Apollo
JF-Expert Member
- May 26, 2011
- 4,920
- 3,240
Kampuni ya Nokia imefanya mabadiliko ya mwonekano wa logo yake. Design ya logo ambayo imekuwa ikitumika tangu mwaka 1966, japo ilikuwa inabadilika kodogo (mwaka 1992, 2006 na 2011); kampuni ya Logo imeamua kuweka logo mpya kabisa ambayo ni tofauti na logo yake ya kawaida.
Nokia ipo katika hatua za kubadili brand yake kabisa, na kuweka usasa na style mpya ambayo itakuwa ni ishara ya kuamua kubadilika. Mkurugenzi Mtendaji Pekka Lundmark amesema Nokia ni kampuni ambayo ina mafanikio makubwa na chap mpya ni ishara ya kutangana mabadiliko makubwa na kwenda na ulimwengu wa kidigitali.
Unaonaje mwonekano wa logo mpya?