NMB: Makato mapya kwa wateja wa NMB yaja yakiwa yameongezeka mara mbili zaidi ya sasa?

NMB: Makato mapya kwa wateja wa NMB yaja yakiwa yameongezeka mara mbili zaidi ya sasa?

Jurrasic Park

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2013
Posts
3,801
Reaction score
6,806
Habari

Kama kichwa Cha mada kinavyojieleza ni kwamba tarehe 3/2/2019 Makato mapya kwa watumiaji wa benki ya makabwela yataongezeka Kama nilivyojaribu kudodosa.

Cash withdrawal fees kwa ATM mashine itakuwa ni sh.1150/= kutoka ile ya zamani sh. 940/=
Kutoa pesa kaunta itakuwa ni sh. 6,500/= kutoka ile ya zamani sh. 4012/=

Kuhamisha fedha kwenda benki nyingine itakuwa ni sh. 2,000/=

Kuweka hundi kutoka benki nyingine itakuwa ni sh. 1,000/= ambayo zamani ilikuwa no bure

Kwenye kutoa pesa kwenda kwenye mobile money hela yake ni Mara mbili ya sasa. Kweli uchumi unakua kwa 7.1/%

Ila mnyonge lakini Haki yake mpeni niwapongeze kwamba mmeondoa yafuatayo;

Monthly maintenance fee ilikuwa sh.1,900/= Sasa itakuwa BURE

Kuhamisha pesa kwa NMB mobile nayo itakuwa bure.

Sasa naona NMB inawahimiza watu mukaweke pesa zenu benki maana hazitakuwa na Makato ila ole wako ujifanye kwenda kuzidraw utafurahi na roho yako.

Kweli uchumi unakuwa tutembee vifua mbele
 
Monthly maintenance fee ilikuwa sh.1,900/= Sasa itakuwa BURE, haikuwa na maana maana kila transaction ulilipia; usiwapongeze kwa kuondoa wizi waliokuwa wanaufanya;
 
Kakope pia Bayport daaah, kopa 1100000/= unalipwa 800000, ukiwauliza unaambiwa RV imepanda cjui mara imeshuka yaani wizi mtupu.
Nawapa RAI watumishi BAYPORT wamekuja kivingine
 
Hizi benki zetu za Tanzania ....NMB na CRDB hazijui jinsi ya kufanya biashara za kibenki zaidi ya kubebwa na serikali na kuwaibia wananchi wanyonge. Kama kweli wanaweza hii biashara kwanini hawajitanui kama kcb na equity. Wao kuongeza mapato n kuiba tu kwenye rates zao
 
Kakope pia Bayport daaah, kopa 1100000/= unalipwa 800000, ukiwauliza unaambiwa RV imepanda cjui mara imeshuka yaani wizi mtupu.
Nawapa RAI watumishi BAYPORT wamekuja kivingine
Hizi microfinance ukienda ni kujiua kwa hiyari! Pia naskia ukienda kuomba salio ili uwalipe usepe wanagoma! Kuna ukweli hapo!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom