NORA Aelezea Jinsi Alivyoteswa na Matapeli

NORA Aelezea Jinsi Alivyoteswa na Matapeli

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Posts
13,053
Reaction score
6,304
MWIGIZAJI mkongwe Bongo, Nuru Nassoro ‘Nora' amefunguka kuwa anakerwa na matapeli walioibuka ambao wanawatapeli wasanii wa kike wakiwadanganya kwamba wanawachezesha filamu kumbe ‘changa la macho'.



Nuru Nassoro ‘Nora'.

Akistorisha na paparazi wetu, Nora alisema hivi karibuni alikutwa na mkasa huo baada ya kupigiwa simu na wanaume wawili waliodai kwamba wana filamu yao hivyo wanataka wamchezeshe kama mhusika mkuu (main character) lakini baada ya kukutana nao, mazungumzo yao yalikuwa tofauti.

"Walinikera sana, waliniambia kwamba wanataka kunichezesha filamu lakini nilipoenda kuonana nao walibadili mazungumzo na kuanza kunitaka kimapenzi, ujinga mtupu, niliwakatalia," alisema Nora.
 
Huyu demu alikamua sana kwenye ile movie ya sikitiko langu ...
 
Back
Top Bottom