Ndagullachrles
Senior Member
- Jun 20, 2023
- 153
- 161
Wananchi wa Kata za Njoro na Kaloleni Manispaa ya Moshi wamevamia na kujenga makazi ya kudumu juu ya mtandao wa majitaka na hivyo kukwamisha Oparesheni ya kuzibua chemba zinazoziba.
Mbali na Hilo,wananchi hao wamekuwa wakitumia vibaya mtandao wa majitaka kwa kutupa takangumu kwenye mfumo wa majitaka na hivyo kusababisha chemba nyingi kuziba na kuwa kero kwa wananchi.
Meneja wa majitaka na usafi wa mazingira wa Mamlaka ya majisafi na uondoshaji majitaka,(MUWSA)mhandisi Philbert Nyangwe amesema kuvamiwa kwa mtandao huo kunakwamisha juhudi za mamlaka kuufanyia ukarabati.
Kwa mujibu wa mhandisi Nyangwe,mtandao huo ulijengwa na mkoloni miaka ya 1950 ulikiwa eneo la ukubwa wa kilometea 15 na Sasa una eneo la kilometa 90.
Amesema MuWSA inahitaji ushirikiano wa Mamlaka nyingine ikiwamo Idara ya mipangomiji ya Manispaa ya Moshi kuhakikisha wananchi waliovamia mtqndao huo wanaondoka.
"Mamlaka pia inakabiliwa na changamoto ya matumizi mabaya ya mtandao wa majitaka,wananchi wanatupa takangumu kwenye chemba na kusababisha mfumo wa majitaka kuziba"
Anasema MUWSA imekuwa ikitumia zaidi ya Milioni 200 kila Mwaka kama gharama za uendeshaji idara ya majitaka ikiwamo uzibuaji wa chemba .
Wakati wananchi waliovamia na kujenga juu ya mtandao wa majitaka,MUWSA pia inapamba na womvi la wizi wa miundombinu ya mfumo huo wa majitaka.
Wizi huo unahusisha mifuniko ya chuma iliyopo kwenye chemba hatua inayotajwa kuwa ni uhujumu uchumi.
Kwa mujibu wa mhandisi Nyangwe hadi Sasa zaidi ya mifuniko 27 imeibwa na kwenda kuuzwa kama vyuma chakavu kwenye viwanda vinavyoyeyusha vyuma.
Mhandisi Nyangwe anasema kila mfuniko mmoja wa chuma unathamani ya sh,laki tisa hivyo MUWSA imepatq hasara ya shilingi Milioni 24.300,000.