Kurenew mkopo mi procedure ya mwezi mzima nawambieni hamtafika popote kwa huu ujinga wenu.
Issue hizo unazoita mikopo uwe na heshima ,Ni pesa za watu wameweka kuna muda nao wana matumizi nazo
Usifikirie zile pesa unazokopeshwa ni za Bank ,Sio za bank hata kidogo ni pesa za wateja wengine kama wewe sema kwa wakati fulani hawana matumizi nayo ndio bank inakukopesha wewe
Mkuu kuna wakati bank zinapambana kupata deposit au pesa kwa wateja ili waweze kukukopesha wewe na wengine
Kama unaona kitu rahisi jaribu wewe kuweka pesa zako bila kuzitumia kwa miaka 5 au 7 ili benk ikopeshe wengine
Mikopo ina sheria zake ,Bank haikopeshi kama njugu au maharage
Kuna kiwango cha deposit ndio unaruhusiwa ukopeshe
Yawezekana NMB wamefika limit kwa BOT regulation kwa mwezi huo hivyo wanatafuta deposit zaidi
Bank sio pyramid scheme kama Desi au kalyanda,Bank zipo regulated na BoT
Unaruhusiwa kukopesha bila kuvunja margin/limit au ratios
Wewe unataka kukopa tu lakini kuweka hutaki,Bank itatoa wapi pesa za kukopesha kama nyie wawekaji mnaenda kuzichukua kila siku na kila mwezi
Think about it
Usilaumu tu ,Hapa JF ni kisima cha maarifa
Kama una swali kuna expert zaidi yangu watakusaidia pia
Have a nice day na uwe na subra