Nina laptop yangu Toshiba m50 Window 7 premier. Nilikuwa nikiiwasha inaleta black screen kwa muda na maandishi mengimengi hivi then inawaka, lakini leo imeleta hiyo screen nyeusi na kuandika CD-ROM BOOT PRIORITY ...........NO MEDIUM halafu haijaendelea kuwaka nifanyaje Wakuu?? Je ni nini tatizo hasa?? Naomba ushauri wenu Wakuu.:frusty:
Nitaaanza kwa kujaribu kufafanua kwanza hilo neno CD ROM BOOT PRIORITY....
Kwa kawaida Computer huwa ina kitu kinaitwa BOOTING SEQUENCE PRIORITY(inaweza ikatumika lugha nyingine ya kitaalam zaidi) ila kwa maana nyepesi ni kuwa Unapoiwasha computer yako mtiririko mzima wa system kuweza kuwaka mpaka mahali ambako user wa kaiwada anaweza kuanza kutumia (tunaita Booting systeam) ni huwa wa namna hii....
1. kwanza Computer inapowaka kitu cha kwanza inachofanya ni kudisplay details za mfumo mzima wa computer na uwezo wake ulivyo.....(ndio yale maandishi unayoyaona yanayotokea kwenye black screen(tunaweza kusema inaitwa booting procedure) yale maandishi yanaweza kukuonyesha uwezo na speed ya computer yako vilevile na version y BIOS system yako na Booting procedure hii inatanguliwa na kitu kinachoitwa POST(power on self test)kama kuna failure yoyote ya attached device(mouse keybord,harddisk, RAM,cd rom na hata CMOS battery) basi hapo ndipo utakapokujulisha kuona tatizo liko wapi (mara nyingi ni kwa lugha ya kiufundi zaidi kwa hiyo unaweza usielewa kama sio mtaalam wa maswala hayo hasa kwa kesi ya RAM na HDD)...
ikiwa mashine yako iko sawa basi unaweza ukasikia single beep ...sometimes double beeps(sio kwa computer zote zingine hazitoi Beep) kuashiria everything is OK na computer inaendelea KU load OS(operating system)
BOOTING PROCEDURE NA OS LOADING......
Hints:
OS(operating system) - E.g Windows XP, windows 7, Ubuntu(linux)
Hard disk/hard drive(HDD) - ni kifaa cha kutunzia files na programs zote zinazopatikana kwenye computer.. kwa lugha nyepesi ndio (container) au tumbo la computer... kila unachofanya kinahifadhiwa humo unit yake ni kwa KB,MB,GB,TERA
RAM - Random Access memory - Hapa tunaweza kusema ndio play ground ya kila activities ya computer.. kwa mfano rahisi tunaweza kusema ndio ndio mahali pa kufanyia kazi kwa programs zako (maelezo zaidi chini) unit ni MB
CPU( central proccessing Unit) a.k.CPU clocks a.k.a proccessor - Hiki kifaa ndio BRAIN OF COMPUTER...... idea na mhimili mzima wa computer uko hapa..na ndio sifa ya computer ilipolalia( kama vile kwa ubongo au brain ya mwanadam) pasipo hii computer is consider to be useless(typical dead) NB: ingawa computer ni muuonganiko wa vifaa vinavyotegemeana) hiki ndio kifaa kinachoprocess activities(request) zote zinazoingizwa na ku zidisplay kupitia screen kwa usahihi na kwa wakati muafaka (acuracy and speed) unit ni kuanzia Mhz , Ghz na kuendelea
BIOS (basic input/output system) - it is a set of instruction that tells computer how to start
HOW COMPUTER START UP AND GETTING READY TO USE...
Bila kujali ni aina gani ya OS inatumika ... unapobonyeza kitufe cha ON katika computer yako ... itaanza kufanya POST kuangalia kama kuna missing au defected device yoyote ambayo itaathiri utendaji wake... baada ya kuhakikisha kuwa kila kitu kiko sawa pamoja na setup nzima ya BIOS hapo computer kwa kutumia some integrated programs itaload OS kutoka kwenye HDD na kuipeleka kwenye RAM tayari kwa matumizi(mind u RAM its a play ground)... na hili linafanyika kwa kila program unayofungua... ni lazima iwe loaded kwenye RAM ili uweze kuitumia ... na unapoizima inarudishwa kweney HDD na kuwa saved hapo.. ndio maana hatuzimi Computer kama RADIO au TV kwani kufanya hivyo ni kusababisha LOADED programs zisiwe retained kwenye HDD na kuwa saved hapo(ingawa baadhi ya computer za kisasa zinauwezo wa kurecover demaged files incase power fault occur)
Sasa ikiwa basi computer itagoma kuendelea ku load OS mara baada ya POST kuna sababu mbalimbali iznazoweza kusababisha
1. OS NOT FOUND( had disk fault au imekufa au haipo kabisa au OS haijawa installed)
2. RAM MISSING ( RAM imekufa au haipo kabisa)
3. SYSTEM FILE corrupted ( Files za OS zimekuwa corrupted na zinahitaji kuwa re installed)
4. BIOS SETUP MISCONFIGURED (BIOUS setup zimekuwa misconfigured au corrupted)
na sababu nyingine nyingine nyingi.......................
Hitimisho
kwa kesi ya laptop yako inaonekana kuwa computer imeshindwa kuiona Booting system files za OS yako kutoka kwenye HDD yako... hii inaweza ikasababishwa na kuwa HHD hajatambulika kwenye mashine yako.. (labda laptop ilipata mushlkeli kidogo na kusababisha hadrware error mfano kuigonga au kuanguka au power fault) kwani kwa kawaida ilitakiwa iende kwenye option ya pili (HDD) kutoka kwenye ya kwanza (CD ROM)
kwa kaiwada booting sequence ya computer huanzia 1.CD ROM ---> 2.HDD - 3.NETWORK 4. EXTERNAL MEDIA (sequence hii sio kwa computer zote) ila hizo mbili za kwanza (1. CD ROM ----> HDD) kwamaana ya kuwa computer itaboot kupitia CD ROM ikiwa tu kama kuna BOOTING MEDIA ndani ya CD ROM (kwa mfano WINDOWS XP OS CD, WINDOWS VISTA OS CD) na kama haipo computer itakwenda kwenye option ya pili yaani HDD ... hapo sasa kwa kuwa tayari HDD yako inakuwa installed na OS basi computer ita boot kupitia hapo ( NB: booting kupitia CD ROM ni kwa ajli ya Technical issues tu ndio maana ikawa ya kwanza unaweza ukachange iwe ya pili au ya mwisho... ili computer yako ianzie kwenye HDD moja kwa moja..
CHA KUFANYA
mara nyingi computer inakupa option wakati inawaka (pale kwenye black screen) mfano.. press f1 or f2, or del, or ALT-DEL or SHIFT-F2 or f12 or f10 orCTRL-ALT to enter (BIOS) setup ...(angalia ya kwako imekupa opt ya key ipi ipi kati ya hizo keys) then ukishaingia kwenye BIOS setup tafuta BOOTING sequence then unaweza ukare arange kufuatana na maelekezo ukimaliza save and exit (fuata maelekezo) then computer ita restart.. kama bado rudi kwenye SETUP nenda kajaribu kuload DEFAULT CONFIGURATION" (fuata maelekezo utaona ilipo "default config" kwani BIOS zinatofautiana siwezi sema yako ikoje
NB: wakati mwinginebaadhi ya computer inakataa kuendelea kuload systm files ikiwa kama umeiwasha wakati kuna CD ndani ambayo sio ya Bootable CD... mathalani cd ya music, video na e.t.c... mfano kwa kesi kama yako angalia kama hujasahau cd ambayo sio bootable ndani ya cd rom/ dvd rom....
naaamini nimejaribu kwa mapana yangu...... all the best
Computer ufanyaji kazi wake kwa lugha rahisi tunaweza tukaufananisha na mwili wa binaadam kwa maana ya kuwa viuongo vya mwili vina umuhimu sawa kinapopungua kimoja au kuwa na hitilafu basi madhara ni ya kiasi kilekile...