Cardinal Pengo,
Mie ni muumini wa Moravian Church na kwa hiyo nakuwa PROTESTANT. Ila siku zote siamini MAJENGO wala WATU. Kwa maana hii huwa sijali kama huyu ni kiongozi wa kanisa langu au sivyo. Sijali kama ni Muislaam au Mpagani. Huwa naangalia watu kwa matendo yao na maneno yao.
Nimekuwa MPINZANI mkubwa sana wa viongozi wa dini na kuwaita WALA VYA BURE. Mlituacha KONDOO wa Mungu kwenye malisho na kuwa mmeyafumbia haya mambo kwa muda mrefu. Nchi imeuzwa, imeliwa na wameiba kiasi cha kutosha. Mzee Mwanakijiji alipiga kelele kwenu bila mafanikio.
Sintauliza mlikuwa wapi ila lazima niseme kuwa kama nyie wakuu wetu wa dini mkiamua kulifuatilia hili, basi ninaamini mabadiliko ya kweli yatatokea. Kusubiri hadi CCM imeguke ili mabadiliko aliyoahidi JKNyerere yatokee ni kupoteza muda wakati huo Rostam Azziz na Edward Lowassa wanazidi kuimaliza nchi huku wakifuata nyayo za mtoto mliemlea (alilelewa na masista wa kikatoliki) ndugu Ben Mkapa.
Nina imani viongozi wengine wa dini watafuata nyayo na kuanza kukemea huu uchafu ili hatimaye nchi iweze kurudi kwa wananchi wenyewe. Na hapo tu, nyie mrudishe silaha zenu na kurudi kwenye madhabahu/kazi yenu kama alivyofanya Askofu Desmon Tutu wa South Africa.
Kardinal Pengo, hata Papa John Paul II alipoona unyama unaofanywa na Wakoministi kwenye jamii yake ya Wa-slovans (Russia, Czeck-Slowavia, Poland, Bulgaria etc) aliingilia kati na kuanza kuushambulia na mwisho AKAUVUNJA. Walitumia silaha na vitisho ila watu kwa kuamini maneno ya Papa, wala hawakuvunjika moyo. Walipigana hadi Mrusi na masilaha yake mazito, akarudi kwake.
Tuna imani kwamba Mafisadi pamoja na kutumia nguvu za dola, pesa na nyenzo zote zinazowafanya wawepo madarakani, muda wao umekwisha. Kama kweli mmekuja kutusaidia kupigana hii vita na MAFISADI, basi lazima niseme kuwa mmetimiza wajibu wenu haswaa. Nguvu ya viongozi wa dini ni kubwa kuliko vyama vya upinzani au waandishi wa habari. Kwenu nyie kila fisadi atagwaya.
Mungu akubarikini na kukupa busara kuongoza kondoo waliopotezwa na VIRANJA wao.
Endeleeni kuwa WACHUNGAJI wema na si wachungaji wa MAFISADI.
Mungu Ibariki Tanzania.