PostGE2025 No Reforms No Election yafanikiwa, Umma umeukataa uchaguzi feki

PostGE2025 No Reforms No Election yafanikiwa, Umma umeukataa uchaguzi feki

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
17,047
Reaction score
63,206
Ni dhahiri wananchi wameukataa uchaguzi feki, wengi hawakujitokeza kwenda kupiga kura na maelfu waliingia barabarani kuandamana kupinga uchaguzi huo na kudai haki.

Kilichofanyika ni kumtangaza yule mama kushinda kwa kura ambazo kimsingi hazikuwepo bali ni magumashi tu.
Kwa sasa huyo mama anatawala nchi hii kwa msaada wa mtutu wa bunduki na si kwa ridhaa ya wananchi.

Kimsingi Samia alipindua katiba inayosema kuwa uongozi wa nchi utatokana na ridhaa ya wananchi na si vinginevyo. Unfortunately yule mama hakupata ridhaa ya wananchi bali amewekwa pale kwa msaada wa Majeshi na Tume iliyotangaza matokeo feki.

Unaweza kujiuliza kama Jeshi lilitangaza shughuli za serikali zisimame ndani ya siku zile nne, Je Tume iliwezaje kuendelea na shughuli zake za kutangaza matokeo?. Hii maana yake ni kuwa kila kitu nchini kilisiamama ikiwemo hata mahakama ila tu eti tume yenyewe iliweza kuendelea na shughuli zake. Hili liliwezekanaje kama siyo Jeshi kushiriki kwenye kumsimika mtawala haramu?

Wasimamizi wa kimataifa wa uchaguzi wamesema kuwa bongo hakukuwa na uchaguzi bali maigizo.

Kwa hiyo ni dhahiri Wananchi waliosema NO REFORMS NO ELECTION wamefanikiwa sana. Hakukuwa na uchaguzi pale bali mapinduzi dhidi ya ridhaa ya umma.
 
Msimamo wetu wa kuendelea kutokumtambua Samuya kama Rais wetu bado uko pale pale .
 
Kiongozi asiye na ridhaa ya wananchi
Na alivyo wa ajabu ,bado anaendelea kuwakwaza hao waliyomkataa hadharani, anaamini vyombo vya dola watu ambao kimsingi wametokana na jamii hiyo hiyo anayoibagaza 🤣🤣 sijui anawaza kwa kutumia kiungo gani cha mwili.
 
Alafu bila aibu baada ya kuapishwa eti anasema turudi kama kawaida. How can we return to normal wakati tumefiwa na wadogo zetu na ndugu zetu na haujatupa majivu??!
 
Rais aliyepatikana kwa njia feki hana moral authority ya kusimamia maadili ya utumishi wa umma, kupiga vita ufisadi, kukemea rushwa na kumuwajibisha yeyote kwenye mambo ya maadili, maana rais huyo kapatikana kinyume cha maadili.
 
Dakika za jioooooni NRNE ikaenda kupiga counter-attack ya kibabe na hawaamini macho yao.
 
Back
Top Bottom