NMB mjirekebishe, mnakera sana huduma ya mikopo kwa watumishi wa umma

NMB mjirekebishe, mnakera sana huduma ya mikopo kwa watumishi wa umma

Halafu wanakata processing fee ya Nini wakati
1.fomu unazunguka nayo kusaini wilayani.
2.kuprocess mkopo ni kazi yao,kwa Nini uwalipe kwenye kazi yao? Wakati Kuna faida wanachukua? Ina maana Ile faida hawawezi kata processing fees mule?
 
NMB ndio benki yenye wateja wengi sana nchini karibia asilimia tisini ya wafanyakazi wa umma mishahara yao inapitia benki hii. Lakini tatizo kubwa la NMB kama benki mama ni huduma ya mikopo mbovu kwa watumishi wa umma kuna mlolongo na usumbufu wa kutosha kwa mtumishi hadi anashawishika kutoa rushwa kwa afisa mikopo za benki ili ahudumiwe haraka.

Mlolongo wa kutembea na fomu za mikopo hadi kwa wanasheria, maafisa utumishi na n.k ni tatizo na adha kwa mkopaji hasa mteja wa kudumu kama mtumishi wa umma.

Najiuliza kitengo cha IT cha benki hii kazi yake nini? Kwanini mikopo isitumie digital technology hadi mtu ahangaike na mafomu kibao wakati taarifa zinaweza zikajazwa na kutumwa moja kwa moja kwa maafisa utumishi?

Mtumishi wa umma taarifa zake zipo kwenye server ya halmashauri kwanini wasiwasiliane na maafisa utumishi moja kwa moja na kupiga hesabu za makato na mkopo husika? Kwanini mtumishi asipate mkopo moja kwa moja bila kufika benki kwa mawasiliano tu ya simu kama BAYPORT WANAVOFANYA KWA WATEJA WAO? Huduma ya salary advance ni nzuri lakini haikidhi haja ya watumishi wa umma.

NMB badilikeni tumechoka kutembea na mifomu ya mikopo wakati tungewasiliana moja kwa moja kwa njia ya simu na kuzijaza fom na kupatiwa mkopo bila kuhangaika kusaga soli mitaani kwenye ofisi za wanasheria kugongewa mihuri pia na maofisa utumishi kisa mihuri na sahihi wakati yote yanawezekana kidigitali.

Utakuta mtumishi yupo mbali na mji anataka mkopo !matokeo yake mlolongo mrefu una muumiza kwa gharama za kufuatilia mwisho wa siku anakimbilia kwa wanyonyaji kama Bayport na Platnum credit.

Badilikeni MNAWAAIBISHA NA KUWAVUNJA MOYO WATEJA WENU WA KUDUMU WATUMISHI WA UMMA!

Kama mna lolote changieni.

Karibuni.
Poleni sana watumishi wa umma. Fikirieni kuwa na SACCOS zenye nguvu ili kuondokana na usumbufu na unyonyaji wa wakopeshaji wanaotaka faida kubwa.
 
Back
Top Bottom