NMB Mafinga Branch waja na maboresho ya huduma kwa wateja

NMB Mafinga Branch waja na maboresho ya huduma kwa wateja

President Elect

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Posts
693
Reaction score
212
Mimi ni mteja wa benki zaidi ya tano hapa nchini, nikijumuisha akaunti za bishara na nyingine za akiba kwa matumizi binafsi.

Kilichonifurahisha kama wiki mbili zilizopita nikiwa njiani kwenda Tunduma (mpakani mwa Zambia na Tz) ilinibidi kusimama kidogo mjini Mafinga, nikaingia benki ya NMB kufanya direct tranfer kwenye akaunti ya supplier kulipia mzigo. Nilikuta wametenga dirisha maalum kupokea fomu za funds transfer, hivyo ndani ya muda mfupi nilihudumiwa na kuendelea na safari yangu. Kwa kweli niliridhishwa na huduma niliyopata ukiachilia mbali muonekano mpya wa jengo na camera za cctv, vitu ambavyo zamani havikuwepo.

Big up NMB Mafinga Branch, keep it up!
 
Do you mean NMB wana huduma nzuri zaidi kuliko hizo zingine NNE???????
 
Do you mean NMB wana huduma nzuri zaidi kuliko hizo zingine NNE???????

Please note neno 'maboresho'. Kwa haraka niliyokuwa nayo na huduma niliyopata, kweli niliridhika. Benki nyingine ziko juu, na kadhalika baadhi ziko chini kutegemea aina ya huduma. Mfano; nikiwa nje ya nchi hupenda kutumia Visa/Mastercard, kitu ambacho NMB hawana! Ila kwa funds transfer kwenda ng'ambo ya nchi NMB wako fasta na gharama zao ziko poa kulinganisha na benki nyingine ambazo mimi ni mteja wao.
 
Back
Top Bottom