Uchaguzi 2020 Noel Msigwa: Tume ya Taifa ya Uchaguzi mlishampanga mshindi wa kiti cha Urais?

Watanzania wanatazama na kwa umati ninaouona kwenye mikutano ya Lissu Ni wazi hata tume imbebe vipi Magufuli bado ataachwa kwa kura za Tsunami. Lissu atawapasha na Kama wanataka haki wamuite pia Magufuli aseme kwa Nini atoe hela kipindi hiki Cha kampeni
 
[emoji706][emoji706][emoji706][emoji706][emoji706][emoji706][emoji706][emoji706][emoji706][emoji706][emoji706][emoji706][emoji706][emoji706]

Sent using Jamii Forums mobile app by My phone

[/url] Eti nabakia Africa. [/url]
 
Kuna kauli tata nyingi toka kwa mtukufu magufuli mojawapo ni ile ya kusema Lisu katumwa na mabeberu , Tumeccm wamuhoji mtukufu magufuli aseme na kuthibitisha hao mabeberu ni akina nani?
 
Zile karatasi zenyewe ni maelekezo yameandikwa tayari yaliotoka CCM, bwana mkurugenzi alikua anasoma tu. Hata ukimwangalia usoni unaona nafsi inavyo msuta.
Zile karatasi ni akili ya Polepole imetumika kujibu hoja za Lissu kupitia NEC.
NECCCM Tumeccm hawafanyi kazi kwa mjibu wa katiba na Sheria sasa bali wanafanya kazi kwa mjibu wa zidumu fikra zisizo sahihi za mtukufu mwenyekiti wa CCM pamoja na polepole.
 
Hiyo tume viongozi wake hawana tofauti na wauzaji papa wa kimboka
 
Mnaofikiria KITOPIAN mko hivi, mgombea wa ccm kila kukichaa anatoa Rushwa kwakuwapigia mawaziri na wkurugenzi wapelekee PESA majimboni!!! Je Nec wamemuita? Endeleeni kupalia mkaaa wa Moto kwenye chungu kitakaposhika joto mtajua...!!
Hata machinga kawapa Rushwa kupitia vitambulisho vya machinga, Tumeccm wamesahau kuwa watanzania siyo wajinga kiasi wanavyofikiri
 
Tumeccm NECCCM wanazidi kujidhalilisha na sasa Duniani kote wamejua tarehe 28 October hakutakuwa na uchaguzi huru na haki bali maigizo tu kwani tayari Tumeccm wanayo matokeo mifukoni mwao.
 
Nakubaliana na mwandishi maana Ukimsikiliza Mahera msingi wa mashtaka yamejengwa kwamba Lissu alisema atashinda na hatakubali wizi wa kura
Twjwa kwanini uchaguzi wa Zanzibar ulifutwa then utaelewa
 
Mkurugenzi mpya wa NEC, Charles Wilson Mahera, ni top CCM ndani ya NEC. Huu mchezo haulisaidii Taifa letu.

Dk. Wilson Mahera Charles aliyeteuliwa kuwa Mkurugenzi wa NEC mwaka 2019 ni mwanachama wa CCM, aligombea ujumbe wa halmashauri kuu ya CCM (NEC) kutoka Musoma. Pia ni kati ya DEDs walioorodheshwa Mahakamani kama DEDs ambao ni wanachama wa CCM katika kesi ya kupinga DEDs kusimamia uchaguzi.

Kwa nini MAGUFULI anaharubu nchi yetu iliyojengwa kwa misingi ya upendo, umaja na amani na waasisi wetu akina Julius Nyerere na Karume kwa ajili ya KUNG'ANGANIA IKULU?

Dr Wilson Charles Mahera is TOXIC hawezi kuwa MWAMUZI kwa vile ana MASILAHI na CCM. Hii ni against principle ya NEMO JUDEX EN CAUSA SUA
 
Chombo binafsi cha CCM kinachoitwa NECCCM chenye maelekezo tokea kwa polepole wa CCM eti kinaenda kumhoji Tundu? haya ndiyo maajabu yaliyopo Tanzania na hayapo popote Duniani
 
CCM wanasema watashinda kwa kishindo, wamefanya na utafiti wakaona uchaguzi ungefanyika jtano iliyopita wangeshinda kwa asilimia 89%. Sasa hawa wanatoa na takwimu kabisa, tume hailioni hilo? Tume acha siasa ziendelee.
 
Tumeccm NECCCM hawafanyi kazi kwa mjibu wa Sheria na katiba bali wanafanya kazi kwa mujibu wa maelekezo ya polepole aliyetumwa na mtukufu mwenyekiti wa CCM
 
CCM wanasema watashinda kwa kishindo, wamefanya na utafiti wakaona uchaguzi ungefanyika jtano iliyopita wangeshinda kwa asilimia 89%. Sasa hawa wanatoa na takwimu kabisa, tume hailioni hilo? Tume acha siasa ziendelee.
Tumeccm NECCCM wamejitoa fahamu zote hawaoni uovu mapungufu ya CCM bali wamekariri uonevu waliotumwa na CCM kuwafanyizia wapinzani
 
Tume ya CCM inaenda kuwahoji chadema wapi na wapi? Kuna Haki hapo?
 
Hakuna tume hapo,ni kamati ya ushindi ya sisiem.Watanzania tunapaswa kumwelewa Lissu anaposema TUTAWAGAWANA wakijaribu kuchezea kura zetu.Hiyo ndiyo dawa yao maana haitatokea KAMWE hawa watu wakakubali kushindwa.
 
Sijawahi kuona mkurugenzi kilaza Kama huyu yaani ajui hata kazi za tume Ni zipi alishindwa hata kuedit hio barua aliyiandikiwa na polepole ana elimu gani huyu kibaraka mbona Ni mweupe Sana kuhusu Sheria za uchaguzi
Ukabila tu unamsumbua...
MAHERA ni Msukuma kama Magufuli
 
Hiyo siyo tume huru,hivi maana ya chafuzi nini?
 

Mwalimu! Umetoa hoja nyingi sana, lakini nikueleze tu kwa kifupi. Kwanza: Fanya mawasiliano na Tundu Lissu au Uongozi wa Chadema ili ujue bayana ni makosa yepi yanayomfikisha mbele ya Kamati ya maadili mgombea wako. Pili: Kuhusu TBC kutangaza LIVE mikutano ya CCM bado sioni kama inamashiko sanaa kwani Mnajua mlichowafanyia hao TBC siku ya kwanza ya uzinduzi wa Kampeni zenu, na waswahili tunausemi, "Ukigongwa na Nyoka ukiguswa na unyasi lazima ushtuke" Mlisha wa jeruhi kwa vitisho hao. Lakini mbona wagombea wengine tunawasikia. Mfano jana nilikua namsikiliza John Shibuda akiunguruma kutokea Maswa. Ila Wenzenu wanaweza hata kuswema TBC isiwarushe lakini hilo lichama ni likubwa lina miliki TV, Redio na Magazeti, Mitndao ya Kijamii na mazaga zaga mengine mbalimbali, lakini TV nyingine nazo zote zitawarusha ukiondoa TBC.

Tatu na Mwisho: Muandalieni vithibitisho Mgombea wenu na si vinginevyo, kulalamika mitandaoni haitoshi jamani. na Huko Jukwaani mumuase awe anaeleza sera za chama chake na nini atatufanyia watanzania.
 
[emoji3][emoji3][emoji3]Yani beberu wa Lisu Amsterdam ambae ni raia wa nje aombe mkurugenzi wa tume kutoka tz ambayo ni nchi huru aondolewe?
Why not? Nyie si mnaonea na kuwachomea ofisi na kuwavua uwakili mawakili wa tz sasa tutatetewa na nani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…