hapo nini hakieleweki sasa!! not secured means no loan"
mkuu hata mimi sijaelewa,
mleta uzi alitakiwa aeleze,alipokuta ameandikiwa hivyo alipewa ufafanuzi gani
wa sentesi hiyo,ili ajue kwa nini amekosa mkopo.
Kwa mfano mimi najiuliza hivi
walioqualify namaanisha walioandikiwa secured wametimiza vigezo gani?
Ambao hawakuqualify wamepungukiwa na nini?
Lengo la kuandika uzi unaojitosheleza ni kutoa taarifa sahihi kwa wana jf
ili kama kuna samaki wanene wa kutatua tatizo hilo watusaidie maana suala la mikopo si dogo,linagusa watoto na wazazi wao pia.
Naamini jf ni kama msitu mnene ambao una wanyama wakubwa na wadogo,na wote huishi kwa kutegemeana
kwa njia moja au nyingine
Hivyo nashauri waleta nyuzi wajitahidi kutoa ufafanuzi mzuri ili kuwarahisishia wachangiaji kuchangia.
ni hayo tu