Nkosana Makate mbunifu wa "Tafadhali Nipigie" ageuziwa kibao, atakiwa kuilipa Vodacom Tsh 1.8 Billion

Nkosana Makate mbunifu wa "Tafadhali Nipigie" ageuziwa kibao, atakiwa kuilipa Vodacom Tsh 1.8 Billion

Stuxnet

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2011
Posts
18,875
Reaction score
29,427
Screenshot_20251029_065924_X.jpg

Mbunifu wa huduma ya ‘Please Call Me’, Makate, ametakiwa kulipa Vodacom R13 milioni (Tsh 1.8 Billlion) kama gharama za kisheria

Mgogoro wa muda mrefu wa kisheria kati ya mbunifu wa huduma ya “Please Call Me”, Nkosana Makate, na kampuni ya Vodacom umechukua mwelekeo mpya wa kushtua, baada ya Mahakama ya Katiba kuamuru Makate alipe kampuni hiyo ya mawasiliano gharama za kisheria zinazokadiriwa kufikia takriban R13 milioni (Tsh 1.8 Billion)

Kwa mujibu wa MyBroadband, agizo hilo limefuatia rufaa ya Vodacom katika Mahakama ya Katiba, ambayo ilifuta uamuzi wa awali wa Mahakama ya Rufaa (SCA) uliokuwa umeamuru kampuni hiyo kumlipa Makate sehemu ya mapato yaliyotokana na huduma hiyo maarufu. Kesi hiyo sasa imerudishwa kwa SCA kwa kuangaliwa upya.

Mahakama ya Katiba iliamua kuwa, kutokana na “ukubwa wa rekodi, ugumu na upekee wa masuala yaliyopo, na kiasi kikubwa cha fedha kilichokuwa hatarini,” Vodacom ilikuwa na haki ya kulipwa gharama za mawakili watatu.

Makate, ambaye alibuni wazo la “Please Call Me” mwaka 2000 alipokuwa mfanyakazi wa Vodacom, amekuwa akipigania kwa miaka mingi kupata fidia anayoona kuwa ni ya haki. Vodacom hapo awali ilikubali kumlipa R47 milioni ( Tsh 6.5 Billion), lakini alikataa akidai anastahili asilimia ya mapato yaliyopatikana kwa karibu miongo miwili.

Licha ya changamoto hiyo, Makate ameapa kuendelea kupigania haki yake. “Mimi ni mtu mwenye uvumilivu,” alisema mapema mwaka huu. “Tutarejea SCA.”

Uamuzi huu unaongeza sura nyingine katika mojawapo ya kesi za kisheria za kampuni zinazofuatiliwa kwa karibu zaidi nchini Afrika Kusini. kesi inayojaribu kupima mipaka ya haki za ubunifu wa mali ya kiakili na fidia stahiki kwa ubunifu (intellectual property rights) wa wafanyakazi
 
mhhh hapo kweli pagumu.
mtu umemuajiri afanye kazi, kazi imekua nzuri anataja malipo extra, kwan hakulipwa huo mwezi?
 
Angekula zake 6.5 bilioni akapita hivi,sasa anaweza asipate hata mia na fidia akalipa.

Ila inaonekana anajua anachokifanya,kwahio anaweza kupindua meza
 
Back
Top Bottom