PreGE2025 No Reform No Election (NORENE) kuwasilishwa kwa lugha ajinabi ni kikwazo

PreGE2025 No Reform No Election (NORENE) kuwasilishwa kwa lugha ajinabi ni kikwazo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

DustBin

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2021
Posts
628
Reaction score
609
Habarini wakuu

Suala la Chadema kuja na kauli mbiu ya No Reform No Election (NORENE) imetafrisiwa na wananchi wadadisi wa mambo kuwa Chadema wamekujanayo kutoka ng'ambo, mbaya zaidi wamesahau hata kubadilisha na kuiweka kwenye lugha mama.

Kuna kitu kimoja ambacho Chadema hujikwaa (technical error) ni kudhani kuwa wananchi wote Tanzania ni werevu, kiasi ambacho hujikuta wanakosa kuwafikia wananchi wengi kwenye masuala yao.

Hii kauli mbiu wangeiweka kwenye lugha ya wenyeji ingepata msaada wa kuisukumu na kuwafikia wengi, lakini hii lugha ya kando iliyotumika imewafanya wengi waamini wameitoa nje kama ni maagizo kutoka huko, na ndio maana imewasilishwa kwa lugha ya hao walioiandaa.
 
Back
Top Bottom