Camilo Cienfuegos
JF-Expert Member
- Apr 23, 2015
- 18,960
- 67,654
Benki ya NMB yazindua tawi jipya Buhigwe nyumbani kwa Makamu wa Rais Philip Mpango.
Makamu wa Rais wa Tanzania, Dkt. Philip Isdor Mpango leo ameipa Benki ya NMB baraka zake na kuzindua Tawi jipya la Benki hiyo Wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma na kuipongeza kwa uthubutu na kuwafuata Wananchi popote walipo na kuwaondolea kero Wananchi ambao walikua wanalazimika kusafiri umbali mrefu kufuata huduma hiyo na wengine kulazimika kutunza fedha majumbani.
Tawi hili la NMB Buhigwe ni Tawi la sita la benki hiyo ndani ya Mkoa wa Kigoma na la 229 kwa Nchi nzima ambapo kabla ya kufunguliwa kwake Wananchi kutoka Vijiji kadhaa walilazimika kutembea karibu kilometa 140 kwenda na kurudi katika Wilaya ya Kasulu kufuata huduma za kifedha za Benki.
Tawi la Benki ya NMB linakuwa la kwanza katika wilaya hii ya Buhigwe ambayo sasa imefunguliwa na kutarajiwa kutoa huduma zote za kifedha ikiwemo kufungua akaunti, kuweka na kutoa pesa, mikopo, kubadilisha fedha za kigeni, huduma za bima pamoja na ushauri wa masuala ya kifedha na biashara.