NMB Yazindua Hati Fungani ya Jamii Bond Yenye Thamani ya Shilingi Trilioni.Yavunja Rekodi ya Kijani Bond ya CRDB

Nina experience mbaya sana kuhusu kuwekeza pesa kwenye mabenki.

Nakumbuka miaka zaidi ya kumi iliyopita nilijaribu kuwekeza laki tatu hivi katika NBC (malengo akaunti) ili kutest mitambo. Sasa baada ya mwaka mmoja na miezi kadhaa kupita nikafika benki kutaka kucheck trend, nilichokikuta kilinihuzunisha sana. Haya ndio niliyokuta:
1. Niliambiwa siwezi kutoa chochote kwa kuwa akaunti yangu imefungiwa kwa sababu sijaweka pesa mara kwa mara!. (Nilipewa fomu ya kujaza, kuzunguka nayo ofisi kadhaa (ikiwemo za mwajiri wangu), kuweka picha ya passport, kuweka kiasi kisichopungua elfu 5 ili kuifufua)

2. Nikatakiwa kuandika barua ya kuomba kuchukua fedha zangu (faida), kusubiri siku kadhaa ili ombi langu kukubaliwa. Kwa wastani ilinichukua kama wiki mbili hivi.

3. Nilifika benki zaidi ya mara tatu na kila nikifika benki nilitumia zaidi ya masaa mawili ya kusubiria kupewa jibu (hakukuwa na foleni yoyote ya wateja). Njoo kesho, njoo kesho niliizoea!

4. Mwisho wa siku nilifanikiwa kupata pesa zangu kwa mbinde sana, lakini nikiwa nimepata hasara. (Niliwekeza laki tatu na nikaongeza elfu tano ya kuifufua akaunti yangu (jumla 305,000/=) halafu nikaja kuambulia 269,000/=, yaani hasara ya shilingi 36,000/=)
 
Halafu ndio hawa wakiingia 18 za mfilisi mkuu kila mteja analipwa mil. 2 hata kama alikuwa na amana za bilioni! Banking sector bado sana; too risky!
 
Dah! Mafisadi na wazee wa 10% watanufaika kweli na hizo bonds.
 
Halafu ndio hawa wakiingia 18 za mfilisi mkuu kila mteja analipwa mil. 2 hata kama alikuwa na amana za bilioni! Banking sector bado sana; too risky!
Hakuna kitu kama hicho
 
Bond za serikali ni nzuri. Ingawa zipo competitive sana na watu private wanapata lakini ni kwa ugumu.
Bondi iwe na faida angalau uweke 50M++++++
Hapo utakula bila jasho kweli.
In all ukitaka kukwepa laana za uzeeni na kuwapa laana za ajabu ajabu watoto wako, wekeza kwenye hii kitu.
 
Niweke million 10 nikapate laki 5 na point si bora nikanunue vidume vya ng'ombe nivinenepeshe
 
Tufafanulie tafadhali hatui hati fungani
 
Fafanua mkuu..japo kidgo
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…