GwaB
JF-Expert Member
- Mar 19, 2014
- 4,291
- 5,786
Katika hali ya kushangaza NMB mmeamua kufunga kimya kimya matawi kadhaa mliyofungua kwa mbwembwe huko nyuma. Hata mawakala mliowapa ujiko wa kufungua matawi kwa niaba yenu mmewaacha solemba baada ya kuingia gharama kubwa za ujenzi au mmelipana kimya kimya pia?
Siku hizi mmekuja na upepo wa kila huduma kufanyika kupitia mtandao, lakini bado hamjawa mahiri kwenye eneo hilo kwa sababu hata hizi Apps mnazotegemea zinahitaji vijana wa IT wanaofahamu vizuri kazi yao. Ajirini basi wasomi hawa wawasaidie kupelekesha mambo. Kuwategemea hao vijana wa zamani waliobobea ku-balance mahesabu wawe ndio wabobezi kwenye IT, Hamtutendei haki tulioweka hela zetu kwenu. Tangu wameondoka waholanzi, ukweli usemwe mnayumba sana katika kutoa huduma zote tawini na mtandaoni.
Jirekebisheni.