Sasa mtu unajiita wakili msomi alafu unavuliwa uwakili kindezi tu, huo usomi wako ni kwenye social media tuWhy not? Nyie si mnaonea na kuwachomea ofisi na kuwavua uwakili mawakili wa tz sasa tutatetewa na nani?
Mwaka wananchi hawatakubali ushenzi huuTUME in adui wa vyama vya upinzani hasa chadema,kwa tume hii hata chadema wakitapa kura 100%. na ccm 0%.bado mshindi in ccm
Sent from my itel A11 using JamiiForums mobile app
Magufuli hawezi kupata 30% ya kura za uchaguzi wa October 28, 2020.CCM wanasema watashinda kwa kishindo, wamefanya na utafiti wakaona uchaguzi ungefanyika jtano iliyopita wangeshinda kwa asilimia 89%. Sasa hawa wanatoa na takwimu kabisa, tume hailioni hilo? Tume acha siasa ziendelee.
Ha Haaa haaaHiyo tume viongozi wake hawana tofauti na wauzaji papa wa kimboka
Mnaofikiria KITOPIAN mko hivi, mgombea wa ccm kila kukichaa anatoa Rushwa kwakuwapigia mawaziri na wkurugenzi wapelekee PESA majimboni!!! Je Nec wamemuita? Endeleeni kupalia mkaaa wa Moto kwenye chungu kitakaposhika joto mtajua...!!
[/QUOTEKajifunze kuandika kwanza.
Anaandika Mwalimu Noel Msigwa
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imejiaibisha kwa mara nyingine tena. Kumuita mgombea wa Chadema Tundu Lissu kwenye Kamati ya Maadili kumtaka ajieleze kwanini anasema lazima atashinda uchaguzi huu ni wazi Tume hiyo Ina mshindi wake mfukoni ambapo wanapata ukakasi wanaposikia mgombea mwingine akisema atashinda uchaguzi huu.
Inafahamika wazi Tume hiyo ya uchaguzi haiko huru na ilichofanya ni maelekezo tu kutoka Chama Cha Mapinduzi baada ya kutishwa na Kasi kubwa ya na Kasi kubwa ya Mgombea wa Chadema.
Wito wa kumuita Tundu Lissu kwenye Kamati ya Maadili Tarehe 29/9 kumeivua nguo Tume hiyo kwani Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Hamphrey Polepole siku moja kabla alishaielekeza Tume hiyo inapaswa kumfanyia nini mgombea wa Chadema.
Habari za ndani za Tume ya Taifa ya Uchaguzi zinasema tayari CCM ilishawaelekeza kumzuia mgombea Urais wa Chadema kuendelea na kampeni kwa siku 14 kwa hiyo wanachofanya Sasa ni mazingaombwe tu na Utekelezaji wa maelekezo ya CCM.Hata kabla ya Mkurugenzi wa NEC kujitokeza hadharani jana kumuita Tundu Lissu kwenye Kamati ya Maadili Tarehe 29 habari zilishavuja kwamba walishafikia maamuzi na CCM kuzuia kampeni za Lissu kwa siku hizo 14 kuanzia tarehe 1 October.
NEC imeshindwa kuficha mapenzi yake kwa CCM kwani Mgombea wa CCM na chama chake wamekuwa wakivunja waziwazi maadili ya Uchaguzi lakini hawakuwahi kukemewa.
Mgombea wa Urais wa CCM amekuwa akitoa ahadi za Ujenzi wa Barabara Kama Rais na anapiga simu kuelekeza mawaziri katikati ya mikutano ya kampeni kinyume kabisa na Maadili ya Uchaguzi.
Mgombea wa Urais wa CCM amekuwa akisema katika kampeni zake kamwe hatapeleka Maendeleo kwenye Jimbo au Kata itakayochagua mpinzani kinyume kabisa na Maadili ya Uchaguzi.
Tume inasema Lissu kosa lake ni kusema atashinda Urais lakini Tume hiyo haijaona Kama mgombea wa CCM kusema watu hatawapelekewa maendeleo wakichagua mpinzani tayari ni kujitangaza mshindi.
Waziri Mkuu wa Tanzania amekuwa akipita kila Kona ya nchi kufanya kampeni za Mgombea Urais wa CCM kinyume kabisa na Maadili ya Uchaguzi lakini Tume ya Uchaguzi imeweka Pamba masikioni.
Mgombea Urais wa CCM amekuwa akitumia Televisheni ya Taifa kuanzia asubuhi mpaka jioni kujitangaza live mikutano yake ya Kampeni huku wapinzani wake wakikosa Fursa hiyo kinyume kabisa na Maadili ya Uchaguzi lakini Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeweka Pamba madikioni.
Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Humphrey Polepole amekuwa akirushwa Live na Televisheni ya Taifa akiongea na Waandishi wa Habari na amekuwa akimtukana mgombea Urais wa Chadema matusi makubwa yasiyoandikika hapa kinyume kabisa na Maadili ya Uchaguzi lakini Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeweka Pamba Masikioni.
Mpaka ninapoandika hapa wagombea kadhaa wa Upinzani walioenguliwa kwenye uchaguzi hawajapewa taarifa rasmi wanarudishwa au kuondolewa kwenye kinyang'anyiro baada ya kukata rufaa lakini Tume hiyo Wala haijali zaidi ya kumfungulia mashtaka mgombea Urais wa Chadema kwamba kwanini anasema atashinda Urais.
Yapo mengi Sana ya kuandika hapa hayo niliyoweka ni machache tu lakini itoshe kusema Tume hii na CCM hawakujiandaa na Upinzani mkubwa hivi kutoka Chadema ndiyo maana bila aibu wanamshtaki Lissu eti kwanini anasema atashinda Urais.
Hakuna Vurugu yoyote itakayofanyika nchi hii Kama Haki itatendeka katika Uchaguzi huu.Hawa wanaojihami wamepanga kuiba kura na kufanya uhalifu kwenye uchaguzi huu ndiyo maana wanatapatapa wanapoona mgombea akitaka Haki Itendeke.
Nitaandika zaidi tarehe 2/10 baada ya maamuzi ya NEC ya kumzuia mgombea Urais wa Chadema kuendelea na kampeni kwa wiki mbili.
Alisemaje hebu tukumbushe, ukimaliza tukumbushe pia kauli za mgombea wenu akiwa Magu za kuwatisha wapiga kura, za kutoa rushwa kule Nyehunge, Uvinza na Itigi halafu umalizie kwa kutukumbusha yeye tarehe yake pale tume ya maadili imepangwa lini.Kwa hiyo kaitwa kwasababu kasema atashinda? Wote tumemsikia Dk. Mahela hivyo usituletee uongo wako humu. Kamati za maadili zimewekwa kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi kufanya kazi hiyo. Mtulie Lissu akatoe ushahidi wa aliyosema Musoma.
Hivi ukivuna mahindi kinachobaki kimelala ama simama kinaitwaje vileHii siyo tume ya uchaguzi ni tume ya kuwakandamiza wapinzani. Tume imesahau kuwa mgombea wa ccm alipokuwa kigoma alitasema kuwa yeye ndio mshindi wa uchaguzi huu, je tume imechukua hatua gani? Hii tume inaenda kusababisha vurugu kwenye nchi yetu
Asante kumweleza naona alisahauAlisemaje hebu tukumbushe, ukimaliza tukumbushe pia kauli za mgombea wenu akiwa Magu za kuwatisha wapiga kura, za kutoa rushwa kule Nyehunge, Uvinza na Itigi halafu umalizie kwa kutukumbusha yeye tarehe yake pale tume ya maadili imepangwa lini.
Why not? Nyie si mnaonea na kuwachomea ofisi na kuwavua uwakili mawakili wa tz sasa tutatetewa na nani?Sasa mtu unajiita wakili msomi alafu unavuliwa uwakili kindezi tu, huo usomi wako ni kwenye social media tu
Huku mtandaoni hatusikiki labda tufanye maandamano πππMahera aondoke, Mahera aondoke wote tuseme , Mahera aondoke.