Northern Dynamo vs Mtibwa Sugar

bagamoyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2010
Posts
24,941
Reaction score
28,869
December 4 , 2018
Victoria Seychelles

CAF Confederation Cup 2018 :
Northern Dynamo vs Mtibwa Sugar


Mtibwa Sugar walivyowasili mjini Victoria ktk visiwa vya Seychelles bahari ya hindi.

Baada ya Mtibwa kuibuka na ushindi mnono wa mabao manne kwa nunge dhidi ya Northern Dynamo nyumbani ktk viwanja vya Chamazi Complex jijini Dar-es-Salaam, Tanzania timu hiyo itaingia uwanjani kucheza mchezo wa pili wa marudiano hapa Seychelles.

Mchezo huo utafanyika leo December 4, 2018 ktk uwanja wa Stade de Linite wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 10,000 uliopo mjini mkuu wa Victoria , Seychelles.
Source : mtibwaofficial
 
Stade de Linite in Victoria, Seychelles
 
04 December 2018
Victoria, Seychelles

Final score :
Northern Dynamo 0 - 1 Mtibwa Sugar

HALF TIME

Northern Dynamo 0 – 0 Mtibwa Sugar



FULL TIME

Northern Dynamo 0 – 1 Mtibwa Sugar (68′ Haruna Chanongo)

AGGREGATES

Northern Dynamo 0 – 5 Mtibwa Sugar

Matokeo ya Mwisho ya Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Kombe La Shirikisho Mtibwa Sugar

Kikosi cha Mtibwa Sugar, kimefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Northern Dynamo katika mchezo wa marudio wa kombe la shirikisho Afrika uliochezwa katika visiwa vya Shelisheli.

Katika mchezo wa kwanza uliochezwa uwanja wa Chamazi, Mtibwa walifanikiwa kushinda kwa mabao 4-0 hivyo mzigo waliokuwa nao Dynamo leo ulikuwa mzito kuweza kufunga mabao 5-0.

Kwa matokeo hayo Mtibwa wanafanikiwa kusonga mbele katika hatua ya kwanza ya michuano hiyo baada ya kufanikiwa kushinda mchezo wa leo ugenini.

Bao la Mtibwa lilifungwa na Haruna Chanongo dakika ya 68 bada ya kipindi cha kwanza kumalizika kwa sare ya bila kufungana.
Source : MTIBWA SUGAR WAWAKALISHA WASHELISHELI NYUMBANI - SALEH JEMBE
 
Ila round ijayo na kampla city council authority lazima wajipange sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…