No Mercy: Mbeya City tunakuja kuchukua Point 3

No Mercy: Mbeya City tunakuja kuchukua Point 3

sembo

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
4,350
Reaction score
3,451
Na hizi ndo sababu;

1. Wachezaji kuikacha Timu
Katika msimu wa 2013/14, Mbeya City ilikua miongoni mwa Timu zilizoonesha kandanda murua sana.. ikiwa ni msimu wake wa kwanza katika VPL. Kandanda hilo lilitokana na juhudi kubwa walizokua wakionesha vijana waliokabidhiwa Jukumu la kuivusha Timu.
Ikiwa imepita takribani misimu 2 tangu tuwe na Mbeya City katika VPL.. robo 3 ya wachezaji waliopandisha daraja na kuifanya iwe gumzo wamehama.. Baadhi yao ni Mwalyanzi, Kaseke, Nonga, Burhani na Mandawa.
17.10.2015.. Simba S.C tutatua Sokoine kuchukua point 3.. maana kama yule Jemedari Mkuu, aliyekua akiongoza mashambulizi ya ardhini, Mwalyanzi tumefika dau lake na sasa yupo kambi yetu.. Unategemea nini tena hapo!?

2. Kuteteleka kwa Timu.. Msimu Huu
Katika msimu wake wa kwanza ndani ya VPL.. Mbeya City ilifanya vyema sana, na kufanikiwa kumaliza ligi ikiwa nafasi ya 3 [Juu ya Simba S.C]. Msimu uliofuata ilianza kwa kujikongoja, japo ilifanikiwa kumaliza ligi ikiwa nafasi ya 4.
Msimu huu, imeanza ligi kwa kushinda 3-0 dhidi ya Ruvu.. Mechi 4 zilizofuata, wamefungwa 3, na kudroo 1.
17.09.2015.. Simba S.C tutatua Sokoine kuchukua point zetu 3.. maana kama Prisons, Toto na Stand United wamejichukulia point.. Simba S.C inayoongozwa na Kocha "mtalamu" Dylan Kerr [Mwenye leseni ya juu kabisa ya ukocha toka UEFA] itashindwaje? Haiwezekani na Haikubaliki.

4. Uwezo wa kuridhibiti "Goli la Mkono"
Viwanja vya Sokoine kilichopo Mbeya, Mkwakwani cha Tanga na Kambarage kilichopo mjini Shinyanga ni vimekua vikilalamikiwa sana na timu mbali mbali zinazoshiriki VPL, kua zimekua zikifanywiwa fitina kubwa sana ili mradi zisiondoke na point hata 1.
17.10.2015.. Simba S.C tutatua Sokoine kuchukua point 3.. maana kama tuliweza kuchukua point 6, Mkwakwani Stadium [fitna zilipozaliwa], tutashindwaje kwa hawa wanaojifunza?! Mbeya City muwe tayari.. Tumejipanga.

4. Kuondoka kwa Juma Mwambusi
Siku chache zilizopita, Kocha Mkuu wa Mbeya City alitimkia Yanga S.C.. Kocha hiyo ndiyo aliipandisha timu ligi kuu.. Mwambusi ndiyo aliijenga timu mpaka ikawa mlima mrefu ambao timu nyingi zimekua zikipata tabu kufika kileleni.. sana sana kwa timu za Dar.
Baada ya kuondoka kwa Juma, timu imekabidhiwa kocha msaidizi.
17.10.2015.. Simba S.C tutatua Sokoine, kuchukua point 3.. maana kama Kamanda wa Kikosi kasanda.. Unategemea nini hapo!?

Haya maangamizi mithili ya yale yanayofanywa usiku na mchana na vikosi vya Urusi nchini Syria.. Hayataishia kwa Mbeya City tu.. Bali pia kaka yake Tanzania Prisons.. Hawa kuna dozi yao maalumu [nadhani itakua kubwa kuliko tutakayompatia mdogo] tushaiandaa kabisa.. Ni suala la mda tu.

Karibu tena Vodacom Premier League.
 
Unajua mikia ni madogo zetu ndo mana tumewaondolea mwambusi walau wapate sare,wkt mikia ikiumiza kichwa jinsi gani watapata sare,wakimataifa tutawapa uzoefu madogo azam ambao nao ni wakimataifa pale uwanja wa taifa.
 
Mwandishi kidogo unamatatizo unajitahidi kuandika vizuri lakini vitu unavoandika huvijui vizur. Pole wait n see hiyo tar17. Oct siku ya jumamosi kitakachoikuta simba.
 
Mwandishi kidogo unamatatizo unajitahidi kuandika vizuri lakini vitu unavoandika huvijui vizur. Pole wait n see hiyo tar17. Oct siku ya jumamosi kitakachoikuta simba.

Asante Mkuu.. Tukutane hapa mpira ukiisha.
 
wamekuwa wababe wenu tangu timu imeanzishwa labda sasa mtumie pengo la mwambusi.

Unajua mikia ni madogo zetu ndo mana tumewaondolea mwambusi walau wapate sare,wkt mikia ikiumiza kichwa jinsi gani watapata sare,wakimataifa tutawapa uzoefu madogo azam ambao nao ni wakimataifa pale uwanja wa taifa.

Nilitegemea kauli kama hizi.. Ndo mana nikasema "No Mecy".. Jumamosi tunachukua point 3, then katikati ya wiki tunaongeza zingine 3 toka kwa Tanzania Prisons.. Aminini nawaambia, Sokoine tunakomba point zote 6.
 
Wosia wa Juma Mwambusi wakati anawaaga wachezaji wa Mbeya City - wafungeni hao mikia!
 
Wosia wa Juma Mwambusi wakati anawaaga wachezaji wa Mbeya City - wafungeni hao mikia!

Haha.. Mwambusi alikua na uwezo wa kusubiri mpaka mechi dhidi ya Mmyama iishe ndo atimkie Jangwani. Lakini kila alipokua akichekecha, alikua haoni ni kwa jinsi gani ataepukana na kipigo kizito.
Na ndo mana akaona ni heri apoteze kimoja.. Maana Jumamosi Simba itashinda na Timu itakua ya 2 toka mkianii.. Hivyo angetimuliwa na Mbeya City.. Pia kwa Yanga angekua kashafeli interview yake [Kumfunga Mnyama].
 
Tukiwa tunaelekea 17.10.2015, hebu tujikumbushe Msimamo wa VPL mpaka sasa ukoje.
1444743086158.jpg
 
Mbeya city FC, chapa hawa! Hii sasa ni dharau yaani unaelezea as if Simba watakuwa 24 uwanjani na Mbeya city watakuwa 12 uwanjani! Shwaini!
 
Mbeya city FC, chapa hawa! Hii sasa ni dharau yaani unaelezea as if Simba watakuwa 24 uwanjani na Mbeya city watakuwa 12 uwanjani! Shwaini!

Huo ni mtazamo wangu.. Unaweza leta na wewe wako.. Ambao utaonesha jinsi gani hao wachezaji 12 wa Mbeya City watacheza na wachezaji 12 wa Simba S.C [Taifa Kubwa].. Na sijui utakua ni mchezo gani, maana kama ni mpira wa miguu wanaoanza ni 11, na sub huwa hawazidi 3.
 
Nilitegemea kauli kama hizi.. Ndo mana nikasema "No Mecy".. Jumamosi tunachukua point 3, then katikati ya wiki tunaongeza zingine 3 toka kwa Tanzania Prisons.. Aminini nawaambia, Sokoine tunakomba point zote 6.

Polite correction:
'No mercy' and not 'No mecy'
 
TATIZO MIKIA mnaongea sana mnafikiri mpira unachezwa kwa mdomo... kwa taarifa yenu mikia mbeya si salama kwa simba.. historia ipo wazi simba haijawah chukua point 3 kwa mbeya city.. sasa huo ujasiri unaokuja nao endelea kuwa nao.. hata hvyo naona ushaanza kujitetea eti mbeya kuna fitna.. pole sana maana unajua baada ya kichapo utakuja na jibu la kuwa fitina zimefanyika.
 
Hiyo mnayoita historia ni ya mechi 2 hapo Sokoine zilizochezwa na Simba. Na historia zipo ili zivunjwe
 
Back
Top Bottom