PreGE2025 ‘No Reforms No Election si Siasa, Ni Falsafa ya Uasi Halali – Hii Ndio Siri Watawala Hawataki Uijue!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

its MalekoGJ

Senior Member
Joined
Aug 27, 2020
Posts
136
Reaction score
292
NO REFORMS NO ELECTION Si Siasa, Ni Falsafa ya Uasi Halali – Hii Ndio Siri Watawala Hawataki Uijue!"

Na

Maleko GJ

Watanzania wanaamka. Kauli ya ‘No Reforms No Election’ ya CHADEMA siyo malalamiko ya kisiasa bali ni kilio cha kizazi kinachotaka haki, usawa na uwajibikaji. Lakini je, kauli hii ina mizizi ya kifalsafa? Inaruhusiwa kikatiba? Je, ni uasi au ni ukombozi?

Kupiga kura bila mabadiliko ni sawa na kutia saini udhalilishaji wako mwenyewe. Karibu kwenye uchambuzi mzito.
🧵

1.Unadhani CHADEMA walikurupuka kusema No Reforms No Election?
La hasha.
Kauli hii ni zao la fikra za muda mrefu – na inakubalika kwa wanafalsafa wa dunia nzima.
Leo tutapitia:
– Rousseau
– Hobbes
– Machiavelli
– Katiba ya Tanzania
– Uhalali wa kumsusia mnyanyasaji wa kisiasa

2.Rousseau: "People give power, and people can take it back."
Katika The Social Contract, Rousseau anaweka wazi:
Serikali ni mkataba kati ya watawala na watawaliwa.
Ukitenguka, wananchi hawana sababu ya kuendelea kutii.

No Reforms No Election = Wananchi wanajitoa kwenye mkataba wa udanganyifu.

3.Kama uchaguzi siyo huru, hakuna maana ya kuendelea kushiriki.
Huo si uchaguzi, ni maigizo.
Ni legitimacy theatre – kuhalalisha wizi wa mamlaka kwa kivuli cha kura.

Rousseau angeuliza: “Je, kuna general will kweli hapo, au ni mwelekeo wa kikundi?”
CHADEMA wanasema: hapana.

4.Hobbes: "Fear is the glue of society, but not fear of rulers – fear of chaos."
Katika Leviathan, Hobbes alihofia machafuko.
Lakini pia alieleza wazi: Serikali ikishindwa kulinda usalama na usawa – haina tena mamlaka ya kutawala.

Serikali inayosababisha hofu ya chaguzi ni hatari kuliko machafuko yenyewe.

5.Hobbes angekemea hali ambayo:
– Vyama vya upinzani vinapigwa marufuku
– Waangalizi wa uchaguzi wanazuiwa
– Polisi wanatisha wapiga kura
– Mahakama zipo kimya

Amani haipo kama inategemea ukimya wa waliodhulumiwa.
“No Reforms No Election” ni kutafuta amani ya kweli.

6.Machiavelli: “People forget injuries slowly, but revenge comes swiftly.”
Katika The Prince, Machiavelli alieleza kuwa watawala wanapaswa kuwa werevu – kusoma dalili za mabadiliko na kujipanga.
La sivyo, hasira ya wananchi hujenga moto wa mapinduzi.

7.CHADEMA wanasema: hatuwezi kuendelea kupiga kura kwenye mfumo uleule unaotunyonga.
Hii si siasa ya kawaida – ni hoja ya kimaadili.
Tusisahau: hata Machiavelli alisema… hakuna dola imara inayojengwa juu ya udanganyifu wa kudumu.

8.Sasa tuingie kwenye Katiba ya Tanzania...

Ibara ya 8(1):

“Mamlaka na nguvu zote juu ya mambo yote ya Tanzania ni za wananchi…”

Ibara ya 20:

“Kila mtu anayo haki ya kukusanyika na kushirikiana kwa hiari na watu wengine.”

Kwa mantiki hiyo, wananchi wanayo haki ya kupinga mfumo, hata kwa kumsusia.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

9.Uasi ni nini?
Si lazima iwe bunduki na moto.
Uasi wa karne ya 21 ni:
– Kususia uchaguzi haramu
– Kuandamana kwa amani
– Kutoa taarifa zenye kufumbua macho
– Kulinda kura yako kwa kuikataa ikigeuzwa silaha ya udhalilishaji

10.“No Reforms No Election” = Uasi wa Kikatiba
Uasi wa hoja
Uasi wa maarifa
Uasi wa kizazi kipya chenye uwezo wa kusoma, kuelewa na kuchambua historia ya mateso.

11.Mabadiliko hayaji kwa hisani ya watawala.
– Hayaji kwa kuomba omba.
– Hayaji kwa kupiga magoti.
– Hayaji kwa kupiga kura kwenye mfuko ulioshonwa.

Mabadiliko huletwa na sauti moja ya kukataa kushiriki mchezo wa kishetani unaoitwa "uchaguzi".

12.Tanzania ya leo si nchi masikini wa fikra.
– Kuna vijana wanaosoma Machiavelli mitandaoni.
– Kuna watu wanaotafsiri Rousseau kwenye WhatsApp.
– Kuna wapiga kura wanaomiliki akili timamu.

Kauli ya CHADEMA ni kielelezo cha kizazi kinachojua kilichopotea – na kinachokitaka.

13.Kushiriki uchaguzi usio na mabadiliko ni kama kuingia kwenye ndoa ya manyanyaso kwa hiari.
Unakubali kupigwa.
Unakubali kudhalilishwa.
Unakubali kuambiwa "utashinda safari hii", halafu unaibiwa tena.

Rousseau would call that madness.

14.Uchaguzi siyo utamaduni tu – ni ibada ya kisiasa.
Na ibada ikichafuka, hakuna haja ya kuendelea kuiabudu.
CHADEMA wanasema: tufunge mpaka mfumo utakasike.

15.No Reforms No Election siyo msimamo wa kisiasa – ni falsafa ya ukombozi.
– Rousseau anaunga mkono.
– Hobbes anaelewa.
– Machiavelli anatoa tahadhari.
– Katiba ya Tanzania inaruhusu.

Mabadiliko hayaji kwa kupiga kura bila mabadiliko.

No Reforms No Election” siyo kibwagizo cha kisiasa—ni sauti ya kihistoria, yenye mizizi ya kifalsafa, inayokumbusha watawala kuwa mamlaka si zawadi—ni mkataba. Na mkataba ukivunjwa, watu hawana budi kusimama.
 
Badala ya kujibu hoja zilibebwa na Falsafa wanadhani mabomu ndio yatakayo fifisha ukweli.

Chadems imesimama sehemu sahihi na msingi wake chini ya Lisu ni imara sana maana ni ukweli na haki.

Mungu hamuachi mwenye haki kamwe
 
Back
Top Bottom