Njooni huku Boko Mnemela viwanja vya bure

Njooni huku Boko Mnemela viwanja vya bure

Mkuu usalama wa viwanja na mashamba ukoje huko?
Tafuta mwenyeji mkuu, mimi nilifunga safari kwenda kutembea na kutafuta fursa, nika mwambia bodaboda anipeleke kwa mwenyeji...nje ya mji kijiji kinaitwa zumba.
 
Wadau hamjambo?

Nimehamia huku panaitwa Zumba mabanzini mkoa wa Pwani, kwa ufupi unapo toka Dar panda magari pale Mbezi yanayokwenda Boko Mnemela ukifika Boko Mnemela kodi boda boda elfu 6 mpaka huku Mabanzini.

LIFE YA HUKU
Huku wamang'ati bado wapo wamezuia maeneo, yaani nilichofanya nimemuhamisha mmang'ati kwa laki 8 eneo la heka 9

Bado bushi sema kanisa katoliki wamekuja juzi nao wanajenga hostel za masister na ndio wanafanya harakati za kuweka umeme.

Life ya huku ni ya ki nzuri maeneo mengi ni msitu na serikali imeweka bango ukisafusha eneo ndio lako nyumba ni chache ila vibanda vya wamang'ati na mashamba ya mahindi tu ndio mengi.

Yaani kwamimi niliekulia tarangire hapa nnahisi kama nipo home aisee ni kuzuri tambarare yake usipime huku watu wengi wafugaji, kuku, nguruwe, mbuzi, kilimo cha karanga, matikiti, mahindi, pilipili mwendo kasi, maziwa ya ng'ombe kwa wingi naona watu hawaja pastukia this gift land.

Karibuni sana
Mabanzini, Zumba
Sawa. Vipi bado mashamba.yapo?
 
Yaani niko hapa vegetables nakuja na vijana kusafisha eneo langu...sasa hao serikalo waje waseme ni eneo lao
 
Back
Top Bottom