No comment - Kingunge

No comment - Kingunge

PENGO VS SIMBA? au PENGO VS JK? au PENGO VS CCM?. ingekuwa shekhe kasema maneno yale tena sehemu kama ile hivi sasa tusingemuona tena. letu jicho...

Why?? Nadhani wewe una agenda ya siri! i do not believe you at all.
 
Ama kweli CCM wamelewa madaraka hata hakuna wa kumwelekeza mwenzake.Yaani kule Dodoma kwenye mikutano yao , Kingunge achane chane waraka na kuutupa kapuni then wao waseme waunde kamati ya usuluhishi kwa lipi ? Yaani Maaskofu wakae waje na kitu cha kuwapa Watanzania Elimu ukidharau mbele ya waumini wa Katoliki kwenye NEC ya CCM then unategemea kanisa litasemaje ?

Pengo kaza buti tuko nyuma yako .Kama wanataka madhara wathubutu kuku summon kwa DCI waone .
 
Pengo kasema kitu sahihi sana na hasa pale anapotutaka wote tujiulize ni kwa namna gani tunachangia kwa kuuendeleza ama kuupinga ufisadi. Sina uelewa sana wa sheria lakini mtu unaposema huna comment manake unakubaliana na kilichosemwa na kama wewe ni fisadi basi unakubali kuwa unaendeleza ufisadi nahautaki utoke

UKWELI HATA UKIPINGWA NI KAMA UMESAKAFIWA KWA VUMBI, UPEPO UKIVUMA...
 
Walijifanya wanajua sana kuongea .......yes, waongee tena kutetea misimamo yao, why ''No comment''?
Next level,
Kama alipewa live JK na BWM akishuhudia,pana mtu mwingine kweli atakayecomment? The message was clear! Waandishi,mfateni Chiligati na Hiza msikie maoni yao pia!
 
No comment!! mbona uli comment, au baada ya pango NO COMMENT!!
 
Better late than never. In the end he has learnt to say no comment.

Kama mnaweza tafuta gazeti la Raia Mwema la wiki hii msome makala ya Joseph Mihangwa kuhusu mzee wetu Kingunge Ngombale Mwiru. Mihangwa amemchambua huyu mzee kwa kirefu sana kwa vile anamfahamu vizuri tangu Mihangwa akiwa kada wa CCM. Huyu mzee inaonekana ana undumila kuwili (hypocrite). Nadhani in the absence of Mwalimu, Kingunge thinks he can fill the void lakini inaonekana wazi kwamba hawezi kwa sababu he is normally on the wrong side. Ni bahati mbaya kwamba atakumbukwa kwa haya ya lala salama katika maisha yake ambayo si mazuri hasa ukumbatiaji wake wa ufisadi. What a shame!
 
Cardinal Pengo,

Mie ni muumini wa Moravian Church na kwa hiyo nakuwa PROTESTANT. Ila siku zote siamini MAJENGO wala WATU. Kwa maana hii huwa sijali kama huyu ni kiongozi wa kanisa langu au sivyo. Sijali kama ni Muislaam au Mpagani. Huwa naangalia watu kwa matendo yao na maneno yao.

Nimekuwa MPINZANI mkubwa sana wa viongozi wa dini na kuwaita WALA VYA BURE. Mlituacha KONDOO wa Mungu kwenye malisho na kuwa mmeyafumbia haya mambo kwa muda mrefu. Nchi imeuzwa, imeliwa na wameiba kiasi cha kutosha. Mzee Mwanakijiji alipiga kelele kwenu bila mafanikio.

Sintauliza mlikuwa wapi ila lazima niseme kuwa kama nyie wakuu wetu wa dini mkiamua kulifuatilia hili, basi ninaamini mabadiliko ya kweli yatatokea. Kusubiri hadi CCM imeguke ili mabadiliko aliyoahidi JKNyerere yatokee ni kupoteza muda wakati huo Rostam Azziz na Edward Lowassa wanazidi kuimaliza nchi huku wakifuata nyayo za mtoto mliemlea (alilelewa na masista wa kikatoliki) ndugu Ben Mkapa.

Nina imani viongozi wengine wa dini watafuata nyayo na kuanza kukemea huu uchafu ili hatimaye nchi iweze kurudi kwa wananchi wenyewe. Na hapo tu, nyie mrudishe silaha zenu na kurudi kwenye madhabahu/kazi yenu kama alivyofanya Askofu Desmon Tutu wa South Africa.

Kardinal Pengo, hata Papa John Paul II alipoona unyama unaofanywa na Wakoministi kwenye jamii yake ya Wa-slovans (Russia, Czeck-Slowavia, Poland, Bulgaria etc) aliingilia kati na kuanza kuushambulia na mwisho AKAUVUNJA. Walitumia silaha na vitisho ila watu kwa kuamini maneno ya Papa, wala hawakuvunjika moyo. Walipigana hadi Mrusi na masilaha yake mazito, akarudi kwake.

Tuna imani kwamba Mafisadi pamoja na kutumia nguvu za dola, pesa na nyenzo zote zinazowafanya wawepo madarakani, muda wao umekwisha. Kama kweli mmekuja kutusaidia kupigana hii vita na MAFISADI, basi lazima niseme kuwa mmetimiza wajibu wenu haswaa. Nguvu ya viongozi wa dini ni kubwa kuliko vyama vya upinzani au waandishi wa habari. Kwenu nyie kila fisadi atagwaya.

Mungu akubarikini na kukupa busara kuongoza kondoo waliopotezwa na VIRANJA wao.
Endeleeni kuwa WACHUNGAJI wema na si wachungaji wa MAFISADI.

Mungu Ibariki Tanzania.
 
..mimi nasubiri huo waraka wa kina Shekhe Ponda utoke halafu tuone kama Kingunge atauchana kama alivyofanya kwa waraka wa Kanisa Katoliki.

..pia tuone kama Makwaia Kuhenga ataandaa program ya kuwashambulia kina Shekhe Ponda kama alivyowashambulia Wakatoliki.

..halafu tuone tena kama Makwaia Kuhenga ataandika makala ktk gazeti la serikali Daily News akiwashambulia Shekhe Ponda na Waislamu wenzake.
 
Waislam wamezindua waraka wao (wao wanauita MUONGOZO). HAPA CHINI NI BAADHI YA KURASA ZA WARAKA HUO.
 
Bravo his Eminence Policarp Cardinal Pengo for your eloquent homily during the burial of the late Archbishop Anthony Mayalla. People like Hon. Aloyse Kimaro who have acquired large pieces of land amidst peasants without land and yet identifying themselves as corruption crusaders are not honest and sincere.

What a spin!!!

omarilyas
 
Mkoministi, mzee wa Ubungo terminal kaufyata, tehe, tehe
 
Kingunge....

Sio sahihi kwa kanisa kujihusisha na siasa. (Hapa uko right 100%)

Lakini, nashindwa kutetea hatua ya kuingiza mahakama ya kadhi kwenye ile election manifesto. Chama kilikosea kuahidi kuanzisha mahakama hizi pindi kitaposhika madaraka. Hili ni kosa, chama kimefanya kosa na kanisa wametumia kosa hili na wao kuiingilia serikali.

No comments (kwa maongezi ya kwenye simu ni sawa lakini inabidi kukiri ilikuwa makosa kuahidi mahakama za kadhi)

Ushauri:

- Chama/Serikali ikiri short sight kwenye hili na itumie kosa hili kuhakikisha kitu kama hiki hakijirudii katika historia. Utawala wa demokrasia unajali majority lakini tujenge utawala wa sheria. Isifike mahali kwa sababu kwenye bunge majority ni watu fulani basi wote tuburuzwe.

- Kingunge, you are man of principles from those days. Admit the short sight and again put your foot down in criticizing any religious institution from meddling into political arena.
 
- Hivi Chiligati, Kusila na Makamba wako wapi wamjibu Pengo tuone kama wana ubavu! Waje wamsomee ilani ya chama na sera zake kama wanaweza, maana huyu Mwanaume ameongea mbele ya baba zao mafisadi, tena wote wawili, saafi sana.

- Chiligati na Makamba, jaribuni basi kugusa hapo kwa Pengo kama mna ubavu!

Respect.


FMEs!
 
- Hivi Chiligati, Kusila na Makamba wako wapi wamjibu Pengo tuone kama wana ubavu! Waje wamsomee ilani ya chama na sera zake kama wanaweza, maana huyu Mwanaume ameongea mbele ya baba zao mafisadi, tena wote wawili, saafi sana.

- Chiligati na Makamba, jaribuni basi kugusa hapo kwa Pengo kama mna ubavu!

Respect.


FMEs!

sasa ukiambiwa live ukweli utakuwa na neno? unajuwa kwa watu wajanja ndiyo huyu maana angeitisha mkutano na waandishi wa habari,waandishi wangepindisha mistari kadhaa na kuwapa akina chilingati nafasi ya kujibu.

Lakini kawasubiria wakaingia kwenye kumi na nane zake kashusha kitufe tufuuuuuu.
Ngoma zote zimetulia tuli kama hazikusikia kitu
 
halafu nasikia JK hakuitwa pale mwanza kwenye yale mazishi ya Askofu Mayala
 
halafu nasikia JK hakuitwa pale mwanza kwenye yale mazishi ya Askofu Mayala

kwenye msiba huwa hatuitwi ,tunajipeleka wenyewe kutokana na jinsi msiba ulivyokugusa.Ama na tamaduni zetu zilivyo
 
kwenye msiba huwa hatuitwi ,tunajipeleka wenyewe kutokana na jinsi msiba ulivyokugusa.Ama na tamaduni zetu zilivyo

Mkamap bwana naona umemshukia jamaa hapa .

Pengo habari hapa Roma wanazijua .Huwa hasemi semi .Lakini anajua la kusema .Sasa nadhani Mkapa alikuwa akidhani mtu wa home basi hatasema mbele yake .JK hana uwezo wa kuelewa maongezi yale ya Pengo huo ndiyo ukweli .Alizoea lugha majukwani pale pazito .Kingunge alisema Nchi haiwezi na Serikali haitavumilia.Haya JK ambaye ni serikali imepewa LIVE aamue sasa kumwita polisi ahojiwe ama andikeni barua kumwambia serikali inataka kwa lazima kuondoe waraka .Kazi kubwa mno
 
nadhani tusubiri katika hotuba ya mwisho wa mwezi ya mkulu kama atarespond!
 
Mzee Kingunge atazamwe kwa makini mno, naona 'upstairs' kwake kuna kasoro! Mambo ya mahakama ya kadhi yalivyoligawa taifa kwake sio issue na ndiye aliyeyaingiza kwenye ilani ya chama huku akijua kuwa nchi yetu haina dini na serikali kujihusisha na dini ni kuvunja katiba! Haya ya waraka wa wakatoliki pekee ameya-isolate kwamba 'yanaharibu umoja wa kitaifa.' Hivi Kingunge elimu yake kasomea wapi jamani? Au kwa kuwa umri ndio umefikia saa kumi na moja jioni ndio thinking capacity ina-operate in a reverse direction?
 
Back
Top Bottom