Njooni tujadili: Jinsi ya kuendesha mradi huku umeajiriwa fulltime

Njooni tujadili: Jinsi ya kuendesha mradi huku umeajiriwa fulltime

mitale na midimu

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2015
Posts
10,420
Reaction score
17,735
Kwa utafiti wangu usio rasmi. Changamoto ya wafanyakazi wengi ni kusuasua kwa miradi na kutokuleta tija kama ilivyopambanuliwa katika Businessplan kutokana na ugumu wa ufuatiliaji.

Lakin pia nimeona watu wengi wamefanikiwa sana katika hili na miradfi yao iko vizuri na pia Kazini wako full time japo sijajua ni mbinu gani wanatumia.

Changamoto hizi zipo katika kufungua maduka ya mbali, Biashara, ila napenda tujikite katika kilimo zaidi.

Kuna mtu anasema ni bora kujenga nyimba kuliko kuwekeza katika miradi ya namna hiyo.


Great thinkers naomba tupeane uzoefu, changamoto na ushauli. Kwenye wengi hakukosekani neno.
 
Kwa kifupi ni ngumu sana maana lazima utaegamia upande mmoja na pia huo mradi utakua sio endelevu maana utafika sehemu moja itabidi uchague moja ya hivyo vitu viwili...
 
Nilijaribu kwenye kilimo,ila sikufanikiwa,maana nilikua namtumia mtu anisaidie kusimamia,pamoja na kwamba mwaka huu mavuno yalikua hafifu,ila nikagundua kuwa msimamizi alichangia kwa kiasi kikubwa,nilichoplan ni kwamba nature ya kazi yangu hainibani saaana,ntakachoamua kufanya ni kuhakikisha naenda mara kwa mara site,kuanzia hatua za awali....usimamizi wa karibu ni muhimu sana
 
Ni raisi sana kama utakuwa na utayali wa kufanya kazi kwa moyo bila kujari changamoto,inabidi uwe na team imara,hapa kwenye team imara ndio muimu sana sana,uwe na watu wahaminifu,wenye nidhamu na kazi pamoja na mradi anao uendesha,utayali wao na wako ufanane,uwape motivation nk
 
Back
Top Bottom