MANAKE MKARI
JF-Expert Member
- Jan 25, 2011
- 299
- 240
Gari aina ya Noah (old model – SR40) inakuwa kama inatetemeka /kushtuka na kuzima ikiwa inatembea kwenye mwendo mdogo (RPM ikiwa chini ya 1,000).Inatokea mfano ukisharuka tuta wakati wa kukanyaga mafuta. Ikizima unawasha na unaendelea na safari. Ukiwasha ‘’silensa’’ ipo vizuri na hakuna ‘’misi’’ yoyote.Mafundi bado hawajaweza kujua tatizo lipo wapi. Naomba kama kuna aliyewahi kupata hili tatizo asaidie jinsi lilivyotatuliwa au fundi mzuri aliyepo Dar.