No reforms, no elections’ yawaweka Chadema njiapanda.
Kampeni inayoratibiwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ya ‘No reforms, no elections’ ikimaanisha “Bila mabadiliko, hakuna uchaguzi”, imewaweka njiapanda baadhi ya viongozi na makada wa chama hicho.
Wanaobaki njiapanda, ni makada ambao kwa namna moja au nyingine wana nia ya kugombea katika uchaguzi mkuu Oktoba 2025 kusaka udiwani, ubunge na hata urais, ambao wanaingia hofu ya kukosa fursa hiyo.
Makada hao hawajui iwapo wajiandae kujitosa kwenye kinyang’anyiro hicho au waendelee kuwa wasikilizia kauli ya chama iliyosisitizwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Tundu Lissu, kwamba kwa sasa nguvu kubwa zinaelekezwa kwenye kupigania mabadiliko ya mifumo ya kiuchaguzi na si vinginevyo.
Wakati Chadema ikiendelea kujiuliza na kupigania mabadiliko, vyama vingine vinaendelea na maandalizi ya uchaguzi. Mathalan, ACT Wazalendo kimeshatangaza wanaotaka kuwania udiwani, ubunge, uwakilishi na urais wajitokeze na kutangaza nia.
Tayari Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othuman Masoud ameweka nia kuwania urais Zanzibar na Kiongozi wa chama hicho, Dorothy Semu ametamgaza kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Chama tawala CCM kimekwishapitisha wagombea wake wa uraia; Rais Samia Suluhu Hassan (muungano) na Dk Hussein Ali Mwinyi (Zanzibar). Dk Emmanuel Nchimbi amepitishwa kuwa mgombea mwenza wa Rais wa Tanzania.
Msimamo wa Chadema
Kwa nyakati tofauti Lissu aliyeshika wadhifa huo Januari 22, 2025, amekuwa akisisitiza dhana hiyo, kuwa iwapo hakutakuwa na mabadiliko kwenye mfumo wa kisheria, Chadema itafanya kila linalowezekana kuhakikisha uchaguzi haufanyiki.
“Hatuzungumzii kususuia uchaguzi, hatutasusia bali tutaenda kuwaambia Watanzania, jumuiya ya kimataifa na walimwengu kwamba kama CCM na Serikali hawako tayari kufanya mabadiliko kwenye mfumo wa uchaguzi ili kuwepo chaguzi huru na haki, uchaguzi wa mwaka huu usifanyike kabisa,” alisema Lissu katika moja ya hotuba zake.
Soma Pia: Pre GE2025 - Tundu Lissu: Kauli ya No Reform No Election hatujasema tunasusia Uchaguzi. Tutaongea na Rais Samia lugha atakayoielewa
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Majibu ya Serikali
Msimamo huo umemwibua Katibu Mkuu, Wizara ya Katiba na Sheria, Eliakim Maswi ambaye anasema kwa ajuavyo yeye mageuzi yalikwishafanyika.
“Mimi nimeona mageuzi yapo, sasa kama mwenzangu hayaoni, hata ukitwambia hakuna uchaguzi, wewe unayezuia kwani ndiye unayechagua pekee? Uchaguzi unafanywa na wananchi na ndio wanaopiga kura,” amesema Maswi.
Source: gazeti la mwananchi mtandaoni