pamoja na hayo wajitahidi wasambaze mtandao wa ATMs zao uwe mpana ili kupunguza jams kwenye matawi yao hasa mwisho wa mwezi, ingefaa wawaige ndugu zao NBC ambao wamejitahidi kusambaza ATMs kwenye filling stations nyingi kwahiyo wanapunguza kwa kiasi fulani misongamano kwenye matawi.
na kwa kuwa NMB ndiyo benki iliyopo vijijini pia wangejaribu kuweka atm kwenye miji midogo ili kupunguza adha waipatayo wananchi toka vijijini kuja wilayani kuweka au kuchukua pesa,kiasi kwamba matawi ya NMB yako always yamejaa wateja