sembo
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 4,350
- 3,451
Na hizi ndo sababu;
1. Wachezaji kuikacha Timu
Katika msimu wa 2013/14, Mbeya City ilikua miongoni mwa Timu zilizoonesha kandanda murua sana.. ikiwa ni msimu wake wa kwanza katika VPL. Kandanda hilo lilitokana na juhudi kubwa walizokua wakionesha vijana waliokabidhiwa Jukumu la kuivusha Timu.
Ikiwa imepita takribani misimu 2 tangu tuwe na Mbeya City katika VPL.. robo 3 ya wachezaji waliopandisha daraja na kuifanya iwe gumzo wamehama.. Baadhi yao ni Mwalyanzi, Kaseke, Nonga, Burhani na Mandawa.
17.10.2015.. Simba S.C tutatua Sokoine kuchukua point 3.. maana kama yule Jemedari Mkuu, aliyekua akiongoza mashambulizi ya ardhini, Mwalyanzi tumefika dau lake na sasa yupo kambi yetu.. Unategemea nini tena hapo!?
2. Kuteteleka kwa Timu.. Msimu Huu
Katika msimu wake wa kwanza ndani ya VPL.. Mbeya City ilifanya vyema sana, na kufanikiwa kumaliza ligi ikiwa nafasi ya 3 [Juu ya Simba S.C]. Msimu uliofuata ilianza kwa kujikongoja, japo ilifanikiwa kumaliza ligi ikiwa nafasi ya 4.
Msimu huu, imeanza ligi kwa kushinda 3-0 dhidi ya Ruvu.. Mechi 4 zilizofuata, wamefungwa 3, na kudroo 1.
17.09.2015.. Simba S.C tutatua Sokoine kuchukua point zetu 3.. maana kama Prisons, Toto na Stand United wamejichukulia point.. Simba S.C inayoongozwa na Kocha "mtalamu" Dylan Kerr [Mwenye leseni ya juu kabisa ya ukocha toka UEFA] itashindwaje? Haiwezekani na Haikubaliki.
4. Uwezo wa kuridhibiti "Goli la Mkono"
Viwanja vya Sokoine kilichopo Mbeya, Mkwakwani cha Tanga na Kambarage kilichopo mjini Shinyanga ni vimekua vikilalamikiwa sana na timu mbali mbali zinazoshiriki VPL, kua zimekua zikifanywiwa fitina kubwa sana ili mradi zisiondoke na point hata 1.
17.10.2015.. Simba S.C tutatua Sokoine kuchukua point 3.. maana kama tuliweza kuchukua point 6, Mkwakwani Stadium [fitna zilipozaliwa], tutashindwaje kwa hawa wanaojifunza?! Mbeya City muwe tayari.. Tumejipanga.
4. Kuondoka kwa Juma Mwambusi
Siku chache zilizopita, Kocha Mkuu wa Mbeya City alitimkia Yanga S.C.. Kocha hiyo ndiyo aliipandisha timu ligi kuu.. Mwambusi ndiyo aliijenga timu mpaka ikawa mlima mrefu ambao timu nyingi zimekua zikipata tabu kufika kileleni.. sana sana kwa timu za Dar.
Baada ya kuondoka kwa Juma, timu imekabidhiwa kocha msaidizi.
17.10.2015.. Simba S.C tutatua Sokoine, kuchukua point 3.. maana kama Kamanda wa Kikosi kasanda.. Unategemea nini hapo!?
Haya maangamizi mithili ya yale yanayofanywa usiku na mchana na vikosi vya Urusi nchini Syria.. Hayataishia kwa Mbeya City tu.. Bali pia kaka yake Tanzania Prisons.. Hawa kuna dozi yao maalumu [nadhani itakua kubwa kuliko tutakayompatia mdogo] tushaiandaa kabisa.. Ni suala la mda tu.
Karibu tena Vodacom Premier League.