"Alikuwa na raha sana alipopata mimba yake ya kwanza baada ya kushirikiana tendo la ndoa na mumewe miaka minne bila ya kupata mimba hata siku moja.
Bahati mbaya ikatoka akabaki na huzuni sana, na mumewe kamuacha baada ya mimba kutoka kwani amehisi kaitoa makusudi wakati ni bahati mbaya!"
Da Lizzy, kila mtu ana mapokeo yake pale apatapo mimba, kuna mwingine huwa na furaha sana kwani yawezekana ndio mtoto tu amekosekana kumalizia furaha ya ndoa. Lakini muda mwingine mambo huwa kinyume kabisa dada akipata mimba huanza kuwaza maisha jinsi yalivyo magumu na matatizo ya ndugu jinsi watakavyoipokea hivyo huamua kuitoa tu.