PreGE2025 No Reform No Election ina logiki lakini mkakati mbovu. Nini kifanyike

PreGE2025 No Reform No Election ina logiki lakini mkakati mbovu. Nini kifanyike

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

tripof

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2024
Posts
853
Reaction score
1,147
Nimekuwa nikifuatilia kwa umakini dhana ya No reform No election na kutafakari iwapo itafanikiwa. Kimsingi kuzuia uchaguzi ni ngumu katika nchi hii bila sapoti ya wananchi, wanachama, vyama vya siasa, viongozi wa dini, NGO nk.

Tathmini yangu ni kuwa zoezi hili ni kama ifuatavyo:

1 zoezi hili ni zuri kwa kuhamasisha kwenye majukwaa, ni tamu kusikiliza ukizingatia kuwa ni kweli michakazo ya uchaguzi imewaumiza sana wapinzani na hata wananchi kwa ujumla.

wana mitizamo hasi kuhusu uchaguzi. Suluhisho linalotolewa la kususia uchaguzi ni gumu na linahitaji elimu na uhamasishaji wa muda mrefu kwa wananchi, ingawa wanafahamu kasoro zilizopo kwenye uchaguzi.

2.Hofu ya wananchi kwa vyombo vya dola inafanya wananchi wasichukue risk ya kutumia nguvu ya umma kuzuia uchaguzi

3 Dhana ya kuzuia uchaguzi kutofanyika siyo shirikishi na wadau wengine na majukumu ya kila mdau ni yapi?

4Hoja hii ni nzuri kwa vile uchaguzi unalalamikiwa na kila mtanzania ila bado suluhisho la kimkakati halipo kwa vile hoja hii ilipaswa ipenyezwe kwa watawala pia.

Aidha semina na makongamano kwa wanataaluma nk kujadili mikakati yangefanyika nchi nzima ingesaidia sana. mwisho CHADEMA isiache kushiriki uchaguzi. Katu!
 
Binafsi naona ni wakati na muda muafaka wa kuhamasisha hii agenda.
Lisu na chadema wanapaswa kuwa wamoja na kukubali maumivu ya sera hii.
Kwa kuwa ni tendo jema ninauhakika watavuna mema.
Ikiwa kila mtu na kila taasisi anaona umuhimu na uhitaji wao jambo hili lakini hakuna wa kuchukua hatua.
Basi ni sahihi kwa chadema kuchukua hatua maana ndio waathirika wa moja kwa moja wa uchaguzi wa nchi hii.
Wananchi watanzania, taasisi za dini na NGO kwa asili yao ukisema uwasubiri unaweza kusubiri hadi elfu mbili na Mia mbili.
Ni Bora wapoteze nafasi lakini waweke msingi ambao Mungu mwenyewe atakuja namna ya kuwalipia
 
Itafika siku itawezekana Tuu.Hivi Sasa Kuna walimu wasio na Ajira(NETO),Hawa nao wasipuuzwe.litakuja kundi la waganga wasio na ajira nk,nk,nk.
Hapo ndipo tutaungana tuu."Shida,dhiki,na mateso vitatuunganisha tuu" siku si nyingi.🤣🤣🤣🤣🤣
 
Uhamasishaji uendelee Nchi nzima na Mabalozi wa nchi za EU nk. wafikishiwe Ngo's na Taasisi za kutetea Demokrasia na HAKI za Binadamu wafikishiwe.

Wakizidi kutia pamba masikioni yakija kubumbuluka wao ndio wakulaumu.
 
Mpaka mda huu wakushiriki uchaguzi bila reforms tiyari anakua batili na kama ndivyo atiambia nini Dunia achana na wananchi.
Hii ngoma chadema wamekabia juu sana , ccm ikisimama nchali ikikaa nchali. Ukilazimisha ni batili ,mpaka wakumi wananchi plus jumuia za kimataifa no reforms no election ,itakua kiganjani, unachomokaje?
 
Lissu inabidi aanze kuongelea pia maisha magumu ya Watanzania ya kila siku kwenye kila mikutano yake kama heche atapata kuungwa mkono zaidi.
 
Iko vizuri tu mbona, CHADEMA wanaongea ugunduzi na uzoefu wa chaguzi zilizopita na kuhamasisha. Waamuzi wa No reforms No election ni wapigakura wanaojitambua wasiorubuniwa na vyama. :KasugaYeah:
 
Naiombea sana Hii No reforms No Election. Lisu atashinda HAKIKA
 
Lissu inabidi aanze kuongelea pia maisha magumu ya Watanzania ya kila siku kwenye kila mikutano yake kama heche atapata kuungwa mkono zaidi.
Hiyo kazi anayo Makam / mwenyekiti chama Taifa Heche au hufatilii,? Chadema wamejipanga
 
Wananchi hasa wa hali ya chini washaelewa ambao ndiyo main target.
No reform ishakamata mwendo...tukutane October.
Mwaka huu mtahonga kila raia ili akapige kura kama mna hela hizo
 
Back
Top Bottom