Nliishi kwa shida na kukaribia kufa ndani ya Miezi ya moto

Nliishi kwa shida na kukaribia kufa ndani ya Miezi ya moto

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2013
Posts
10,931
Reaction score
24,816
Hiki kilikuwa kipindi kigumu sana katika maisha yangu. Nlikonda ghafla, nikawa na mawazo wakati wote na nikawa nashawishika kunywa sumu. Nliona hiyo ndo ilikuwa njia rahisi pia kuniondolea mawazo na manyanyaso ambayo naelekea kuyapata.

Nlikuwa nimesafiri kwenda mkoa flani kikazi kama week 3 nikiwa huko nilipata kabinti flani kazuri kamemaliza form four. Nikawa namenyana nako.

Kale kabinti kwa kweli kalikuwa smart kalikuwa hakataki nikale mpaka niwe nimevaa kinga. So mara kadhaa tukawa tunaenda hivyo.

But mimi kwa kweli sikuwa naenjoy sana kutumia kinga. Nikawa najisahaulisha sometimes najaribu kuingiza bila kinga. Kananibadilikia kabisa kanaenda kabatini kanachukua ndom kananivesha.

Siku moja nikaamua kukachanganya.... Nikakaandaa sana. Mpaka kakawa kama kamelewa hakajielewi. Nikaingiza bila condom. Kakafurahi sana. Tumemaliza ndo kakashtuka. Kakalia sana na kusema nimekafanyia kitendo kibaya. Maana hatukuwa tumepima. Kweli kaliamua kuondoka.

Baada ya siku mbili nikakabembeleza sana kanisamehe. basi tukaendelea safari hii sasa ni ngadu kwa ngadu. Bila kinga maana tulisha rasimisha kutembelea rim.

Baadaye nikamaliza issue iliyonipeleka kule nikarudi Dar. Tukawa tunawasiliana kama kawaida pia sometime nakatumia pesa maana kalianza chuo flani.

Mpaka siku hiyo kamenipigia simu kanalia sana. Kanalia kakiomboleza na kunilaumu kuwa nimekaunga kwenye grid ya taifa. Kalienda kupima kakakutwa kana ngwengwe. Kakaniambia kumbe nlijua nimekanyaga miwaya halafu nikakafanyia makusudi.

Nlichanganyikiwa. Nikakakauliza kakasema kamepima na kamekutwa kamejumlishwa, yaani ni chanya umeme upo. Na kuwa hakakuwahi ku fanya bila condom toka kametolewa bikra.

Nliishi kwa mashaka sana. Nikifanya vikao mbalimbali kichwani mwangu na wadau kuwa sasa inakuaje. Nikapime au iweje. But nawaza kama nikienda kupima nikakutwa ninao si ndo nitachanganyikiwa zaidi. Nikaanza kuona maisha hayana faida. Sili nikashiba. Nikaanza kuwazia wazazi wangu na ndugu zangu..

Kutoka kilo 96 nlishuka mpaka 72 na hapo ndo nikaanza kuwaza zaidi. Ninao, ninao. Yule binti sikutaka tena hata kuwa naongea naye. Nliji feel guilty and yet sikujua kama ni yeye aliniambukiza au mimi.

Miezi 2 baadaye siku hiyo alinipigia sana simu. Sikutaka kupokea. Baadaye akatuma msg. Tafadhali pokea simu ni muhimu love

Kidogo nikashusha pumzi maana alishaacha kuniita hilo jina. Nikampigia. Alipokea kwa bashasha kidogo. Nikamuuliza kulikoni. Ndo kuniambia amepima mara 3 sehemu tofauti tofauti amekutwa hana ngwengwe. Ni hasi katika suala la umeme. Sikuamini. Nikamhoji na kumtaka aende tena kituo kikubwa cha kupima. Akaenda akaleta majibu yupo safi.

Anasema aliambiwa kuwa kuna vipimo flani kuna kipindi vilikuwa vinatoa majibu ambayo hayakuwa sahihi. Vikionesha watu wana ngwengwe kumbe hamna.

Nlishukuru sana. Sikwenda kupima mpaka miaka kadhaa mbeleni. Haya mambo kwa kweli si ya kuyafanyia mzaha wadau. Na hapo nazungumzia miaka ya 2000s. Hakukuwa na dawa nyingi za kufubaza kama leo hii.
 
Mlikua mna tumia simu gani mkuu .mimi ni mpenzi wa simu za zamani ovaa
 
mlkua mna tumia simu gani mkuu .mimi ni mpenzi wa simu za zamani ovaa
Utakuwa na umri mdogo sana. Kama hujui miaka hiyo kuna Nokia, Samsung, Blackberry, Sony Ericson etc. Anyway nadhani hizi kwa uchache utakuwa umezifahamu.
 
Back
Top Bottom